The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Nimefuatilia mjadala kwa umakini sana na binafsi nilimwelewa mleta hoja. Nilichoelewa ni;
1. Kumbe hizo 176bn ni za tangu mwaka 2011 si kwamba zinatolewa kila mwaka!
2. Kumbe fedha hizi ni si kwa ajili ya kutengenezea kitambulisho pekee kwa kila anayestahili bali ni pamoja mobilization, elimu, kufungua ofisi ktk kila wilaya, kulipa consultants, ununuzi wa vifaa vya kazi kama magari, computers nk na kufunga mfumo na pengine mishahara ya wafanyakazi na gharama zingine za uendeshaji.
Kama hii ndivyo, basi kuna picha kubwa kuwa fedha hii inaweza kuwa imetumika kama ilivyokusudiwa na ili kukamilisha zoezi nchi nzima defenetely zinahitajika fedha nyingi zaidi na zaidi!!
Lakini serikali sometimes nayo inapaswa kusikiliza ushauri wa kitaalamu unaotolewa na ma expert wetu na kuacha kufanya kila jambo kisiasa siasa tu ambayo matokeo yake ni kuingia kwa gharama kuubwa zisizokuwa na tija!
Serikali ilishauriwa mara nyingi sana kuwa mfumo wa NEC uunganishwe na wa NIDA ili kila mwananchi apate kitambulisho kimoja tu cha Uraia na hicho hicho kiwe ni cha kutambuliwa kupigia kura.
Hii si tu tungeweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja bali ingeweza kuokoa gharama kubwa na pengine mpaka sasa kila mtu angekuwa na National ID yake!!
Sina hakika ni kwa sbb zipi zilifanya wazo hili lisikubalike.
Binafsi sina tatizo na kuchunguzwa kwa matumizi ya fedha hizi ambazo kwa picha hii pekee kwa mtu yeyote mwenye fikra huru atakuwa ameshaona kuwa hakuna ufisadi wowote hapo.
Nadhani Rais asiwe ni mtu wa kutafuta kukamata mwizi tu na kumfunga bali tunataka awe ni mtu wa kutatuta kasoro za kimfumo ya kiutendaji na kuzirekebisha ili kupata suluhisho la kudumu la matatizo yetu!!
Lakini mimi tayari nilishaanza kupata mashaka na kasi ya JPM kwani imefikia time inakosa mwelekeo kwa kauli na matendo. Ni kama tunarudi kule kule tu ambako tunataka tutoke.
Kiukweli hisia zangu zinakataa kabisa kama JPM atatupeleka kwenye nchi tofauti na ya JMK iwapo anafanya kazi na mfumo ule ule waliomwachia watangulizi wake.
Haiwezekani tukawa na Tanzania mpya kama JPM amezungukwa na washauri wale wale waliotengeneza matatizo haya ambayo tunaaminishwa kuwa anapambana nayo ili kuyaondoa zaidi ya kuona visa na visasi tu kwa walio na mrengo tafauti na wa kwao. Hili la NIDA nalo liko ktk mwelekeo huohuo tu!!