Ahmed Ally, Msemaji wa Simba, Mungu anakuona!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,198
25,517
Kuwa Msemaji wa timu, tena kubwa kama Simba au Yanga, si lazima uwe unamwaga porojo na ndoto ambazo si rahisi kutimizika.

Kabla ya mechi ya Al Ahly Benjamin Mkapa, Ahmed Ally aliwaaminisha washabiki na wanachama wa Simba kuwa Ahly anakufa kifo kibaya na HATOKI BENJAMIN MKAPA.

Baada ya kupigwa kimoja cha dakika ya 5, Ahmed Ally sasa amekuja na SIMBA, TIMU YA MAAJABU.Amedai kuwa Simba itaenda kufanya maajabu kule Cairo, Misri. Eti, imeshawahi kufanya maajabu makubwa huko nyuma.

Hadi sasa, Simba ndiye pekee aliyefungwa kwenye awamu ya kwanza ya robo fainali ya ACCL. Tena amepigwa nyumbani...akashindwa hata kutumia mwiko au jengo kujilinda. Washindi wenzake wengine wa pili, akiwemo Yanga, wamepata suluhu nyumbani kwao.

Ahmed Ally, Mungu anakuona. Endelea tu kuwajaza upepo mashabiki na wanachama wa Simba. Ila tambua kuwa Yanga inatinga nusu fainali kwa mechi ya ugenini kwa Madiba...sare yoyote ya magoli inaivusha Yanga...timu ya wananchi!
 
Ahmed Ally anaihujumu timu yetu ya simba. Mashabiki wenzangu tuungane kumuondoa Ahmed Ally na Mwenyekiti Mangungu. Hawa watu wawili ni Yanga dam dam!

Ukiona tu simba imefungwa, basi chanzo kikuu ni Ahmed Ally na Mwenyekiti Mangungu. Haya malalamiko hata shabiki mwenzangu Kalpana anayafahamu.
 
Duh, kuna watu mna vichwa vibovu sana. Yani maneno ya mhamasishaji wewe unachukulia kama scientific fact?

Hivi uliwahi kuona wapi, mchezaji, kocha, mshabiki, msemaji/mhamasishaji anaesema team yake inaenda kufungwa?

Mambo mengine mchukulie kama ni sehemu ya kawaida ya michezo sio kukaza ubongo.
 
1. Kwani anaecheza ni Ahmed Ally?

2. Kwani kocha ni Ahmed Ally?

3. Aliefunga simba ni Ahmed Ally?

4. Kwani kazi ya Ahmed Ally ni nini mpaka unampa lawama zote?

NB: kila mtu atimize majukumu yake tuone panapo vuja.
 
Kubwa jinga la First leg ni timu ambayo haina medals yoyote ya CAF, kwenye orodha hiyo timu zote zina medals kasoro iliyopigwa
IMG-20240331-WA0002.jpg
 
Simba Ulishindwa juzi kutokana na striking force dhaifu! Acheni ujinga... Hii tatizo ni la miaka 2 Sasa na linaanza kuwa sugu!
 
Msimuharibie kijana mkate wake wa kila siku,yeye siyo Kocha.....hamasa zake na maneno yake ni kwenda kujaza uwanja.........Benchi la ufundi ni kiwanjani kumlaumu ahamed kwa matokeo ni zaidi ya umbumbumbu aliousema Rage
 
Kuwa Msemaji wa timu, tena kubwa kama Simba au Yanga, si lazima uwe unamwaga porojo na ndoto ambazo si rahisi kutimizika.

Kabla ya mechi ya Al Ahly Benjamin Mkapa, Ahmed Ally aliwaaminisha washabiki na wanachama wa Simba kuwa Ahly anakufa kifo kibaya na HATOKI BENJAMIN MKAPA.

Baada ya kupigwa kimoja cha dakika ya 5, Ahmed Ally sasa amekuja na SIMBA, TIMU YA MAAJABU.Amedai kuwa Simba itaenda kufanya maajabu kule Cairo, Misri. Eti, imeshawahi kufanya maajabu makubwa huko nyuma.

Hadi sasa, Simba ndiye pekee aliyefungwa kwenye awamu ya kwanza ya robo fainali ya ACCL. Tena amepigwa nyumbani...akashindwa hata kutumia mwiko au jengo kujilinda. Washindi wenzake wengine wa pili, akiwemo Yanga, wamepata suluhu nyumbani kwao.

Ahmed Ally, Mungu anakuona. Endelea tu kuwajaza upepo mashabiki na wanachama wa Simba. Ila tambua kuwa Yanga inatinga nusu fainali kwa mechi ya ugenini kwa Madiba...sare yoyote ya magoli inaivusha Yanga...timu ya wananchi!
Ulitaka afanye nini sasa? Aangue kilio na kuwaambia mashabiki wa Simba kwamba timu yao imeshatolewa? Hata vitani Kamanda hatakiwi kuwakatisha tamaa wapiganaji wake hata kama anajua kwamba wamezidiwa. By the way, kwa nini hutaki kuamini kwamba Simba anaweza kuifunga Al Ahly kwao?
 
Duh, kuna watu mna vichwa vibovu sana. Yani maneno ya mhamasishaji wewe unachukulia kama scientific fact?

Hivi uliwahi kuona wapi, mchezaji, kocha, mshabiki, msemaji/mhamasishaji anaesema team yake inaenda kufungwa?

Mambo mengine mchukulie kama ni sehemu ya kawaida ya michezo sio kukaza ubongo.
Kuna viumbe hawajielewi kabisa, wasamehe.

Wanataka Ahmed aseme Simba Sc inaenda kufa 3-0 kwa Mkapa!.
 
Ahmed Ally anaihujumu timu yetu ya simba. Mashabiki wenzangu tuungane kumuondoa Ahmed Ally na Mwenyekiti Mangungu. Hawa watu wawili ni Yanga dam dam!

Ukiona tu simba imefungwa, basi chanzo kikuu ni Ahmed Ally na Mwenyekiti Mangungu. Haya malalamiko hata shabiki mwenzangu Kalpana anayafahamu.
Mtuachie Ahmed Aliii wetuuu...
Tamka hyo Alii kama mpemba Tate Mkuu
 
Ila mnakosaga cha kuongea jamani so kwa sasa Ahmed Aly haruhusiwi kutia mashabiki moyo kisa nini labda?.kwahyo mwenye ruhusa ya kuongea na kuwapa moyo kuwa mtawaua mamelode kwao ni Yanga Ali Kamwee basi??
Hebu tutoleeni upuuzi...
 
Kuwa Msemaji wa timu, tena kubwa kama Simba au Yanga, si lazima uwe unamwaga porojo na ndoto ambazo si rahisi kutimizika.

Kabla ya mechi ya Al Ahly Benjamin Mkapa, Ahmed Ally aliwaaminisha washabiki na wanachama wa Simba kuwa Ahly anakufa kifo kibaya na HATOKI BENJAMIN MKAPA.

Baada ya kupigwa kimoja cha dakika ya 5, Ahmed Ally sasa amekuja na SIMBA, TIMU YA MAAJABU.Amedai kuwa Simba itaenda kufanya maajabu kule Cairo, Misri. Eti, imeshawahi kufanya maajabu makubwa huko nyuma.

Hadi sasa, Simba ndiye pekee aliyefungwa kwenye awamu ya kwanza ya robo fainali ya ACCL. Tena amepigwa nyumbani...akashindwa hata kutumia mwiko au jengo kujilinda. Washindi wenzake wengine wa pili, akiwemo Yanga, wamepata suluhu nyumbani kwao.

Ahmed Ally, Mungu anakuona. Endelea tu kuwajaza upepo mashabiki na wanachama wa Simba. Ila tambua kuwa Yanga inatinga nusu fainali kwa mechi ya ugenini kwa Madiba...sare yoyote ya magoli inaivusha Yanga...timu ya wananchi!
naitakuwa hivyo huko cairo ahaly atapigwa 2 bila
 
Ahmed Ally anaihujumu timu yetu ya simba. Mashabiki wenzangu tuungane kumuondoa Ahmed Ally na Mwenyekiti Mangungu. Hawa watu wawili ni Yanga dam dam!

Ukiona tu simba imefungwa, basi chanzo kikuu ni Ahmed Ally na Mwenyekiti Mangungu. Haya malalamiko hata shabiki mwenzangu Kalpana anayafahamu.
Wa henya Tate mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom