Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 115
- 258
Na Mwl Udadis, Tarime
Gharama za kusafirisha mizigo kwa meli hadi Bandari ya DSM zinazidi dola za Kimarekani 1,000 kwa kasha moja, tofauti na gharama za chini katika Bandari kama Mombasa. Hii inatokana na ukosefu wa meli za moja kwa moja kwenye Bandari ya Dar es Salaam kutokana na miundombinu yenye uwezo mdogo wa kazi kama vile upakuaji wa mizigo.
Kwa kuwekeza katika miundombinu, tunaweza kupunguza kusubiri kwa meli kutoka siku 5 hadi masaa 24, na kupunguza muda wa kupakia na kupakua mizigo kutoka siku 4.5 hadi siku 2. Hii itasaidia wafanyabiashara na kuwavutia watumiaji wengi wa bandari kutoka nchi mbalimbali na pia mzunguko mkubwa wa biashara katika bandari hii.
Changamoto nyingine ni utegemezi mkubwa wa Bandari yetu hii kwa watoa huduma binafsi kama vile ICDs(Inland Container Depots) na CFS(Container Freight Stations). Hii inaathiri ufanisi wa bandari kwa kiwango kikubwa na ni changamoto inayoweza kumalizwa ndani ya muda mfupi ikiwa muwekezaji serious atapewa kazi na kuwekeza.
Inaweza kuwa vigumu kukubali ukweli, lakini ni muhimu kuelewa kuwa Bandari ya DSM ni rasilimali muhimu ambayo haijatumika vyema. Kuwa na muwekezaji mwenye uzoefu wa kimataifa katika uendeshaji wa bandari kunaweza kutoa suluhisho la changamoto hizi na kufungua ukurasa mpya wa uchumi wa nchi yetu kupitia rasilimali hii adhimu.