Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,199
- 10,932
Tumezoea kusoma na kufanyia mitihani nadharia za wazungu.Leo na mimi mswahili naleta nadharia yangu juu ya mgawanyo wa ukoloni.Napendekeza wasomeshwe vijana wetu wa masomo ya DS mwaka wa mwanzo na wa pili chini ya kipengele chenye jina la Ami's colonial classification.
Hapa nitazitaja hatua tano za mwanzo kwa ufupi bila kuingia kwenye undani wake.Pia nitaidokeza hatua ya sita ambayo bado hatujaifikia kikamilifu.
Hatua ya mwanzo ni pale binadamu alipopata ladha ya vitu mbali mbali na kuvipenda halafu vikakosekana maeneo alipo na akafikiria uwezekano wa kupatikana maeneo ya mbali na anapoishi.Vitu hivyo vizuri ama alivijua kwa kuwepo maeneo yake halafu vikaadimika au vililetwa kibahati na wasafiri kutoka mbali.Walipofika huko mbali akakuta kuna watu kama yeye lakini wanatumia vitu vyengine tofauti na vile walivyovipenda wao,
Ili kuvipata vitu hivyo binadamu akawaza jinsi ya kuvichukua bila kuingia ugomvi na wenyeji waliovikalia.Sehemu hii imegawanyika makundi matatu.
a)Wazungu kutoka Ulaya walitumia vifaa vya kimaendelel ya kiteknolojia kama bunduki na vioo na mapambo ili kujikuribisha na wenyeji.Vile vile walitumia dini na kujifanya wachamungu ili kubadili fikra za wenyeji.
b)Waarabu: Kutokana na njaa na ukame na ugomvi katika maeneo yao wakasafiri kwenda mbali Afrika na Asia.Kila walipofika walijifanya kama wamefika na kutopenda kurudi kwao kwa namna yoyote ile.Wakaowana na wenyeji na kuingia miradi ya kiuchumi na kulima vile walivyovikosa kwao.Kwa vile wengi wao walikuwa na dini ya Uislamu basi na Uislamu ukaingia maeneo waliyojiimarisha.
c)Kugombea maeneo kwa vita na hatimae kugawana maeneo.
Kipindi hicho ni kirefu sana mpaka 1884
Hatua ya pili ni pale wakoloni walipoendelea kufaidi kupata matunda waliyoyataka bila msuguano na wenyeji kwa muda mrefu mpaka pale walipoanza kukwaruzana na wenyeji kwa kutokutaka kuishi kwa wema na kugawana mapato.Kipindi hiki kulikuwepo na malalamiko ya chini kwa chini na uchochezi wa kugombanisha watu ili wasiwe wamoja.Wakoloni ili kujilinda walitia fitna kwa watu kwa faida zao.
Hatua ya tatu ni wenyeji wa maeneo mbali mbali kuanzisha harakati za kutaka kuwa huru ili na wao wasibaguliwe na wafaidi matunda yaliyowazunguka ambayo kwa sasa na wao wamejuwa ladha zake na kujua thamani zao.Matokeo ya hatua hii maeneo mengi yakafanikiwa kujiweka huru kwa njia ama kupigana au wakoloni kuona bora waachie tu wajitawale.Lakini hawakuondoka kwa kupenda ikabidi wafanye njama za kuondoka na kubaki wakati huo huo.
Hatua ya nne ni wale walioachiwa madaraka kutokuweza kujiendesha ikawa nafasi ya wakoloni kurudi kwa mlango wa nyuma wa ukoloni mamboleo.Wenyeji wa maeneo mengi hatimae wakashtukia kwamba wakoloni waliondoka lakini bado wao ndio wanaoendesha mambo yao na kufaidika na matunda yaliyowazunguka.
Kiwango cha juu cha ukoloni mamboleo ni pale wakoloni walipoona kutofanikiwa sana kutumia vita vya kidini ili watu wapigane vita vibaya.Hapo yalitumika makundi ya kigaidi kama kisingizio.
Hatua ya tano.Nchi nyingi zenye vijana waliozisoma kwa namna zao hatua nne za mwanzo na kupata elimu za kisasa kuamua kutaka kujitenga moja kwa moja na ukoloni mambo leo hata hivyo inaonekana hawajakuwa na nyenzo za kujitenga moja kwa moja,
Hatua ya sita ni pale wakoloni kutokutaka kuondoka kwa namna yoyote ile na watakapokuwa tayari kutumia nguvu na huku wenyeji nao wakiwa na nia ya kujitawala hata kwa nguvu ili wasinyang'anywe vitu vizuri walivyonavyo.Hatua hii itahusisha vita vikali na kuifanya dunia isiwe mahali pazuri pa kuishi .Watu watatamani kiama kifike na waliokufa wakijua mambo yalivyo duniani watafurahi kufa mapema na hawatotamani kurudi tena.