Ukweli kuhusu Mabilioni ya NIDA: Kulinganisha NEC na NIDA Kimantiki

Huyu Tanzania njema ndo jipu lenyewe kama sio mhusika mkuu basi anahusika either directly or indirectly...JF ni kisima cha ma intelligence sasa analeta upashkenge wake hapa kumtetea maimu...huyo mtu wake mie namjua toka amepanga kijitonyama na sasa ana hio pesa ya wizi ya NIDA..tutaonana mahakamani kujua ipi mbichi na ipi mbivu...ngenge nini???
 
Ha haaa haaaa..... kwa kweli sijabanduka niko likizo kidogo ila nilitaka kuhakikisha naondoa upotoshwaji unao letwa, suala la smart card, contact less etc ni mambo mapya hapa kwetu..... cha muhim ni je uzi huu una mashiko? Je kuna kitu tunaweza jifunza hapo maana ratiba za watu sio juu yako mkuu....

Mkuu kuna mchangiaji huko juu alitaka ufafanuzi kuhusu ununuzi wa "server" 100. Ikikupendeza fafanua hiyo kitu ili sasa nijazie hoja yangu ni nirudi hapa kwa kina zaidi
 
Tanzania yangu ilifika hatua mbaya sana, Rais yuko 100% sahihi kulingana na mmoja wao kati ya waliosimamishwa anayejenga gorofa kule bonyokwa na haliendani na kipato cha mtumishi wa serikali
 
Haijalishi kama wamekuwa underfunded au la.

Kazi waliyoifanya mpaka sasa ni majanga.

Kwa sasa hakuna moral au legal obligation ya wao kuendelea katika kazi zao.

Watu wamejadili sana hapa kuhusu hawa jamaa. Kwa maelezo zaidi hizi ni mada/thread zinazowahusu;

]

Nahisi mleta mada unamwingiliano wa kimaslahi na NIDA kwa maana utafiti wako unatoa taswira ya upànde mmoja tu wa shilingi.
Ni kwa nini NIDA hawakuemweleza RAIS kuwa wamenuia kutoa vitambulisho vya ubora wa juu zaidi na vyenye gharama ya juu na kuwa sahihi si muhimu katika zama hizi za teknolojia.Nina hakika rais angeelewa.
Pili hizo gharama za BVR za NEC ni bora ungetuwekea chanzo cha habari ili tuhakiki.
Hizi tuhuma ni mpaka tusikie upande wa pili ndio zitaeleweka.Mtoa mada ametoa utetezi tu kwa NIDA.
 
Kuna watu hawatakiwa kuwa karibu na watu maaana hawapo proffessional wala si watu wa kuwategemea na ndiyo reason president amesema ana kazi kubwa saaana
 
Haijalishi kama wamekuwa underfunded au la.

Kazi waliyoifanya mpaka sasa ni majanga.

Kwa sasa hakuna moral au legal obligation ya wao kuendelea katika kazi zao.

Watu wamejadili sana hapa kuhusu hawa jamaa. Kwa maelezo zaidi hizi ni mada/thread zinazowahusu;

]
Hizo threads hata ukifuatilia wakati wa usajili wa NEC nadhani ziko zaidi ya 100.... hizo threads sio kigezo cha ku water down nilicho andika....
 
Nahisi mleta mada unamwingiliano wa kimaslahi na NIDA kwa maana utafiti wako unatoa taswira ya upànde mmoja tu wa shilingi.
Ni kwa nini NIDA hawakuemweleza RAIS kuwa wamenuia kutoa vitambulisho vya ubora wa juu zaidi na vyenye gharama ya juu na kuwa sahihi si muhimu katika zama hizi za teknolojia.Nina hakika rais angeelewa.
Pili hizo gharama za BVR za NEC ni bora ungetuwekea chanzo cha habari ili tuhakiki.
Hizi tuhuma ni mpaka tusikie upande wa pili ndio zitaeleweka.Mtoa mada ametoa utetezi tu kwa NIDA.
Mkuu upande upi tena? Mi nimeeleza nnacho jua na kujipu upande ulio isha elezwa kwenye magazeti hivo basi pande zote zitakuwa zimeelezwa otherwise kama shilingi yako ina pande 3....
 
Naona na magazeti yanakopi na kupasti vitu vya JF, kuna uzi uliwekwa humu kuhusu hii kitu kama wiki hivi.
Ni aibu kuona gazeti linalotoka kila siku kuandika habari kishabiki bila hata upembuzi yakinifu.Tena heading ya gazeti na content iliyomo ndani haziendani.Mwandishi kaoanisha mistari miwili mitatu na maelezo ya kuunga unga.Nimeionea huruma pesa yangu niliposoma ndani habari nzima.
Mwandishi kama yule ajiongeze nextime.
 
Sio waozee jela ndg yangu@Jyhamah Juma....naaaah wanyongwe tuu tujue moja 179Billion kwa watu million 2..naaaah
 
nashukuru mkuu... ni vema watanzania tukajenga tabia ya kuwa wakweli, kwetu wenyewe na kwa viongozi wetu.... kama vitambulisho vya NEC haviwezi tumika uchaguzi ujao, vina expire in 3 yrs na vya NIDA vita expire in 10 years, huwez walinganisha wote at per.... hapa ni sawa na kulinganisha chungwa na apple eti kwa sababu yote ni matunda....
Wewe endeleza ligi hapa. Kama unafahamu kuna uchunguzi unaendelea si uende ukatoe huo ukweli huko ? Hapa unajiweka matatani tuuu.
 
huo siyo utafiti Bali ni utetezi dhidi ya ufisadi wenu NIDA!!! HAMNA CHA KUJITETEA .........NYIE NI WEZI AISEE YAANI KAKIJITAMBULISHO KAMA HAKO ETI NI 890000=\???? HUO NI UBADHILIFU WA HELA ZA WANANCHI WA HALI YA CHINI!!! kiasi mlichotumia na kulinganisha na idadi ya vitambulisho ni kubwa mnoooo

mtumbua majipu kashasema na hata mfanyeje yeye kasema na aliyepost huu upuuzi Mimi namjua tena ni mtumishi wa nida na sehemu anayoishi ninaijua
 
Nimesoma Magazeti mbali mbali na kumsikiliza mhe.Rais, baadhi ya mitandao ya kijamii na utafiti wangu mwenyewe , ki mantiki NEC na NIDA ni mbingu na Ardhi.

Wakati NIDA ni taasisi mpya na zoezi linalofanyika halijawahi kufanyika nchini kwetu kwa maana ya kumtambua mtanzania, mazoezi mengine yalikuwa ni ya usajili tu kama NEC wanavo fanya.

Madhumuni ya NIDA ni kumtambua nani Raia, nani Mgeni mkaazi na nani mkimbizi. Hili zoezi sio rahisi maana nchi yetu inapakana na nchi nyingi na kuwatofautisha watu wake sio rahisi.

Zoezi la NEC ni la kisiasa wakati mfumo wa NIDA una manufaa kiuchumi, kijamii na kiusalama ndo maana kazi yao inafanywa kwa umakini sana kwa kuhusisha vyombo vingine Kama RITA, Uhamiaji, Tamisemi na vyombo vingine vya ulinzi.

NIDA vs NEC.

1. Card ya NEC ni ya plastic na ina expire in 3 yrs kulingana na material iliyo tumika wakati ya NIDA ni smart card na life span yake ni miaka 10. Hivo ununuzi wa card za NIDA utakuwa ni wa juu kuliko wa card za NEC.

2. Kwa kuwa card za NIDA ni smart Card, hata printers zake ni specialized ili kuweza kuingiza data kwenye chip (watu wa IT watanielewa) wakati NEC ni printer za kawaida unazo weza print popote. Hivo ununuzi wa printa za NIDA utakuwa ghali.

3. Teknolojia ya NIDA ni ya kisasa na
ndo inayo tumika kwa sasa ulimwenguni na ni takwa la E. Africa comunity.

4. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania la leo tarehe 08.02.2016, ukurasa wa 4 , mwandishi amegawanya pesa za usajili za NEC (70b) kwa idadi ya vitambulisho (23m) na kupata kila
kimoja ni sh. 3,010 na kwa NIDA kachukua 179.6b kagawa kwa vitambulisho 2m. Kimsingi 70b ya NEC ni ya usajili tu bila kuweka gharama za BVR. Kama sikosei wakati wa zoezi la usajili wa NEC magazeti yaliwahi kureport gharama ya BVR moja kuwa ni kama $ 6,800 na walinunua BVR 8,000 hivo basi NEC walitumia kama $54,400,000 sawa na karibu 120b bila gharama za usafiri (logistics), karatasi nk hivo si kweli NEC walitumia 70b tu. Wakati gharama za NIDA sh179.6b ni pamoja na gharama za kujenga mfumo wa kielectronic, kumlipa mkandarasi, kununua mashine za usajili na consultant aliye andikwa gazeti la Mtanzania la leo, magari, ofisi zao kila wilaya, na jukumu kubwa la utambuzi linalohusisha vyombo mbalimbali ambalo NEC hawalifanyi (nilivo vitaja hapo juu) na kama mnavyojua uanzishwajiwa ofisi ni pamoja na ununuzi wa samani etc.

5. Wakati NEC hizi pesa walipewa ndani ya mwaka mmoja, na kwa sababu ya uchaguzi NEC walikuwa na cut off time, NIDA pesa hizi
wamepewa tangu mradi uanze mwaka 2011.

6. Kama expiration ya card za NEC ni 3 yrs na NIDA ni 10 yrs hivo cost of investment ya NEC ni mara 3 ya NIDA.

7. Kuhusu sahihi (signature) kuto kuwa kwenye kitambulisho ni suala la kiteknolojia na kiusalama zaidi.Vitambulisho vingi vya kisasa na hata vya nchi nyingi tu havina signature on the face ya kitambulisho maana data zimo ndani ya kitambulisho na zinasomeka kielectronic. Vitambulisho vya Nigeria, Malaysia, Philippines etc havina signature . Data za mhusika husomwa na kitu kinaitwa Card reader. Ni kwa sababu za kiusalama tu maana signature inaweza kugushiwa lakini finger prints haziwezi. Nimeona kwenye magazeti mengi NIDA wamepata award (tuzo) mbili za kimataifa kuhusiana na teknolojia yao lakini hapa kwetu hatuvithamini, mi naona kuna shida.

Mpaka sasa hivi, kwa utafiti wangu, toka 2011 NIDA ilipo anza, NIDA imepata 20% ya pesa zilizo idhinishwa na bunge kwa miaka yote hiyo na sababu hii ya ukata ndo maana zoezi linasuasua na hawajaweza malizia usajili na wameshindwa toa elimu kwa Umma sababu ya Ukata.

Sio nia yangu kutetea ufisadi na ndo maana najiita "Tanzania Njema Yaja". Naiona Tanzania ikielekea kwenye nuru lakini hatutafika kilele cha uzuri huo kama ukweli hautaelezwa... ni vema Watanzania wakauelewa ukweli kabla ya kuhukumu. Mh. Raisi alisema, "msema kweli ni mpenzi wa Mungu" nami naona nimetimiza usemi huo. Na ninaamini baada ya uchunguzi ambao mh. Raisi ameelekeza ufanyike, ukweli utafahamika na haki itatendeka.

Long live Tanzania. Ukweli utatuweka huru.......
Kwa hiyo unajibu hotuba ya Rais????
 
Mchanganuo wako unaweza kuwa ni sahihi kwa upeo wako au Ilivyopaswa kuwa, lakini katika uhalisia na utekelezaji ulivyofanyika inaweza kuwa ni tofauti.(Tuwaachie wahusika).

Lakini ukweli utabaki paleple NIDa ni jibu toka mwanzo wa uwepo wake.
Hiyo kazi ya NIda tayari inafanywa na RiTa, kilichotakiwa ni kuboresha huduma za RIta na sio Kuanzisha shirika lingine linalofanya kazi kama za RITA au amabazo RITA wangeweza kuzifanya.
 
Kwavyovyote vile hawa jamaa kaziyao ni yakusuasua,wenye vitambulisho niwachache sana kulinganisha na miaka yao kazini. Hayo mabilioni pia nimengi mno.
Hii nchi kunaofisi watu wanakula mishahara bila kazi ya mana,naona hawa ni mojawapo.
rais kasimamia wizara miaka, Tena ambayo ela nyingi zinatengeneza kazi ndogo (barabara),mpaka kuwatilia shaka hawa jamaa lazima kunajambo! Tusubiri vyombo sahihi vya uchunguzi.
mkuu umehadithia vizuri lakini hilisuala sio la kusimuliana,linahitaji concrète évidence na viambatanisho kibao (mareceipt, matangazo ya tenda,nukuu za vikao etc.) bila vitu hivyo nivigumu kumshawishi mtu anayejua maana ya utafiti. Wewe umeperuziperuzi huja tafiti.pole lakini
 
RIT
Mchanganuo wako unaweza kuwa ni sahihi kwa upeo wako au Ilivyopaswa kuwa, lakini katika uhalisia na utekelezaji ulivyofanyika inaweza kuwa ni tofauti.(Tuwaachie wahusika).

Lakini ukweli utabaki paleple NIDa ni jibu toka mwanzo wa uwepo wake.
Hiyo kazi ya NIda tayari inafanywa na RiTa, kilichotakiwa ni kuboresha huduma za RIta na sio Kuanzisha shirika lingine linalofanya kazi kama za RITA au amabazo RITA wangeweza kuzifanya.

RITA haifiki zanzibar mkuu.... si ya muungano....
 
Viongozi wetu wa kitaifa hawakukurupuka kamwe!
utafiti ulifanyika kwanza!
read here:----

Baadhi ya wafanyakazi wa
mamlaka ya vitambulisho
(NIDA) waliokumbwa na
"Operesheni tumbua
majipu" walikutwa na mali
nyingi "kupita maelezo"
kwa mujibu wa Waziri wa
Mambo ya Ndani, Charles
Kitwanga.
Operesheni hiyo ambayo
inatekelezwa tangu kuingia
madarakani kwa Serikali
ya Awamu ya Tano, juzi
ilimkumba Dickson Maimu,
ambaye alikuwa
Mkurugenzi wa NIDA,
Joseph Makani
(Mkurugenzi wa Tehama
Rahel Mapande (Ofisa
Ugavi mkuu)< Sabrina
Nyoni (Mkurugenzi wa
sheria) na George Ntalima
ambaye ni Ofisa
Usafirishaji. Waziri wa
mambo ya ndani Charles
Kitwanga alisema hatua ya
kutengua na kusimamisha
watumishi hao
imechukuliwa baada ya
uchunguzi wa hali ya juu
kwenye mamlaka hiyo.
"Walipoulizwa walisema
wamepata mali hizo
kutokana na mikopo na
mali walizonazo" alisema.
Waziri huyo alisema
uchunguzi zaidi
unajielekeza kujua ni jinsi
gani sh 180 bilioni
zilitumika kusajili watu
milioni 6 tu na kati yao
kuwapatia vitambulisho
watu milioni 2.5 tu.
Mbali na kuwaweka kando
watendaji hao, Rais
aliagiza vyombo
mbalimbali kufanya
uchunguzi wa matumizi ya
fedha katika mamlaka hiyo
ikiwemo TAKUKURU, PPRA
na Ofisi ya Mdhibiti na
mkaguzi mkuu wa hesabu
za serikali.
Chanzo: Dar es salaam
wire/
 
Back
Top Bottom