Ukiwa na tabia hizi, jiandae kuwa middle class na kuteseka ki uchumi!

Kwa tafsiri sahihi ya asset, nyumba sio asset,ni liability. asset ni kitu kinachokuingizia pesa, sasa kama nyumba unakaa tu mwenyewe inaingizaje pesa? sana sana inakutoa pesa kwa kurepair nk. gari pia si asset cuz linakutoa pesa kila siku za mafuta na repairs. asset takes money to your pocket,liability takes money out of your pocket.

Mkuu, hii copy and paste kutoka rich dady poor dady ya robert kiyosaki itakufikisha kubaya. Inaamaana hawa wenye nyumba sinza tunakopanga kwao ni liability? Acha utani bana.

Hata kama nyumba yangu sijapangisha ninaishi mwenyewe, nisingekua nayo si ningekua ninatumia pesa ku rent nyumba nyingine? Sasa hii rent ambayo nakua situmii kwakukaa kwenye nyumba yangu huoni kwamba nyumba yangu ninayo ishi teyar ni ASSET?

One final thing ..., ku-own nyumba US na Tz ni vitu viwili tofauti sanaaa. Wakati bei ya nyumba US ina flactuate (ie appreciate and sometimes depreciate) Taz nyumba na hasa kiwanya kina appreciate constantly ... that is fact.
 
Ndio nikasema kwamba Bodaboda zote ni kwa kujenga nyumba na Carry moja ni kusomesha my two children International School na matumizi binafsi.
Yaani nimejenga kwa urahisi sana,maana kila mwezi nilikuwa naenda na mafundi kwa ajili ya ujenzi wa kidogo kidogo mpaka nikamaliza kwa huku,then ndio nikahamia Chanika Dar na pia nikajenga kwa style ile ile.
Maana Bodaboda moja naletewa hesabu ni Tsh:50,000 kwa wiki,kwa hiyo inakuwa (Tsh:50,000 x 5 Bd x 4wk = Jumla Tsh:1,000,000 kwa mwezi

Inamaana wakati wa ajira yako ambayo uliiacha hukuwa na uwezo wa kutenga 1,000,000/- kwa mwezi kama akiba ili ujenge sio? Sasa kama mwenzio ana take home ambayo inamwezesha kuweka akiba ya 1,000,000/- baada ya matumizi yake ya kawaida, kuna ubaya gani akianza kujenga?

Tena akimaliza kujenga atanunua suzuki caryy kila baada ya miezi kadhaa maana atakua halipi kodi ya pango tena, au kama nimekosea naomba kusahihishwa.

Na vipi ungekua huna nyumba uliyojenga (hata kama haikumalizika) ungepata wapi mtaji? Na huoni uliiuza kwa faida? So nyumba ni asset kwa Bongo na sio liability kama US!
 
Mkuu, hii copy and paste kutoka rich dady poor dady ya robert kiyosaki itakufikisha kubaya. Inaamaana hawa wenye nyumba sinza tunakopanga kwao ni liability? Acha utani bana.

Hata kama nyumba yangu sijapangisha ninaishi mwenyewe, nisingekua nayo si ningekua ninatumia pesa ku rent nyumba nyingine? Sasa hii rent ambayo nakua situmii kwakukaa kwenye nyumba yangu huoni kwamba nyumba yangu ninayo ishi teyar ni ASSET?

One final thing ..., ku-own nyumba US na Tz ni vitu viwili tofauti sanaaa. Wakati bei ya nyumba US ina flactuate (ie appreciate and sometimes depreciate) Taz nyumba na hasa kiwanya kina appreciate constantly ... that is fact.

Very wise kaka.... Unajua jamaa anataka kufabya maisha kama coin kwambe ukifanya hv utabaki middle class maisha yako yote hivi hautabaki middle class.....
 
Very wise kaka.... Unajua jamaa anataka kufabya maisha kama coin kwambe ukifanya hv utabaki middle class maisha yako yote hivi hautabaki middle class.....

Kuna vijana wazazi wao wana nafasi serikalini, wanaanzishiwa makampuni halafu wanakabidhiwa halmashauri wanapata tender bwerereeeeee ... halafu mitaani wanaona wenzao ni wazembe hawataki ku-invest. Ndo maana na sisitiza, vitabu vya kiyosaki havi apply sana kwetu kwasababu the system is not fair ... ujanja ujanja ni mwingi mno
 
Inamaana wakati wa ajira yako ambayo uliiacha hukuwa na uwezo wa kutenga 1,000,000/- kwa mwezi kama akiba ili ujenge sio? Sasa kama mwenzio ana take home ambayo inamwezesha kuweka akiba ya 1,000,000/- baada ya matumizi yake ya kawaida, kuna ubaya gani akianza kujenga?

Tena akimaliza kujenga atanunua suzuki caryy kila baada ya miezi kadhaa maana atakua halipi kodi ya pango tena, au kama nimekosea naomba kusahihishwa.

Na vipi ungekua huna nyumba uliyojenga (hata kama haikumalizika) ungepata wapi mtaji? Na huoni uliiuza kwa faida? So nyumba ni asset kwa Bongo na sio liability kama US!
Mie nimemaliza,sipo tena huko.
Na alietoa Mada alitoa ushauri tu is not a fixed Order
 
Anayesema nyumba ni asset hyo akapimwe akili nyumba kila mwisho wa mwezi inakukamua kulipia umeme maji,....still unasema eti ni asset labda km umeipangisha lkn km unaishi ww ni still liability ....wengine wanasema eti unaweza chukulia mkopo mnajua riba za benk au hamjui nyumba inaweza kuwa na thamani ya millioni 75 wakakwambia thamani yake millioni 40 baada ya hpo wanakupa mkopo million 20 ambayo riba yake ni juu waweza jikuta marejesho ni 27 ina maana Kuna obgezeko la 7million ambayo ukiitoa kwa 20 unaipata 13 million ambayo kwa malengo yko utakuwa umekula hasara
 
Your somehow right ila kuna mambo mengine mfumo wa nchi hii yetu unachangia watu kuwa na hulka au tabia ya namna fulani. Cha kwanza ni housing sub-sector. Wenye nyumba wengi ni watu binafsi na wengi wao ni either wastaafu au wafanyabiashara. Hakuna mfumo unaoeleweka wa kodi na ndio maana hukuti wahindi unaozungumzia kwenye nyumba za uswahilini -- wao ni wankufa na msajili na wako karibu na mji ambapo swala la usafiri si tatizo. Huwezi kuta Mhindi anaishi Mbezi mwisho, Kinyerezi etc. Pili hakuna mfumo unaoeleweka wa mikopo ya nyumba. Mortgage ya nyumba hapa kwetu ndio inaanza tofauti na nchi zilizoendelea. Ni tatizo kwa kweli kuona msomi au mfanyabishara anakimbizani na malori ya mchanga, fundi aliyekimbia na mfuko wa smenti, etc. Hiyo inaleta inefficiency kubwa sana kwenye uchumi. Mwisho ni swala la mfumo wa usafiri. Hakuna public transport inayoeleweka na barabara zetu bado ni hovyo. Usalama bado pia tatizo.
 
Anayesema nyumba ni asset hyo akapimwe akili nyumba kila mwisho wa mwezi inakukamua kulipia umeme maji,....still unasema eti ni asset labda km umeipangisha lkn km unaishi ww ni still liability ....wengine wanasema eti unaweza chukulia mkopo mnajua riba za benk au hamjui nyumba inaweza kuwa na thamani ya millioni 75 wakakwambia thamani yake millioni 40 baada ya hpo wanakupa mkopo million 20 ambayo riba yake ni juu waweza jikuta marejesho ni 27 ina maana Kuna obgezeko la 7million ambayo ukiitoa kwa 20 unaipata 13 million ambayo kwa malengo yko utakuwa umekula hasara

Mkuu ukweli ni kuwa nyumba ni basic need kama iliyo chakula.Issue ni aina gani ya nyumba na umiliki wake. Unaweza kuwa na nyumba ambayo unawea ipangisha ikawa asset inayoleta kipato. Ukiamua kwa mfano kuishi kwenye nyumba uliyoijenga ambayo kodi yake inawezakuwa TZS 800,000 hii kwako inakuwa ni 'implicity rent' kwa maana ya kwambaunailipa kila mwisho wa mwezi ingawaje huipokei (i.e. unasave). Hivyo ukiwa unaishi nyumba ambayo ‘alternatively’ ungeweza pangisha maana yake unailipa kodi ambayo ungeipata au ungeilipa. Kwa hiyo watu wote waliojenga nyumba na kuishi humo ndani 'implicitly' wanalipa kodi, ingawaje si kwa watu wengine. Swala la umeme, maji na matumizi mengine ni yamsingi kwenye nyumba, iwe nyumba ya kupanga au la.
 
Usipotoshe watu,sio lazima kuanza kama walivo anza wahindi.
Naweza nunua gari ya 10m,lakini siwezi jenga nyumba (yoyote ile)ya 10m.

Kama uwezo wangu ni 10m kwa sasa,na nahitaji gari kwanini nisinunue gari huku nikijipanga na mengine hayo?

Hivi ndivo nilivo anza,na i promise you sita struggle kama unavo taka watu waamini.

1.Nikiwa chuo nikanunua shamba ekari8 kwa 1.3m mkuranga.
2. Nika graduate 2012 na nikanunua gari 2013, (hili lilinisaidia kutembelea shamba kirahisi zaidi,point: Fanya kile unacho weza kufanya kwa wakati huo,don't stretch beyond your limit kwa kukimbilia kujenga afu unaacha nyumba ikiwa kwenye msingi kwa 10 years)

3. Etc etc etc,najua ujenzi jinsi ulivo na gharama zake,ukibebesha mtu mawazo ya JENGA KWANZA kabla ya chochote,tena unasema JENGA NYUMBA YA BIASHARA. Nadhani hauwi realistic,au haujui unacho kiongea in terms ya gharama halisi na maisha halisi ya mwajiriwa wa kitanzania.

Good day.
Ushauri wako nao ni ushauri mzuri maana hata mie nilikuwa sina uwezo wa kujenga lakini kwa kuwa kama kijana lengo langu lilikuwepo kichwani kwamba ipo siku nitajenga, nilichofanya miaka ile ya 2005 maeneo yalikuwa si bei sana kwa hapo Dar kwani nikajipatia eneo japo halijapimwa lakini nililipa 1 million tena ilikuwa pembeni ya mji pia nikajipatia na heka zangu 6 maeneo ya Vianze - Mkurunga kipindi hicho ekari moja ilikuwa haizidi hata laki moja (lakini leo pamoja na kwamba vyote sijavijenga but thamani yake imepanda maana sasa hivi ekari moja Vianze mpaka Malogolo inanunuliwa kwa 1 million na kule kwingine sasa hivi kwa kale kaeneo naweza kulamba hata 10+ million. (tayari hapa ela ambayo kidogo ambayo hata kujenga ilikuwa haiwezekani lakini leo hii nikiamua kumega kajisemu tayari nimepata mtaji na kasehemu kadogo kengine kanabaki kwa ajili ya kujenga, tufanye biashara huku uwe na rasilimali ya in case of anything inaweza kuwa tena dhamana ya kukurudisha relini)

Wazo la jamaa ni zuri ila lina condtion especially kwa mtu ambae ameajiriwa inakuwa ngumu kwa baadhi ya watu kutokana na aina ya kazi wanayofanya (kwa sababu ukiweka msimamizi anaweza kukuchakachua pia na mwisho wa siku biashara ikafa na nyumba huna) but kama utakuwa una muda kiasi unaweza ukafanikisha,
 
Mkuu ukweli ni kuwa nyumba ni basic need kama iliyo chakula.Issue ni aina gani ya nyumba na umiliki wake. Unaweza kuwa na nyumba ambayo unawea ipangisha ikawa asset inayoleta kipato. Ukiamua kwa mfano kuishi kwenye nyumba uliyoijenga ambayo kodi yake inawezakuwa TZS 800,000 hii kwako inakuwa ni 'implicity rent' kwa maana ya kwambaunailipa kila mwisho wa mwezi ingawaje huipokei (i.e. unasave). Hivyo ukiwa unaishi nyumba ambayo ‘alternatively' ungeweza pangisha maana yake unailipa kodi ambayo ungeipata au ungeilipa. Kwa hiyo watu wote waliojenga nyumba na kuishi humo ndani 'implicitly' wanalipa kodi, ingawaje si kwa watu wengine. Swala la umeme, maji na matumizi mengine ni yamsingi kwenye nyumba, iwe nyumba ya kupanga au la.
Hapo bold nimepapenda pia lazima tuelewe kwamba ultimate goal ya yote tunayofanya hapa duniani kama wanadamu ni kutafuta happyness hivyo kuna watu wamejiweka kwamba wao si wa kuishi sehemu nzuri siku zote hivyo kila siku unajibana tu. Ni kweli kwamba nyumba ukijenga na ukaishi inakukamua lakini kumbuka kwamba kama ni nyumba yako unakuwa na amani kwenye moyo wako kwa kuwa huwazi kupandishiwa kodi pia hata kama unalipa umeme na maji bado hata kama ungekuwa kwenye ya kupanga bado nako utalipa. Pia ni vizuri kuishi maisha ya kujiachia wakati ukiwa kwako bado umri haujasonga kuliko mtu anakuja kujenga ana miaka 50 mpaka 60, muda mwingi wa maisha yake ameishi kwenye nyumba za kupanga ambazo kiukweli chache huwa zipo katika kiwango though kibongobongo zinaonekana kiwango

Ukiangalia hela kama ndio chanzo pekee cha mafanikio kiukweli unaweza ukaingia choo cha kike kwani wakati mwingine ukiwa na amani kwenye moyo wako inakufanya akili ifanye kazi vizuri katika kufikiria mambo ya maana kwani unapokuwa kwako unakuwa unawaza kitu kimoja tu ni namna gani ya kuendesha familia yako na maisha kwa jumla
 
Huu ni woga tu wa maisha. Lengo la maendeleo ni kuwa mobile, sheltered, healthy na mambo kama hayo. Kuwa na fedha ni primary na inategemea na hayo hapo juu kama yako sawa. Biashara, kuajiriwa vyote ni vyanzo vya pesa. Pesa haiwezi kuwa inatosha. Ingetosha Bill Gates angeshajitoa na kuishi kivyake. Hii ni fact pia. How much is enough??? Kipimo unajiwekea mwenyewe na aidha baadae unaishi kwa amani au kwa pressure.

Kimsingi kabisa gari, nyumba ni kama tv, panga, sahani, etc. yaani kirahisisha kazi na kiokoa muda. Ikiwa kwako yaonekana luxury basi hata biashara utafeli. Tuangalie kwa mtazamo huu.

Na tena kwa taarifa yako angalia vizuri takwimu zako middle class sio kuwa na gari na nyumba. Middle class kwa Tanzania ni wachache sana. Unaonaje mtu mwenye Tsh million kadhaa kwa Tanzania ndio ana-qualify kuwa middle class. Kwa definition ya Wikipedia - US middle class ni wale wenye kipato cha kuanzia million 42 hadi million 162 kwa mwaka. Hapo ni sawa na kusema kiasi cha million 3.5 kwa mwezi. Kwa picha na mtazamo huu kwa Tanzania ni wachache sana tayari wanaweza kuwa na kipato hiki. Wengi wako chini kabisa ya middle class.

Kwa mtazamo wangu nafikiri kuwa lengo kuwe na jitihada za kila mmoja kuipata middle class and then tutapata opportunities zikifunguka na kutakuwa na idadi ya kutosha ya watu kui-support class ya juu yake, la sivyo class ya juu itaanguka vile vile. Unapoongelea haya mambo ya classes ni kama ujenzi wa nyumba ulivyo. Msingi ni bora kuliko kuta, na kuta ni bora kuliko paa etc. In any country, middle class ndio watumiaji, ndio waendesha uchumi na ndio mhimili wa maendeleo ya nchi. Si class ya kupuuzia. Ni class muhimu kuliko hawa mabillionea au wa chini yao. Na ni hawa middle class ndio wanawashikilia mabilionea, la sivyo wangefilisika. Middle class kwa lugha nyepesi hu-support lower classes and top classes. Hawa ndio highest spending force. In a way hawa ndio roho ya uchumi.

Mtoa mada jifunze zaidi kuhusu middle class na ujisomee zaidi kuhusu maisha bora ni yapi?

Hint: Maisha bora ni unayoishi sasa. Future can not be worked out better than the present.

Asante
 
ukiwa muoga wa maisha daima utaogopa kununua gari au kupanga nyumba nzuri ukidai unaweka hela..maisha hayana formula maalum kama vile hesabu..kuna watu wameanza kununua magari na sasa hivi ni matajiri, wengine walianza kuinvest au kujenga ili kukwepa kodi, sasa hivi ni maskini bado na wengine wamenunua viwanja hivi sasa miaka kumi hawajainua hata tofali.Mshauri wa maisha yako ni wewe mwenyewe, angalia ni lipi linakwenda kutegemea na wewe, njia alopita mwenzio akafanikiwa haimaanishi nawe utafanikiwa, alipopita mwenzio akashindwa haimaanishi nawe utashindwa, starehe zilizozidi zinaponza, lakini mfano mtu kuwa na gari hapa mjini sio starehe, kwa mtu mwenye kufanya kazi let say sehemu ,2 au 3 anahitaji gari, watanzania tujifunze kuwa gari sio luxury ni nyenzo ya kutufikisha sehemu kwa haraka, ila wengi wanadhani ni luxury kwa sababu wanatafuta magari ili kuvutia wanawake..ndio pale wananunua magari yenye kula mafuta mengi sana kuliko hata kipato..na wengi wanabweteka ti na mishahara ndo maana wanaogopa hata kuishi kwa raha make hana hata shughuli nyingine, na hawana shughuli nyingine kwakuwa wengi tunajidai tumesoma,,hata kama kuuza chips kunalipa zaidi ya kufanya kazi ofisini, mtu atataka akae tu ofisini ili apate heshima ya kufanyia kazi jengo zuri au kampuni nzuri.
Tusiwe waoga wa maisha,kila kitu kinawezekana, na mtu unafanya kazi ili uishi vizuri, kuwa busy, fanya kazi nyingi, panga nyumba nzuri, nunua gari, anza biashara wakati huo unaweka za kujenga nyumba yako, mawazo haya ya kuogopa kuoshi vizuri ndiyo yanafanya mtu aihame toka kwa wazazi wake eti anasubiri ahame akijenga kwake..huo ni uvivu na uoga,toka kwenu, panga, na tumia akili utajenga na utaanza miradi ya kwako..
na daima ukitumia hela unapata akili ya kutafuta zingine, ukikaa ndani unaziangalia unaogopa zisiishe hazitaisha kweli na bado hazitakufaa maana huzitumii.
Mawazo ya wanauchumi huwa ni mazuri, lakini jiuliza, yanaendana na maisha yako halisi?maisha hayana kanuni..tumia akili zote utaishi kwa faha na utafanikiwa...
 
Mkuu ukweli ni kuwa nyumba ni basic need kama iliyo chakula.Issue ni aina gani ya nyumba na umiliki wake. Unaweza kuwa na nyumba ambayo unawea ipangisha ikawa asset inayoleta kipato. Ukiamua kwa mfano kuishi kwenye nyumba uliyoijenga ambayo kodi yake inawezakuwa TZS 800,000 hii kwako inakuwa ni 'implicity rent' kwa maana ya kwambaunailipa kila mwisho wa mwezi ingawaje huipokei (i.e. unasave). Hivyo ukiwa unaishi nyumba ambayo ‘alternatively’ ungeweza pangisha maana yake unailipa kodi ambayo ungeipata au ungeilipa. Kwa hiyo watu wote waliojenga nyumba na kuishi humo ndani 'implicitly' wanalipa kodi, ingawaje si kwa watu wengine. Swala la umeme, maji na matumizi mengine ni yamsingi kwenye nyumba, iwe nyumba ya kupanga au la.

hivi umemuelewa mtoa mada? yeye anakwambia ukianza kwa kujenga utaishia kuwa middle class, maisha hayana formular. mbona wapo walioanza na biashara na matokeo yake biashara zimekufa na nyumba za kuishi hawana. hii kitu haina guarantee bali ni wewe mwenyewe utakavyojipanga kukabiliana na maisha.

nakubaliana nawe asilimia mia moja
 
Back
Top Bottom