Ukweli kuhusu Dr. Slaa

:48 Today-

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, ambaye tayari amekwishakujivua uanachama wa chama hicho, amesema maisha yake binafsi pamoja na ya familia yake sasa yapo hatarini.-

Hatua hiyo ya Dk. Slaa kufichua hatari hiyo inayomkabili dhidi ya maisha yake aliiweka bayana mwishoni mwa wiki katika mawasiliano yake na chumba cha habari cha Kampuni ya Raia Mwema Ltd, inayochapisha gazeti la kila wiki la-Raia Mwema-na gazeti hili la-Raia Tanzania, linalochapishwa kila siku.-

Slaa alilieleza-Raia Tanzania-kwamba kuna juhudi kubwa zinazofanywa na watu ambao hakuwa tayari kuwataja, akisema juhudi hizo zinalenga kutengeneza mizengwe ya kila aina na kisha kumdhuru, lakini hata hivyo, akisema haogopi chochote na kama ni “Mapenzi ya Mungu yatimizwe.”-


“Ni dhahiri ninatengenezewa mizengwe ya kila aina. Inaonekana maisha yangu na ya familia yangu sasa yako hatarini. Nimekuambia (mwandishi wa gazeti hili) ili ikitokea chochote ujue siyo bahati mbaya. Sijawahi kuogopa na wala sitaogopa. Mtetezi wangu ni Mungu aliye hai na nina hakika atanilinda kama yanayopangwa siyo mapenzi yake. Kama ni mapenzi yake yatimie na isiwe kama ninavyotaka mimi,” alisema Dk. Slaa.-

Ilivyokuwa kujivua uanachama-

Maisha ya Dk. Slaa yapo hatarini ikiwa ni takriban wiki moja tangu ajiuzulu wadhifa wake wa Katibu Mkuu Chadema na kisha kujivua uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.-

Katika uamuzi wake wa kujiuzulu na kisha kujivua uanachama, Dk. Slaa pia aliweka bayana kwamba anastaafu shughuli za kisiasa, akifanya hivyo kutokana na uongozi wa juu wa Chadema kumkaribisha “kwa mizengwe” ndani ya chama hicho aliyekuwa kada wa CCM, Edward Lowassa, ambaye sasa ndiye mgombea wao pekee wa urais.-

Dk. Slaa hakubaliani na namna Lowassa alivyokaribishwa Chadema bila kufuata utaratibu waliokubaliana ndani ya vikao vya chama hicho.-

Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata wiki iliyopita zinasema, miongoni mwa mali za Chadema ambazo Dk. Slaa alizirejesha baada ya uamuzi wake wa kujiuzulu na kujivua uanachama, ni pamoja na gari alilokuwa akitumia kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu. Mbali na gari hilo, alirejesha pia nyaraka nyingine za chama hicho.-

Raia Tanzania-lilipata taarifa za kurejeshwa kwa mali hizo za Chadema na kupiga kambi Ijumaa iliyopita, maeneo ya Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam hadi liliposhuhudia tukio hilo la kihistoria.-

Majira ya saa 3.15 hivi, gari aina ya Noah lenye namba za usajili T 217 BUZ liliingia katika Ofisi za Chadema likiwa na watu wawili na gazeti hili liliwashuhudia wakiteremka na mkoba mwekundu na kisha kuingia ofisini.-

Wakati huo nje ya ofisi, kulikuwapo pikipiki moja iliyokuwa ikizunguka Mtaa wa Ufipa kana kwamba inafanya doria.-

Baada ya muda mfupi, saa 3:20 hivi, watu hao walitoka nje ya Ofisi ya Chadema wakiwa mikono mitupu, wakaingia kwenye gari lao na kuondoka eneo la Ufipa.-Raia Tanzanialilishuhudia pikipiki hiyo iliyokuwa ikifanya doria ikiingizwa ofisini humo muda mfupi baadaye.-

Kuhusu kurudisha kadi yake ya uanachama wa Chadema Ijumaa usiku, Dk. Slaa aliliambia-Raia Tanzaniaakisema: “Sikuwahi kurudisha kadi ya CCM, kwa nini nirudishe kadi ya Chadema? Kadi ni mali yangu na hili nimekuwa nikilieleza mara kwa mara.”

Mbali na kauli hiyo ya Slaa, moja ya vyanzo vyetu vya habari kutoka Makao Makuu Chadema kilieleza; “Hilo sasa ni suala ambalo confirmed (ni rasmi). Dk. Slaa amejivua nafasi yake ya Ukatibu Mkuu na kujivua pia uanachama wa Chadema. Amekerwa na namna mambo yalivyofanyika hovyo, bila kujali misingi ya utawala na maadili katika chama.”-

Dk. Slaa aliacha uanachama wa CCM na kuingia Chadema mwaka 1995 baada ya kutoridhishwa na mchakato wa kusaka wabunge ndani ya chama hicho.-

Mwaka huo 1995 alishinda ubunge kupitia Chadema na kudumu bungeni hadi mwaka 2010 alipogombea urais na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Jakaya Kikwete, huku matokeo ya kura za urais yakigubikwa na tuhuma za uchakachuaji.-

Tangu gazeti hili lilipoweka hadharani wiki iliyopita ukweli kwamba mwanasiasa huyo anayekubalika zaidi nchini ameacha nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema, kumekuwa na uzushi mwingi katika mitandao ya kijamii nchini.

Uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wake Chadema kwa kutoridhishwa na kupokewa kwa Lowassa kwenye chama hicho bila masharti, umefuatiwa na juhudi kubwa kutoka kwa watu mbalimbali kukanusha taarifa hizo kwa malengo ambayo hayajaeleweka wazi, lakini Ijumaa Dk. Slaa aliliambiaRaia Tanzania-kwamba ameamua kukaa kimya na kutojibizana na watu hao, asije akawa kama wao.-

“Nimezoea kusimamia maadili ninayoyaamini. Nimeheshimu na kutii dhamira yangu daima kwa kuwa naamini Mungu huzungumza nasi kupitia dhamira zetu ndiyo maana binadamu tuko tofauti na viumbe wengine. Watasema mengi, propaganda daima hazijengi,” alisema Dk. Slaa na kuongeza:-

“Wanaotumia propaganda kuhalalisha uamuzi mbovu, hawajui madhara wanayoyasababisha.-

“Nitakuwa sina tofauti na wao nikipoteza muda kujibu kila kinachoandikwa kwenye mitandao. Nakuhakikishia sitakwenda chama kingine, bali nimestaafu siasa ili nitumikie taifa langu kwa njia nyingine,” alimwambia mwandishi wetu.-

Akizungumzia taarifa zilizozagaa kwamba angezungumza na waandishi wa habari, Dk. Slaa aliliambia-Raia Tanzaniakwa kifupi: “Sina mpango huo, sina papara, najua kuna mengi yatasemwa. Wakati ukifika nitayazungumzia.”-

Kutokana na uamuzi huo wa Dk. Slaa ni dhahiri sasa Chadema kinakabiliwa na wakati mgumu wa kusaka mrithi wa Katibu Mkuu huyo wa zamani aliyekuwa amekifikisha chama hicho katika kilele cha siasa Tanzania, na tayari watu wa karibu na Lowassa wameanza kujipanga kwa ajili ya kuinasa nafasi hiyo ya Katibu Mkuu.-

Makongoro Nyerere ashangaa-

Katika hatua nyingine, mmoja kati ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa akiwania kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, Makongoro Nyerere, amesema Chadema kitapata wakati mgumu kumsafisha mgombea wao wa urais, Edward Lowassa.-

Makongoro na Lowassa ni miongoni mwa makada 32 wa CCM waliokatwa majina yao na Kamati Kuu ya chama hicho mjini Dodoma mwezi uliopita.-

Akizungumza na-Raia Tanzania-jana, Makongoro alisema uamuzi wa Lowassa kuhamia Chadema ni wa kidemokrasia na haki ya kila Mtanzania.-

“Huo ni uamuzi binafsi, uheshimike. Lakini chama chake kipya kitapata wakati mgumu sana kumsafisha kutokana na tuhuma za ufisadi anazoandamwa nazo.-

“Chadema walikubalika mioyoni mwa wananchi kutokana na hoja ya ufisadi dhidi ya Lowassa. Hiyo sabuni au brashi ya kumsafisha haipo hata Nakumatt,” alisema Makongoro, mmoja kati ya wanaCCM wachache waliokuwa wakimnyooshea kidole Lowassa wakati wa kusaka wadhamini ndani ya chama hicho.-

Kuhusu uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa kuachana na siasa, Makongoro alisema hilo si jambo jema hata kidogo.-

“Tuna muhitaji. Taifa linamuhitaji. Wanasiasa wa aina yake wanatakiwa kuendelea kutoa mchango kwa mustakabali mwema wa taifa letu. Ninamshauri asiache siasa, aje CCM tujenge taifa,” alisema.
 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, mzee Yusuph Makamba, aliwahi kusema haya, 'pale CHADEMA hakuna msafi hata mmoja, ukipenyeza rupia wote watachukua isipokuwa mzee wao yule Dr. Slaa.'

Hata na hivyo, Samwel Sitta alishawahi kusema 'hakuna mwenye sifa ya urais pale isipokuwa Dr. Slaa..'

My take:
Haya leo yametimia, Mbowe kapiga mihela kawapa chenji kina Lissu na wengineo kuwafunga midomo. Kaamua kukubali mgombea kutoka nje as if hakuna mwenye sifa ya urais CHADEMA. Kweli money talks.
 
Ongelea vitu vyenye ushahidi hapa, kama Mh. Mwigulu na Nape wamekamatwa na Takukuru kwa tuhuma za rushwa ili waweze kupata nafasi za uongozi. Wizi wa kura kwa kuweka kura zilizopigwa kwenye masanduku ambazo zimekamatwa sehemu mbalimbali ambapo wagombea kadhaa wanaowania ridhaa ya chama cha Mapinduzi wamekamatwa. Sasa wewe unatuletea porojo zisizo na udhibitisho na kuacha hizi zilizo wazi kabisa.
 
CCM kuna mwenye sifa ya kuwa Rais? Muadilifu mchapakazi hatakiwi CCM ndo Maana Lowassa amepokelewa CHADEMA na UKAWA ... Mwaka huu hata mkitaga haitasaidia ...
 
Naona watu tunajibu swali gumu kwa hoja nyepesi sana ambazo hazina mashiko.
Wote tunapenda mabadiliko kwa manufaa yetu na vizazi vinavyokuja, ila swala la E.L kuingia Chadema limeleta sintofahamu kubwa sana.
e.g Mnyika kupotea na kurudi zimetolewa kauli zenye kijikanganya sana;
- Mara anaumwa, mara anashida za kifamilia... Mara yupo busy na kuandaa mkutano mkuu?!!
Mwenye akili ataelewa kuna kitu hakipo sawa.

Swala la Dr. Slaa, kauli tata zimeendelea kutolewa, Mbowe alinukuliwa na Radio one kama sijakosea akisema Slaa Yupo likizo "Seriously" likizo kipindi hiki!! wengine wanasema yupo busy na maandalizi ya vikao vya chama. Vikao vimeanza jana, Dr. Slaa hajaonekana.

Tuwe wakweli watu wote wenye akili timamu na wapenda mabadiliko, kuiondoa CCM madarakani sio kazi ndogo, inahitaji umoja na mshikamano wa hali ya juu hasa kwa key figures e.g Dr. Slaa. kujiweka pembeni kwa Dr. kutakuwa na athari kubwa sana ndani na nje ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, na hapa CCM itapata mwanya wa kufanya kampeni chafu zidi ya wapinzani.

Rai yangu, chonde chonde kamati kuu fanyeni kila jitihada kumaliza mpasuko na sintofahamu hii haraka sana, la sivyo kuingia IKULU itakuwa ngumu sana na pengine ikawa ndio mwisho wa Upinzani.

Time will tell, October 2015.
 
Tanzania nchi ambayo inamatmiz makubwa na ya ovyo amvayo hayazingatii vipaumbele.ndo masna kika mtu analilia uongoz badala ya kufanya mengine
 
Ule ushahidi waliosema wakina Mbowe na Dk Slaa umeyeyuka ghafla au ulikuwa ni wa uongo.....maana wao ndio walizunguka nchi nzima kwa kumtangazia jamaa kuwa ni fisadi....huku wakisema wana ushahidi mkononi.....sasa iweje leo ushahidi wao waufiche alafu waombe ushahidi mwingine.....au ushahidi wao una walakini........

Wenyewe walikuja kushtaki kwenye mahakama za kiraia(wananchi), watuhumiwa 11 ndiyo walipaswa kwenda mahakamani kwa kudhalilishwa, na wengine(Gavana wa wakati huo) walitukejeli kuwa hizo ni kelele za mlango, hazimzuii mwenye nyumba kulala! Akina Dr Slaa hawana kosa!
 
1. Hao wanaoeda kumuoana hawafungulii sasa watamediate saa ngapi?

2. CHADEMA sio kitengo cha maaskofu wa katoliki hivyo hizo jitihada za kumpeleka Italy zinakihusu vipi Chadema?

3. Hivi mnajua maana ya wengi wape? Sasa mtu anapogeuka mungu mtu ndipo anapopuuzwa

4. Na sasa rangi halisi ya huyo mnaemwita mchumba/mke ndipo inapoonekana kama Mumewe angekuwa Rais kuna siku angemfungia ndani hivyo hivyo muanze kutafuta wanawake wa kwenda kumshauri mke ali aongee na mumewe

5. Hivi aliyesotea chama na yeye peke yake?

6.Wale waliopata kusikia habari za vita wakati mwingine askari akiwa vitani anapojeruhiwa na kutoonesha matumaini ya kupona huwa anauliwa sio kwa sababu hakuwa na mchango bali ni kwa mstakabali wa kushinda vita

7. Ifike mwisho tusiengeneze miungu watu. Wengi wape ndio utaratibu katika kufikia mwafaka wa makundi

Dr SLaa unamwita mungu mtu ila ya lowasa huoni? kwani yeye nani atetemekewe na mwenyekiti mpaka amuombe kuimba peeepoozi.
 
Wenyewe walikuja kushtaki kwenye mahakama za kiraia(wananchi), watuhumiwa 11 ndiyo walipaswa kwenda mahakamani kwa kudhalilishwa, na wengine(Gavana wa wakati huo) walitukejeli kuwa hizo ni kelele za mlango, hazimzuii mwenye nyumba kulala! Akina Dr Slaa hawana kosa!
Kwa hiyo ushahidi mliotuambia kuwa mnao ulikuwa ni wa uongo.......??
 
Ongelea vitu vyenye ushahidi hapa, kama Mh. Mwigulu na Nape wamekamatwa na Takukuru kwa tuhuma za rushwa ili waweze kupata nafasi za uongozi. Wizi wa kura kwa kuweka kura zilizopigwa kwenye masanduku ambazo zimekamatwa sehemu mbalimbali ambapo wagombea kadhaa wanaowania ridhaa ya chama cha Mapinduzi wamekamatwa. Sasa wewe unatuletea porojo zisizo na udhibitisho na kuacha hizi zilizo wazi kabisa.
sasa wewe ndio huna ushahidi,
 
Mzee Makamba Ni Moja ya Wanufaika Wa Mfumo Kandamizi wa CCM.Je UKAWA Ni CHADEMA Tu?, Mbona Wenyekiti wenza Wamekubali

Kumwachia Lowassa Kugombea. Unafiki Chadema Ingempendekeza Mtu Asiye Chaguo la Wengi UKAWA Wangekubali??.

Hakika Lowassa Atawapelekesha MaCCM Naa Wanalijua Hilo. Swalia Rahisi Kama CCM Wanaona Mwh. Lowassa Ni Mwepesi Si Ndio Mfurahi

kwa Kurahisishiwa Kazi.
 
tizo la wengi wetu ni kusahau tu. kwa kifupi:
Mh. Mbowe anaona mbali sana yeye ni kama mvuvi anaejua samaki walipo hili si jambo la kubeza kwa mtu mwenye kufikiri. maneno mengi yanaweza kusemwa lakini ikumbukwe kwamba ni yeye na viongozi wengine wa CHADEMA aliyemshawishi dr. Slaa agombee urais na si ubunge na hesabu hizi zilikubali wengi tumesahau. Hata hizi hesabu za sasa kwangu mimi ziko sawa kabisa kwa mustakabali wa upinzani na siasa za Tanzania, hiki ni kimbunga.
Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa taarifa vikao vya kumshawishi EL apitie CDM kugombea urais Dr. alishiriki sass hizi filimbi tunazoziona zinatoka wapi?

Kweli huu ni wakati wa wasiouza kuuza habari zao... utumbo utanunuliwa sana wakati huu.. kwi kwi kwi kwiiii!

VIVA CHADEMA... VIVA UKAWA...

Aluta Continua...
 
Hizi ni dalili za chama cha ccm kuwa cha upinzani ifikapo oktoba
 
Naona CHADEMA wapo sahihi as long as katiba yao inaruhusu yeyote mwenye kadi ya chadema kuweza kugombea uraisi. Then kwa fikra za kawaida, EL ana influence kubwa kwa wananchi ambapo ndipo kura zilipo,,,, so kumpA EL nafasi hyo ya juu,, sio makosa kwa CHADEMA kwa kuwa wanataka ushindi.
 
mzee makamba ni moja ya wanufaika wa mfumo kandamizi wa ccm.

km umenisoma vzuri makamba hajabisha kwamba hakuna mafisadi ccm yy anachodai hata cdm wapo isipokuwa mzee slaa.tulimbishia sna hapa mtandaoni leo yametimia mbowe kauza chama iliyotukuka ktk misingi imara ya uzalendo nakupigana vita dhidi ya ufisadi na ukandamizaji wa demokrasia.yale yale ya ccm yapo cdm subiri time will tel mbowe akiwa pm na luwasa rais ujue nchi imeuzwa yote.labda huyo mzee slaa awe mwenyekiti wa chama cdm anaweza kuwa control wasiuze nchi.bila slaa big no tumekwisha tutauzwa km pp.
 
Mimi nashangazwa na watanzania, sijui tumerogwa na nani, leoa hii watu wamegeuka wanaimba wimbo wa kwamba hakuna ushaidi na kama unao nenda mahakamani, wakati huo hawa viongozi waliyasema hayo na wanaendelea kusema, hvi ni mtanzania gani asiyejua kwamba Lowasa ni fisadi? Tuliaminishwa hivyo siku zote, na kama si kweli basi hzi lawama ziende kwa hawa viongozi wetu, kutuaminisha upuuzi huo, na ss bila kuiliza kama wanoa ushahidi nasi tukaanza kuimba wimbo huo huo kama mazezeta na hasa chadema. na mbona sikusikia mtu kumuuliza Dr. Slaa au Lissu kwamba mna ushahidi wazee, watambue tu kwamba pia huwa kuna mazingila ya kuaminika na hata mhakama yajua hayo, ss ukiona mtu anakomaa kweli kweli, ujue kwamba aidha uelewa wake ni mdogo au kaamua kuwa mshabiki, na hii nchi tunasumbuliwa na ushabiki, nadhani pia hzi siasa tumezianza hapa karibuni.
 
Back
Top Bottom