EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Hili ni tatizo la kihistoria na inaonekana halifuatiliwi tena tokea Nyerere aondoke madarani. Kwanza kuna tatizo kuhusu jina la ziwa. Malawi wanasema ziwa linaitwa "Lake Malawi wakati sisi tunadai ni "Lake Nyasa". Nchi nyingine na ramani za kimataifa zinalitambua jina la Lake Nyasa. Tatizo lilizanza baada ya Malawi kupata uhuru wake mwaka 1964. Kwa wale waliosoma historia watakumbuka kuwa kabla ya uhuru wake, Malawi ilikuwa ikiitwa Nyasaland. Walipopata uhuru na kubadilisha jina, walitaka pia kubadilisha jina la ziwa kutoka ziwa Nyasa kwenda Ziwa Malawi.
Kitu kingine kilichochangia huu mgogoro ni Banda kuanzisha uhusiano wa kibalozi na serikali ya makaburu Afrika Kusini miaka ya 1960s. Viongozi wengi wa Kiafrika akiwemo Nyerere alipinga sana hili. Hii iliongeza chachu ya mgogoro juu ya jina na ramani ya ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi. Kwa sasa mgogoro juu ya jina la ziwa ni dormant.
Ukija kwenye ramani, Tanzania inadai mpaka unapita katikati ya ziwa. Huu ni mpaka uliowekwa kati ya Uingereza na Ujerumani wakati wa Berlin Conference juu ya kuigawa Afrika katika makoloni. Malawi wanadai ziwa lote liko Malawi ispokuwa ile sehemu ya chini iliyo Msumbiji. Tatizo ni pale Ujerumani iliponyang'anywa makoloni yake baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, ambapo Tanganyika iliwekwa chini ya Uningereza. Kitu ambacho serikali ya kikoloni ya Uingereza ilifanya ni kuweka maeneo yote ya maji ya Ziwa Nyasa chini ya mamlaka ya Malawi (wakati huo Nyasaland) ikiwemo pia ile sehemu ya maji iliyokuwa upande wa Tanganyika. Hiki ndicho kiini cha tatizo kwa sababu baada ya Malawi kupata uhuru, automatically walidhani maji yote ya Ziwa Nyasa yako kwao kwa sababu yaliwekwa chini ya mamlaka yao tokea ukoloni.
Japokuwa kumekuwa na migogoro ya hapa na pale, Malawi imekataa kusema wazi kuwa ziwa ni lao. Kulikuwa na mgogoro miaka ya 1990s na miaka ya 2000s lakini haukufika mahali. Hata hiyo imeadhiri kwa kiasi kikubwa haki za wavuvi hasa wale wa upande wa Tanzania wanaoishi kando kando ya ziwa. Mara nyingi wamekuwa wakilaumiwa na wenza wa Malawi kuwa wanavua kwenye maji ya Malawi.
Serikali ya pande zote husika zinabidi kulichukulia hili suala kwa uzito zaidi. Vingenevyo ukitokea mgogoro wa wananchi wa pande zote husika hapa, itakuwa ngumu kusuluhisha. Haya mambo sijui ya kuunda tume, yatachukuwa miaka na miaka kutatua hili tatizo. Resources are very scarce. Siku ikugundulika kuna madini ndani ya ziwa itakuwa ni balaa.
Chini hapo ramani ya Google inaonyesha Ziwa Malawi halipo Tanzania. Serikali ilishawahi hata kuwaandikia Google kujua ni vigezo gani walivyotumia kuchora hii ramani?