Je wajua haya kuhusu Tanga?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,927
1. Reli ya Kwanza Tanzania Bara - Tanga 1893.

2. Shule ya kwanza ya Sekondari- Tanga 1890 (Tanga Old School).

3. Shule ya Kwanza (Anglikana) Tanzania 1848 - Tanga Magila Muheza.

4. Taasisi ya Kwanza ya Utafiti wa Malaria Duniani - Tanga Muheza, Ubwari 1949.

5. Hospitali ya Kwanza (1st Modern Hospital) - Tanga, Cliff Block 1895

6. Hoteli ya Kwanza ya Kisasa Tanzania - Tanga, Kaiserhof Hotel 1906.

7. Upandaji wa Mkonge wa Kwanza Afrika - Tanga, Pangani 1900.

8. Nembo ya Benki Kuu ya Tanzania ni msukumo kutoka kwa Kiwanda cha Mkonge Tanga kwani kilichangia zaidi ya asilimia 60 ya Pato la Taifa.

9. Tanga lilikuwa jiji la kwanza kuwa Manispaa mwaka 1891.

10. Tanga ilikuwa na Soko la kwanza la kisasa nchini Tanzania - 1903 Soko la Uzunguni.

11. Risasi ya kwanza ya Vita Kuu ya Kwanza ya Afrika ilipigwa Tanga - Novemba 1914.

12. Tanga ilikuwa na kanisa la kwanza Tanzania - Magila Msalabani Muheza - 1840s.

13. Tanga ilitoa padre mzaliwa wa kwanza (Mlutheri) nchini Tanzania, Jacob Lumwe (1880 - 1970).

14. Zaidi ya 95% ya Kata za Jiji la Tanga zina maji ya kutosha, hivyo kuwa jiji pekee nchini.

15. Tanga ina mfumo wa maji taka kongwe na unaofanya kazi Afrika Mashariki.

16. Tanga inashikilia rekodi ya jiji lenye mpangilio mzuri zaidi Afrika Mashariki.

17. Tanga inashikilia rekodi ya kuwa na maktaba ya kwanza ya umma nchini Tanzania miaka ya 1950.

18. Tanga ina mtambo wa kwanza wa kufua umeme nchini Tanzania tangu mwaka 1905 huko Muheza Amani.

19. Bandari ya Tanga ndiyo bandari inayohudumu kwa muda mrefu zaidi Afrika Mashariki (Rejea Mtandao wa Bandari ya Tanga).

20. Tanga ina mnara wa saa kongwe zaidi nchini Tanzania (pengine Afrika) 1901.

20240324_175814.jpg
20240324_175810.jpg
20240324_175806.jpg
 
Asilimia 70 ya watu "maarufu" zaidi nchini kwa mwaka 2020-2024 ni wazaliwa wa Tanga,,
 
Tanga Kunani Palee, Mbona Kila Kitu Pale Kimekufa
Kama Mae Amwali Aliyefunga Kizazi!

Hatujawahi Kulalamika Hata Siku Moja Sisi
Na Juu Ya Maisha Ya Tanga MC Ninatoa Hoja

By Wagosi Wa Kaya
sijui Wako Wapi Sasa Hawa Walikuwa Wanaimba Ukweli
 
Back
Top Bottom