Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,346
- 33,183
UKOROFI WA MCHINA: SAMSANG YAWALIPA APPLE $ BILLION 1 KWA KUPELEKA MALORI 30 YENYE SARAFU ZA SENTI 5
Juzi malori 30 yaliyokuwa yamejaa sarafu (ama kunogesha zaidi chenchi) za senti tano tano, yaliwasili kwenye makao makuu ya Apple, jimboni California, Marekani.
Awali, walinzi wanaolinda makao hayo makuu walidhani malori hayo yamepotea njia, lakini dakika chache baadaye, Tim Cook (CEO wa Apple) alipokea simu kutoka kwa CEO wa Samsung Lee Kun-hee, akimueleza kuwa wamewalipa faini yao ya dola bilioni 1, kutokana hukumu dhidi ya kampuni hiyo ya Kikorea.
Kitu cha kuchekesha zaidi ni kuwa nyaraka iliyosainiwa haioneshi njia moja ya kulipa faini hiyo, hivyo Samsung ilikuwa na haki ya kuwapelekea faini hiyo watengenezaji hao wa simu za iPhone vyovyote wanavyotaka.
Mchezo huu mchafu na wa kijanja utawaumiza kichwa wakurugenzi wa Apple kwakuwa itabidi iwachukue muda mrefu kuhesabu fedha zote ili kuhakikisha kama zimetimia na kujaribu kuzipeleka benki ambako hawajui kama zitakubalika.
Mwenyekiti wa Samsung Electronics Lee Kun-hee, amewaambia waandishi wa habari kuwa kama Apple wanataka kucheza mchezo mchafu na wao pia wanaujua. Undava undava na kama noma iwe noma tu!
Juzi malori 30 yaliyokuwa yamejaa sarafu (ama kunogesha zaidi chenchi) za senti tano tano, yaliwasili kwenye makao makuu ya Apple, jimboni California, Marekani.
Awali, walinzi wanaolinda makao hayo makuu walidhani malori hayo yamepotea njia, lakini dakika chache baadaye, Tim Cook (CEO wa Apple) alipokea simu kutoka kwa CEO wa Samsung Lee Kun-hee, akimueleza kuwa wamewalipa faini yao ya dola bilioni 1, kutokana hukumu dhidi ya kampuni hiyo ya Kikorea.
|
Tim Cook |
Lee Kun-hee |