Ukweli kuhusu kampuni ya Katani LTD

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
UKWELI KUHUSU KAMPUNI YA KATANI LTD

UUNDWAJI WA KAMPUNI:

Kampuni ya Katani Limited iliundwa wakati wa zoezi la ubinafsishwaji wa shirika lililo julikana kama TANZANIA SISAL AUTHORITY (TSA) – kwa Kiswahili – MAMLAKA YA MKONGE TANZANIA (MMT).

Katani Limited ilishinda zabuni na kununua hisa 999,999 kati ya hisa 1,000,000 za Kampuni ya MGC (sehemu ya TSA/MMT) zilizouzwa na The Presidential Parastatal Sector Reform Commission (PSRC). Katani Limited ni kampuni ya uwekezaji na uongozi (Investment & Management Company) ambayo ilikuwa inamilikiwa na wanahisa wafuatao:

Wawekezaji wa nje ambao kwa pamoja walimiliki asilimia 90 ya hisa za Katani Limited. Makampuni hayo ni;

Grecian Investment (UK) Ltd, ambayo mmiliki wake ni raia wa Kigiriki ambaye aliwahi kuwa mkulima wa mkonge Tanzania.

Wigglesworth & Co Ltd, ambayo ni kampuni ya Uingereza ijulikanayo duniani kama ni wanunuzi, wauzaji na wasambazaji wakubwa wa mkonge na bidhaa zake. Kampuni hii imekuwa inafanya shughuli hizi kwa zaidi ya miaka 105.

Dekowe GmbH ambayo ni kampuni ya Kijerumani inayotengeneza, kusambaza na kuuza mazulia ya mkonge, Amerika ya Kaskazini, Ulaya, Japani na Bara la Asia. Pia ina viwanda Portugal, Romania na India. Kampuni hii imekuwa ikifanya shughuli hizi kwa zaidi ya miaka 120.

Umoja wa wafanyakazi 87 akiwemo Salum Shamte na wenziwe 86 ambao walikuwa wataalamu waajiriwa wa ofisini na mashambani. Hao kupitia mafao yao kwa pamoja waliweza kulipia asilimia 10 ya hisa za Katani Ltd., kupitia kampuni waliyoisajiri na iliyojulikana kwa jina la Mkonge Investments and Management Co. Ltd (MIM).

Katani Limited iliingia mkataba na Serikali wa kununua baadhi ya mali hizo za TSA (ambazo zilihamishiwa kwenye kampuni ya MGC), tarehe 13 Februari 1998.

MALIPO YA AWALI, UWEKEZAJI NA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MAUZO:

Wawekezaji hao wanne kwa ujumla wao walilipa malipo ya awali na kuanza uwekezaji kama ilivyo kwenye mkataba.

Hali ya mashamba na mitambo kabla ya kuanza uwekezaji ilikuwa mbaya sana;

Chini ya TSA (ambalo lilikuwa ni Shirika la Umma lililopewa dhamana ya kusimamia na kuendesha shughuli za mkonge baada ya utaifishaji); uzalishaji wa mkonge ulishuka kutoka tani 234,000 mwaka 1964 hadi tani 19,000 mwaka 1997;
Miundombinu ilikuwa imechakaa na kuharibika;

Mashine zilikuwa zimechakaa na mitambo ilikuwa mibovu;
TSA ilikuwa imetengeneza hasara kwa zaidi ya miaka 15 kabla ya kubinafsishwa.

Mchakato wa ubinafsishaji ulichukua takribani miaka 6 kabla ya kukamilika Februari 1998.

Kipengele muhimu kwenye mkataba wa mauzo ni upatikanaji wa hati za mali zilizohamishiwa MGC kutoka TSA, ambazo Serikali iliahidi kuzitoa ndani ya miezi sita.

Uwekezaji ulianza mara moja kwa wawekezaji kutumia fedha zao.

Kiwanda cha TANCORD, kilichokuwa kimefungwa, kilifanyiwa ukarabati na ndani ya miezi saba tu kilianza kazi.

UKIUKWAJI WA MAKUBALIANO YA MKATABA WA MAUZO

Wawekezaji walifuatilia hati hizo kwa muda wa miezi 22 bila mafanikio;

Hati zilikuwa ni nyenzo muhimu kwa wawekezaji kutafuta mitaji na mikopo ndani na nje ya nchi;

Desemba 1998 Wawekezaji wa Nje walisimamisha utoaji wa fedha zao na Desemba 1999 waliamua kuondoka na kuuza hisa zao kwa kampuni ya KiTanzania HIGHLAND ESTATES LTD.;

Highland Estates Ltd nayo ilifuatilia hati bila mafanikio. Iliwekeza kiasi cha dola laki nane za Kimarekani (US$ 800,000);

Highland Estates Ltd iliposhindwa kupata hati, mwaka 2000 nayo iliuza hisa zake kwa kampuni nyingine ya Ki-Tanzania AFRIKA MPYA LTD.;

Wakati wote huo MIM (Kampuni ya Wafanyakazi) ilikuwa bado ipo palepale na hisa zao asilimia 10.

MZOZO WA UKIUKWAJI WA MASHARTI YA MAUZO YA HISA BAINA YA PSRC NA KATANI LTD NA USULUHISHI WAKE

(AFRIKA MPYA na MIM) wakiwa kama KATANI Ltd iliendelea kufuatilia upatikanaji wa hati na ilipofika Februari 2002 Katani na PSRC walifikishana mbele ya Wasuluhishi wa mgogoro huo kama ilivyo elekezwa kwenye mkataba.

Wasuluhishi katika mgogoro huo walikuwa Wanasheria nguli wafuatao:

Marehemu Mzee Peter Bakilana (Wakili wa Kujitegemea) - Mwenyekiti
Mheshimiwa Mzee Joseph S. Warioba (Waziri Mkuu Mstaafu) – Mjumbe
Mzee Mohamed Ismail (Wakili wa Kujitegemea) - Mjumbe

Katika shauri hilo, yafuatayo yalibainika:

Katani ililipa mikupuo miwili ya bei ya mauzo ya mali za MGC kama ilivyotakiwa kwenye mkataba:

Katani ilitekeleza baadhi ya vipengele vilivyo kwenye Mpango wa Biashara (Business Plan), ambao ulikuwa ni sehemu ya mkataba;

Katani haikuharibu na ililinda mali na miundombinu iliyo karabatiwa, kinyume na madai ya PSRC;:atani haikukiuka haki za Serikali kama PSRC ilivyodai.

HUKUMU - Ilielekeza Katani waingie makubaliaano upya na Serikali. Hii ilipelekea Katani na Serikali kutengeneza na kutiliana saini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding), Aprili 2005 na kusaini Mkataba Mpya Machi 2007, ULIOTHIBITISHA KATANI LTD HAIDAIWI NA SERIKALI.

KUINGIZWA KWA MFUMO WA WAKULIMA WADOGO NA WA KATI

Katani Ltd iliasisi mfumo wa Wakulima Wadogo wa mkonge kuanzia mwaka 2000, ili kupanua milki ya mashamba ya mkonge. Mfumo huo ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Kwa kuwa Katani ilipewa baadhi tu ya hati mwaka 2005; iliona badala ya kung’ang’ania hati iwashirikishe wananchi wengine 2100 ambao wengi walikuwa wafanyakazi katika mashamba hayo, na kuwaendeleza ili wawe Wajasiriamali Vijijini;

Kila Kaya ya hao wananchi 2100 pamoja na wote wa MIM walipewa kila kaya eka 15 bure.

Serikali ilitoa hamasa kubwa sana iliyopelekea watu wengi kujitokeza kuchukua mashamba hayo.
Masharti ya mashamba hayo ni kwa kila Mkulima kulima mkonge ingawa katikati ya miraba walilima mazao ya chakula.

USHIRIKI WA NSSF KATANI LTD

Katani Ltd ilitambua kuwa wengi wa wakulima wadogo hawana uwezo wa kuendeleza mashamba hayo. Lakini hata wakulima wa kati hawakuwa na uwezo hasa ukitilia maanani zao la mkonge linalochukua miaka mitatu kabla kuanza kuvunwa.

Kwa mantiki hiyo Katani Ltd iliomba ushiriki wa NSSF ili watoe mkopo kwa kuendeleza kilimo cha mkonge.

Ili kukidhi mahitaji ya Mpango mzima wa miaka kumi (10) wa Biashara, Katani Ltd iliomba mkopo wa dola za Kimarekani milioni sabini (US$70 milioni). NSSF ilikuwa iungane na mashirika mengine ya fedha ili kufanikisha mkopo huo.

NSSF, kama ilivyo mifuko ya jamii/penseni ulimwenguni ndiyo chanzo kimoja kikuu kwa kukuza uchumi na inatumika duniani hasa kwa mikopo ya muda mrefu.

Kwa bahati mbaya sana NSSF haikufanikiwa kupata fedha zilizohitajika za Mpango wa miaka kumi wa Biashara, wa Dola za Kimarekani milioni sabini (70). Waliweza kutoa sehemu ndogo sana, ya kiasi cha Dola za Kimarekani milioni sita na laki saba (US$6.7 milioni).

NSSF walikubali kwa masharti kuwa Katani watoe mkopo huo kwa wakulima kwa njia ya HUDUMA ambazo ni;

KUWALIMIA
KUWAPANDIA MBEGU BORA
KUWAPA UTAALAMU
KUWASAIDIA UPATIKANAJI WA MASOKO

Mkopo wa NSSF wa US$ milioni 6.7 uligawanywa katika sehemu mbili;

Ununuzi wa vifaa kama matrekta, mabuldoza, makatapila, mashine za uendeshaji wa mashamba na viwanda;
Uendeshaji kwa Katani Ltd.

Kadhalika, ilielekezwa malipo kutoka kwa wakulima yatakatwa watakapo anza kuvuna na kulipwa;

MATOKEO YA UFANISI WA MKOPO

Uzalishaji ulipanda kutoka Tani 849 mwaka 2005 mpaka Tani 5,420 mwaka 2017.

Katani Ltd iliweza kukarabati viwanda vitatu na kujenga viwanda vipya vinne vya kusindika mkonge katika wilaya ya Korogwe ambavyo awali vilikuwa vimekufa kwa zaidi ya miaka 15.

Katani ilijenga kiwanda cha kwanza duniani cha kuzalisha umeme kutoka kwenye mabaki au takataka za mkonge ambazo awali zilikuwa zinatupwa tu – (FIRST IN THE WORLD SISAL ENERGY PLANT AT HALE ESTATE).

Katani iliweza kukarabati na kupanua Kiwanda cha Tancord cha kuzalisha bidhaa za mkonge.
Katani iliweza pia kutoa gawio kwa Wanahisa mwaka 2013, 2014 na 2015.

USHIRIKI WA NSSF KAMA WANAHISA

NSSF waliona upungufu mkubwa wa mahitaji ya fedha zaidi kwa Katani Ltd kama waliyoomba awali.

Hii ilitokana na wananchi zaidi kutaka kuingia kwenye mradi, ikiwa ni pamoja na Wahariri wa baadhi ya Vyombo vya Habari ambao walifanya kazi nzuri sana ya kuhamasisha wananchi.

Wananchi waliona mabadiliko mazuri ya wenzao walioko kwenye mradi wanavyoweza kuyakabili maisha.

NSSF baada ya kuombwa na kujadiliana na Katani Ltd ilikubali;

Kuubadilisha mkopo wa kwanza wa US$6.7 milioni kuwa hisa na walikubaliana hisa asilimia 49 (49%);
Kutoa mkopo wa ziada kukidhi ongezeko la mahitaji.

NSSF walikubali kwa masharti yafuatayo;

Mwenyekiti wa Bodi ya Katani Ltd ateuliwe na NSSF na mjumbe mmoja mwingine wa Bodi.

NSSF ishiriki kumteua Mkurugenzi mpya wa Fedha na walishiriki kumteua Ndugu Fadhili Mhina kama Mkurugenzi wa Fedha wa Katani Ltd.

NSSF ifanye ukaguzi wa Katani Ltd kila miezi 6.

Isitoshe, ilikubaliwa kwamba Meneja Mwandamizi kutoka idara ya Mipango na Uwekezaji ya NSSF atakuwa anahudhuria mikutano yote ya Bodi ya Katani ambapo atapata taarifa ya maendeleo ya miradi inayotekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka NSSF.

Hayo yalikuwa yakinafanyika bila kukosa. Hali ya Katani Ltd ilikuwa inaimarika kila walivyokuwa wanaendelea.

KILICHO TEREMSHA UTENDAJI WA KATANI LTD BAADA YA MAAGIZO YA MKUU WA MKOA – MHESHIMIWA MARTIN SHIGELA NA ATHARI ZAKE KWA KAMPUNI, TAIFA NA WANANCHI HUSUSAN WA MKOA WA TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Ndugu Martin Shigela alileta vikwazo vingi kwa kampuni.

Kibaya zaidi aliifungia kwa nguvu Katani Ltd isizalishe kwenye viwanda vyake vyote kwa muda wa miezi sita (6) mwaka 2018.
Huu ni muda mrefu sana kwa kampuni kubwa kama Katani kufungiwa.

Alielekeza mkonge wote uuziwe kampuni ya Kichina pekee.

Kiwanda cha TANCORD kilinyimwa mkonge. Hata uliokuwa unatoka kwenye mashamba ya Wanahisa, alielekeza pia auziwe Mchina ambaye mkonge wote alikuwa anaupeleka China.

Kiwanda chetu ambacho ni cha kwanza kwa ukubwa Afrika kiliporomoka na kuzalisha asilimia 20 tu kwa kukosa mali ghafi.
Kiwanda kilibidi kipunguze wafanyakazi kufuatana na uzalishaji.

Serikali ilikosa kodi mbalimbali kwani Katani Ltd ni mmoja kati ya walipaji wakubwa wa kodi mkoani; na mauzo ya nje ya takriban shilingi bilioni kumi (bilioni 10).

Katani Ltd tarehe 3 Septemba 2018 ilimuandikia barua Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa yenye kichwa cha habari “ATHARI ZA MAAGIZO YA KIKAO CHAKE CHA AGOSTI 2018 NA KUORODHESHA ATHARI ZOTE NA USHAURI”.
Katani Ltd bado wanasisitiza kuangaliwa upya maagizo hayo ambayo kimsingi yanaua zao la mkonge Tanzania na tutakuja juta.
Menejimenti na Wafanyakazi wa Katani Ltd wamekuwa kwenye soko la mkonge kwa zaidi ya miaka hamsini (50), na inazijua mbinu zote ambazo zinaweza kutumika ikiwemo bei, upatikanaji, n.k. ambazo zitalenga kwenye kuididimiza Sekta ya Mkonge Tanzania.

MKOPO WA SHILINGI MILIONI 400 KWA TANZANIA PHARMACEUTICALS LIMITED

Tunapenda Umma uelewe kwamba, kampuni hizi mbili, Katani Ltd na Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) ni Kampuni binafsi (Private Companies), ambazo zina mamlaka kamili ya kukopa na kukopesha, kushtaki na kushtakiwa. Ndio maana Katani Ltd iliweza kukopa popote ilipokubalika.

Kampuni nyingi za binafsi (Private Companies) zina utaratibu wa kukopeshana, iwe fedha na/au malighafi. Kwa mantiki hiyo, Katani Ltd ilipokuwa na UKATA na kukosa fedha za kuendeshea mkutano wa Kimataifa wa Nyuzi Ngumu Asilia (International Conference on Hard Natural Fibres), ambapo Ndugu Salum Shamte alikuwa ni Mwenyekiti wa “FAO Conference on Hard Fibres”; na mkutano huo ulikuwa unafanyika Tanga, Tanzania, Katani iliomba mkopo kutoka TPI. TPI iliikopesha Katani Ltd fedha hizo. Mkutano ukafanyika, na Katani ilipokuwa na UKWASI, walizirejesha fedha hizo.

Kadhalika TPI ilipopata dharura na kuhitaji kile kinachoitwa “bridging finance”, iliomba mkopo kutoka Katani Ltd. Katani Ltd ilitoa mkopo huo kwa TPI kwa riba ya asilimia kumi na sita (16%). TPI iliurejesha mkopo huo wote, ikiwa ni pamoja na riba. Uhusiano huu ulikuwa ni wa kibiashara na pande zote mbili zilinufaika. Na hiyo ndio biashara.

NYUMBA YA LONDON ILIYOKUWA NI MALI YA TASMA LTD.

Zimetolewa tuhuma pia, zikielekezwa kwa Ndugu Salum Shamte kwamba aliuza nyumba (na pesa kutia mfukoni mwake), mali ya Mamlaka ya Mkonge Tanzania, iliyoko London na ambayo alikuwa akiishi alipokuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanganyika Sisal Marketing Association (TASMA); Kampuni tanzu ya Tanzania Sisal Authority (TSA). Nyumba hiyo ya London ipo Edgware na Salum Shamte alipoondoka aliiacha mikononi mwa Ubalozi wa Tanzania. Ushahidi upo. Na mpaka leo kuna Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza anayekaa humo. Haingii akilini kwanini “TUME” ilishindwa kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na kupata ukweli. BADALA YAKE, WANAOMBA RUHUSA YA KWENDA LONDON “KUFANYA UCHUNGUZI…!”

NYUMBA YA TANGA ALIYOUZIWA SALUM SHAMTE

Nyumba ya Salum Shamte anayokaa Tanga aliuziwa wakati wa Ubinafsishaji, miaka ya 1990/2000. Mauzo haya yalifanyika kihalali kama yalivyofanyika kwenye nyumba nyingine za Mashirika ya Umma yaliyo binafsishwa kama vile Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Tanzania Breweries Limited, Tanzania Cigarette Company Limited, SIMU 2000 – kwa kuyataja baadhi tu ya mashirika. Isitoshe, kuna nyumba nyingi ziliuzwa kwa wafanyakazi wa Serikali na Mashirika ya Umma waliokuwa wanaishi kwenye nyumba hizo. Hatuamini kuwa Serikali ina nia ya kuwanyang’anya maelfu ya Watanzania hao nyumba zao walizouziwa kihalali kutokana na maamuzi sahihi ya Serikali ya wakati huo.

MWISHO

Kwa kuwa taarifa ile ilisomwa kwa Umma, basi Umma ni lazima upate taarifa ya upande wa pili, ili uwe kwenye nafasi nzuri ya kupambanua kati ya HAKI na BATILI. Siku zote tunaambiwa kwamba ili haki sio tu inatakiwa itendeke, bali inatakiwa ionekane kuwa inatendeka. Ni muhimu Ndugu Shamte na wenzake wapewe fursa ya kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwao na “Tume” ya uchunguzi.
 

Attachments

  • JAHAZI LA SIASA.pdf
    4.3 MB · Views: 26
NYUMBA YA TANGA ALIYOUZIWA SALUM SHAMTE

Nyumba ya Salum Shamte anayokaa Tanga aliuziwa wakati wa Ubinafsishaji, miaka ya 1990/2000. Mauzo haya yalifanyika kihalali kama yalivyofanyika kwenye nyumba nyingine za Mashirika ya Umma yaliyo binafsishwa kama vile Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Tanzania Breweries Limited, Tanzania Cigarette Company Limited, SIMU 2000 – kwa kuyataja baadhi tu ya mashirika...
Asante Mkuu Maalim Mohammed Said kwa bandiko hili kutoka gazeti hilo. Na mimi ni muumini wa haki bin haki, ila katika hili la nyumba kwanza ni kweli nyumba za TSA ziliuzwa kihalali na PSRC.

Kanuni ya kwanza ya biashara yoyote ya mauziano ni muuzaji kutoa offer na mnunuzi kukubali, wakiishakubaliana, mnunuzi analipia anakabidhiwa alinichonua biashara inaishia hapo.

Hivyo kwenye hizo nyumba za TSA, kuna watu walio zinunua kihalali, wakalipa fedha na kupewa stakabadhi za malipo na kukabidhiwa nyumba zao. Nyumba hizo ni zao kihalali na hawajanyang'anywa.

Waliokuwa wafanyakazi wa Mkonge, nao wakaomba kuuziwa nyumba hizo kwa mkopo na kuahidi kuzilipia kwa mafao yao yatakapotoka, na kwa vile ni kweli walikuwa wanasubiri mafao yao, ikakubalika wakopeshwe hizo nyumba na mafao yao yatumike kama bond, wakakabidhiwa nyumba kwa mkopo na kuzimiliki kihalali kusubiria mafao wazilipie.

Kwa vile TSA imebinafsishwa, wafanyakazi hao 87 wakiongozwa na Salum Shamte wakaunda umoja wao wa wafanyakazi na kusajili kampuni ya MIM, kwa share capital ya mafao yao.

Hapa ndio mchezo ulipoanza kwa baadhi yao mafao yao tayari waliisha yatumia kama bond kununulia nyumba za TSA na nyumba wameisha kabidhiwa kwa mkopo, bado tuu kuzilipia, halafu wakaunda kampuni hiyo ya MIM na kutumia mafao hayo hayo ku subscribe as the share Capital ya hiyo kampuni yao.

Wafanyakazi hao kupitia mafao yao kwa pamoja waliweza subscribe 10% shares za Katani Ltd na kuzilipia hizo hisa za Katani Ltd kwa mafao yao yale yale ambayo ndio wangeyatumia kulipia zile nyumba walizouziwa kwa mkopo wa bond ya mafao yao.

Hivyo mafao yalipotoka, badala ya kutumika kulipia nyumba walizokopeshwa, wakayatumia yakalipia hisa. Kwa vile hakuna figures za mafao yao yalikuwa kiasi gani, kama yalikuwa billions yanaweza kununua nyumba, yakanunua hisa na bado balance ikabaki wakapewa cash.

Kamati ilipochunguza ikakuta mafao yalilipia shares tuu na stakabadhi za malipo zipo. Walipotafuta stakabadhi za malipo ya kulipia nyumba hazikuwepo!. Hivyo wameuziwa nyumba kihalali kwa kukopeshwa na kuzilipia kwa ahadi ya mafao, mafao yalipotoka, hawakulipia nyumba bali sasa mafao hayo yakanunulia na kulipia hisa huku nyumba waliisha kabidhiwa kwa mkopo.

Kilichofanyika ni kuitisha kila aliyenunua nyumba aje na kuonyesha stakabadhi ya malipo, walio onyesha proof ya malipo, walibaki na nyumba zao, walionunua kwa mkopo wa ahadi bila kulipa chochote, walisainishwa surrender note na kuzirejesha hizo nyumba na zimerejeshwa serikalini.

Ila kwenye nyumba zilizoko kwenye mashamba kuna watu waliuziwa na kuzilipia kihalali na stakabadhi wanazo, ila wamelazimishwa kuzirejesha kwasababu nyumba hizo hazina hati, hawa wanapaswa wafidiwe kurejeshewa fedha zao. Mauziano yoyote ya jengo ni hati na sio jengo. Huwezi kuuziwa nyumba bila hati kama ambavyo huwezi kununua gari bila kadi.

P
 
Utetezi mzuri sana ila Uncle wangu alikufa kutokana na stress na dhuluma za watu wa Katani Ltd. Alikua mtaalam pekee wa mambo ya Mkonge, aliandika vitabu kuhusu mkonge but hakupata chochote, ndio aliyefaanya research kuhusu maji yanayokamuliwa kutoka kwenye mkonge kuweza kuzalisha umeme, mabaki ya mkonge kutengeneza chakula cha mifugo na kutengeneza pombe kutokana na mkonge. Rest in Peace Uncle, watesi wako wanakabiliana na karma.
 
Upo vizuri kupigania haki za wenzako, ila pia uwe makini wasijekuwa wanakutumia kwa namna moja au nyingine bila wewe kujua, binadamu hawaaminiki.

Naamini kama kweli ameonewa, haki yake ataipata wakati wake ukifika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo vizuri kupigania haki za wenzako, ila pia uwe makini wasijekuwa wanakutumia kwa namna moja au nyingine bila wewe kujua, binadamu hawaaminiki.

Naamini kama kweli ameonewa, haki yake ataipata wakati wake ukifika.

Sent using Jamii Forums mobile app

Jd...
Ingekuwa mimi ndiye niliyeandika haya majibu ungeweza kusema ''natumiwa,'' lakini utasema hivyo ikiwa humjui Mohamed Said.
Ukimjua utajua kuwa Mohamed Said si mtu wa kutumiwa na yeyote awaye yule sembuse ndugu yake kwani ndugu hawatumiani bali wanasaidiana.

Mimi nimeikuta hii kwenye gazeti la Jamvi la Siasa na nimeipenda nikaona niwape na wenzangu kama ilivyo kawaida yangu.
Elimu Bila Khiyana.
 
Mzee wangu Sheikh Mohamedi Said,

Kuna Mahala naiona fraud kwenye mlolongo mzima wa hiyo Katani ltd.. Bwana Shamte na wenzie 80 na zaidi waliokuwa wafanyakazi walijichanga kupitia mafao yao wakanunua hisa 10%. Katani ilibinafsishwa kama sehemu ya mpango wa Serikali kubinafsisha mashirika yake.

Serikali ilibinafsisha haya mashirika baada ya kukosa ufanisi, huoni hawa akina Shamte walihujumu shirika ili waje wanunue hisa? Na baada ya wao akina Shamte kuweka hisa kwanini Shirika liliweza kuwa na ufanisi na walishindwa kuleta huo ufanisi wakiwa waajiriwa?

Hao wenzie na Shamte 80 na zaidi wakwapi na kwanini Shamte tu ndio awe na ukwasi huku wote ni wanahisa? Kwanini Shamte ndio awe na nguvu kiasi cha mwanawe na mkewe kuwa wakurugenzi? Je, na hao wanahisa wengine wanandugu wakurugenzi hapo Katani?

Mzee wangu Sheikh Mohamedi Said, umeshawahi kuyaona makubaliano ya Serikali na Katani wakati Katani inabinafsishwa? Shamte aliteuliwa au kuchaguliwa na nani kuwa Mkurugenzi pale Katani?
 
Mohamed Said hili jambo la Katani Ltd limegusa maswahiba zako nilitegemea utaleta utetezi,nina maswali kidogo;

1. Unaposema walikiuka baadhi ya vipengele na kukidhi baadhi ya vipengele ni utetezi kwenye mkataba?

2. Ulishawahi kusoma "facility agreement" baina ya BASED na Katani Ltd? Nini dhumuni la mkopo? Kuna mahali katika mkataba waliruhusiwa kukopesha kampuni nyingine? Kama hakuna,je wamekiuka au hawajakiuka?

Kwa sasa jibu maswali hayo kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo haya sio mepesi hata kidogo.

Kwa kuwa taarifa yote ua nd. Musabila Kusaya baadhi hatujaiona in writings (bali tulisikia muhtasari) inakiwa ngumu sana kusema lolote.

Japo nina swali la msingi kwa kuzingatia precedence (what we may call good practices kwa yaliyopita)

Barrick na ndugu zao ACACIA walituobia. Airtel nao walituibia sana tu.

Ila wote hawa tulikaa nao mezani, tukajua wapi wametuibia na kutudhulumi na kuna sehemu tukasamehe yaliyopita na kuanza upya kwa kiroho safi.

Kama hawa katani (akina Shamte) kwa assets (wema waliofanya) kuzalisha, kulipa kodi, kutoa ajira, kufufua kiwanda the list goes on vs

Makandokando (liabilities) walizoziona akina Kusaya. Kwanini model ya Barrick na Bhart Airtel hapa haiku-apply?

Kama tunaweza ku-deal na wahujumu uchumi mabeberu bila kuwatia korokoroni bali tunakaa nao mezani, kwa hawa Watanzania kulikuwa na ubaya gani kukaa nao chini?

Anyway, mimi sijui sana ila nawaza tu kwa msingi wa mantiki rahisi; ili kutoleta hofu kwa Mtanzania anaeweza kuthubutu kama akina Shamte.

Yesu akasema yeye ambae hajawahi kutenda dhambi awe wa kwanza kumpiga yule mama kwa mawe hadi kifo.

Kama makosa sio makubwa kwa hadhi ya Barrick/ACACIA au Bhart Airtel; mazungumzo ya mezani yangeweza kuwa suluhu.

Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom