Ukweli kuhusu Dr. Slaa

SAA hizi mmeshakisahau chama chenu cha ccm mmebaki kucheza ngoma ya ukawa
 
Dah,
Lizaboni kaja na wasifu mwingine; eti mwasheria na kada wa mda mrefu wa Chadema. Lowasa atawatesa sana watu wa Lumumba. Nawashauri muanzishe tredi za Magufu maana atapotea hevi hivi kwenye media.
.

Mkuu Lumumba wamepoteana wameshamsahau hata magufuli,kazi yao ni kuja na ID mpya kila siku
 
Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.

:ban: :welcome:
 
Dr. Slaa nafikiri alifaulu sana saikolojia. Maana 2010 aliwaambia, bati 5000, cement 5000, mkaacha kunadi sera zenu, mkahamia kwenye sera za CDM. Baadae mkanunua ZZK ili CDM ife lkn akafa yeye CDM ipo.

Tulimwita Lowassa ni fisadi mmemkataa na sasa sisi tumemchukua. Yaani kifupi Lumumba hapakaliki. Dr. yupo na wanaandaa ilani ya chama na wanajiandaa kushika nchi, na Lowassa atawanyoosha.
 
Wahenga walipata kunena kuwa DAIMA PANAPO FUKA MOSHI LAZIMA KUNA MOTO CHINI.......na DAIMA LISEMWALO LIPO NA KAMA HALIPO LAJA...........
 
Hivi kwa mfano Dr Slaa akitoka Chadema na kuingia Majukwani kumpinga inaweza athiri kura za Lowassa?
 
Wakuu, wakati kamati kuu ya chadema ilikaa kujadili ujio wa lowassa chadema kulitokea malumbano ya hoja.upande mmoja ukikubali ujio wake na upande mwingine ukipinga ujio wake.lakini taarifa zinasema kwamba mwisho wa siku pande zote ziliridhidhiana na kukubali kwa pamoja ujio wa lowassa chadema...

Ukweli ni kwamba lowassa ana nguvu kubwa sana na pasipo yeye itakuwa ni ndoto kuiondoa ccm madarakani.kwamba ili tuiondoe ccm madarakani ni lazima tuipasue kwanza na lowassa ndie mwenye uwezo wa kuipasua ccm..kufikiri kwamba tunaweza kuiondoa ccm madarakani pasipo kuipasua kwanza ni ndoto za alinacha..

Na kama ukawa watashindwa kuiondoa ccm madarakani mwaka huu basi wasahau kuchukua serekali kwa miaka atleast 50 ijayo,kwasababu ccm nao wataanza kujipanga..ndo maana mbowe na ukawa wanafanya kila njia kuhakikisha wanachukua nchi mwaka huu hata kama njia wanazopitia zitawakwaza baadhi ya viongozi wenzao..

Dr Slaa ni mpole na mtu wa dini aliyepitiliza,hana guts za kuchukua maamuzi magumu ambayo ndiyo yanayohitajika kwa sasa..naamini kabisa kwamba chadema na dr slaa watafikia makubaliano soon kwasababu ccm has to go,,by any means neccesary..Tushukuru chadema kwa kuwa na mwenyekiti shupavu na imara kama mbowe..be blessed!
 
Mleta mada plz kutuaminisha ukweli wako kwa nini usingepiga screenshot hiyo conversation ya group la whatsapp ukaweka hapa tujaona Josephine anavyosema? Vinginevyo utakuwa unaleta porojo tu
 
Tukimpoteza Slaa tusahau kushinda.

Kuna watu wanaichukulia hii issue ya Slaa vs Lowassa very simple, ni hivi hii issue itawacost sana Chadema, time will tell. Eti leo Dr hana hathaminiki ndani ya chama, watu wanadiriki kusema kwani chama kakijenga yeye peke yake? Ukweli ni kwamba Dr ndio kaifikisha chadema pale ilipofika, sasa hivi wote mmemgeuka
 
Hujaeleweka bado kama unachemka tu. Dr. Slaa anamachungu na urais wakati mbowe ameona huu ndo wakati wa ukombozi kwa vyama vya upinzani.
 
Nchi hii sijui inalaana maana sielewi kabisa mwaka huu ulikuwa ni mwaka Wa kuiondoa ccm madaraka dalili zote zilionyesha hivyo Leo tunafika ukingoni wale waliopambana hata kuweka uhai wao rehani ndio wanataka kutukwamisha aiseee inatia uchungu sana Dr Slaa tafadhali usituangushe tupo chini ya miguu yako tunakuomba baba Samehe mlioko huko ndani ya chama ndio mnaujua ukweli huku njee hatujui mnatuumiza mioyo yetu kwa hii sintofahamu tunatamani kuifikia ile furaha kuu (ushindi octoba) tukiwa pamoja wenye umoja.Mungu akuongoze katika tafakuri unayofanya ufanye maamuzi sahihi ambayo hayatafanya jeraha katika mioyo ya wanamabadiliko. Without you octoba tunaweza pata furaha but with you tatapata furaha kuu.Mungu ibariki Tanzania.
 
Swala ni kuweka pembeni utawala na kuingiza utawala mwingine. That s all mengine baadae. Come back Slaa together with you we can change.
 
Back
Top Bottom