Ukiwa na tabia hizi, jiandae kuwa middle class na kuteseka ki uchumi!

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,175
3,200
Wadau, hasa vijana wenzangu,

Ushauri kwa vijana wenzangu. Ukiona wewe kwanza ndiyo umepata kazi, ukaanza kwa kununua gari la kutembelea, baada ya hapo ukanunua kiwanja na ukaanza kujenga ujue wewe utaishia kuwa middle class na kuteseka ki uchumi katika maisha yako yote. Ninaposema kuteseka ki uchumi namaanisha kila ikihitajika laki moja wewe kuitoa mpaka ukope au ukitoa unaishiwa. Vijana wengi wanapenda kuishi maisha ya luxury wakati hawana sifa ya kuwa na luxury, unakuta ndani kwake kajaza vifaa expensive wakati hana rasilimali ya kumpa kipato, wengi wanafanya hivyo ili waonekane wako na maisha safi kwa jamii, kumbe wanajichimbia kaburi

Asilimia kubwa ya middle class walieanza kwa ku invest kwenye mambo yasiyozalisha, mfano nyumba ya kuishi mwenyewe au gari, ukianza, ukianza kwa kujenga nyumba ya kuishi wewe ndio mbaya kabisa. Watu tunaowaita matajiri, walianza kwa ku invest kwenye kitu kinachozalisha pesa then gari la kutembelea, nyumba vikaja baadae. Huo ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu

BAADA YA KUONA SIELEWEKI, NIMEONA NIWAPE MFANO HUU.

Hapa Tanzania, Wahindi wamekuwa waoga kujenga Tanzania kwa hofu kuwa labda hapa si kwao. Wahindi wanaishi National Housing kwa kupanga, ni mabillionaire, wameshika uchumi wa nchi hii, hawatishwi na kodi za nyumba, mfano kwa Arusha wanalipa kodi hadi 1.5m kwa mwezi kwa nyumba ambazo si national housing huko Arusha.
Sasa vipi wewe Mtanzania ungeanza na biashara then Nyumba?
 
Wadau, hasa vijana wenzangu,

Ushauri kwa vijana wenzangu. Ukiona wewe kwanza ndiyo umepata kazi, ukaanza kwa kununua gari la kutembelea, baada ya hapo ukanunua kiwanja na ukaanza kujenga ujue wewe utaishia kuwa middle class na kuteseka ki uchumi katika maisha yako yote. Ninaposema kuteseka ki uchumi namaanisha kila ikihitajika laki moja wewe kuitoa mpaka ukope au ukitoa unaishiwa. Vijana wengi wanapenda kuishi maisha ya luxury wakati hawana sifa ya kuwa na luxury, unakuta ndani kwake kajaza vifaa expensive wakati hana rasilimali ya kumpa kipato, wengi wanafanya hivyo ili waonekane wako na maisha safi kwa jamii, kumbe wanajichimbia kaburi

Asilimia kubwa ya middle class walieanza kwa ku invest kwenye mambo yasiyozalisha, mfano nyumba ya kuishi mwenyewe au gari, ukianza, ukianza kwa kujenga nyumba ya kuishi wewe ndio mbaya kabisa. Watu tunaowaita matajiri, walianza kwa ku invest kwenye kitu kinachozalisha pesa then gari la kutembelea, nyumba vikaja baadae. Huo ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu

Nimependa sana ushauri wako, ni kweli kabisa, Kuanza kwa kujenga nyumba ya kuishi ni sawa na kuzika pesa, ila watu wengi hili hawalijui kabisa na kuna baadhi ya nchi kisheria huruhusiwi kujenga nyumba kwa pesa yako mwenyewe kwa sababu wanafahamu madhara yake.

nIMEPENDAS
 
For your information! The richest investor in the world Warren Buffet alianza kujenga nyumba yake before hajaanza biashara alikuwa ameajiliwa wakati huo.
Nawashauri vijana in their 20's to build their career rather than entering into debts.
 
sidhani kama kuna ukweli, maisha ni kujipanga na kupanga ni kuchagua. nyumba na gari nayo ni mahitaji ya msingi sana tu ya kuanza nayo kama hukuwa navyo na haijalishi ununue vya kwanza au vya mwisho, jitihada binafsi ndio muhimu zaidi

Huo ni ukweli mtupu, mfano wewe unatumia milioni 60 kujenga nyumba ndani ya miaka 4, ukimaliza hiyo nyumba haizalishi chichote, unaishi mwenyewe, vipi kama hiyo 60 kama ungewekeza mfano kwenye ufugaji wa kuku, kama uko serious hao kuku wangekupa hata milioni 4 kwa mwezi na ukajenga kirahisi
 
For your information! The richest investor in the world Warren Buffet alianza kujenga nyumba yake before hajaanza biashara alikuwa ameajiliwa wakati huo.
Nawashauri vijana in their 20's to build their career rather than entering into debts.

Mkuu watu kama hao huwa wapo lakini ni wachache, mfano kuna mzee mmoja alifirisika akiwa na umri wa miaka 60, lakini alipambana hadi akawa tajiri hasa, lakini wangapi wanaweza kwa umri huo?. Gari inatoa pesa yako mfukoni, nyumba pia, baada ya hapo kuna mambo ya kuoa na kuzaa watoto ambao watahitaji ada, kwa staili hiyo hujawa middle class?
 
Huo ni ukweli mtupu, mfano wewe unatumia milioni 60 kujenga nyumba ndani ya miaka 4, ukimaliza hiyo nyumba haizalishi chichote, unaishi mwenyewe, vipi kama hiyo 60 kama ungewekeza mfano kwenye ufugaji wa kuku, kama uko serious hao kuku wangekupa hata milioni 4 kwa mwezi na ukajenga kirahisi
hivi umemuelewa mtoa mada? yeye anakwambia ukianza kwa kujenga utaishia kuwa middle class, maisha hayana formular. mbona wapo walioanza na biashara na matokeo yake biashara zimekufa na nyumba za kuishi hawana. hii kitu haina guarantee bali ni wewe mwenyewe utakavyojipanga kukabiliana na maisha.
 
For your information! The richest investor in the world Warren Buffet alianza kujenga nyumba yake before hajaanza biashara alikuwa ameajiliwa wakati huo.
Nawashauri vijana in their 20's to build their career rather than entering into debts.

nashangaa huyu anataka kutisha watu. hebu waangalie na kodi wanazolipa wenye nyumba sahv ndio waone kama kujenga nyumba mapema inalipa au lah.
 
kwa harakaharaka unaonekana kama huna kitu au una kipato kidogo n aunatafuta support tu hapa ya umaskini wako.........

kwani gari ni nini hadi likuogopeshe namna iyo?...mfano mimi n amke wangu tumepanga ila tuna gari..nikitumia gari nasevu sana kuliko hata kutumia bodaboda na daladala.......

kuhusu investiment hapa tumetofautiana...
 
Hiyo ni kweli kabisa angalieni mifano toka kwa wahindi.

Wengi wakianza kazi kitu cha kwanza kukimbilia ni Gari matokeo yake mshahara unaanza kuhudumia gari.

Tusijifananishe na marekani au ulaya. Uko watu hawanunui magari kwa cash ( pesa taslimu) kule unachukua tu gari na kukatwa pesa kidogo sana kwa kila mwezi ata nchi za Asia nimeona ili kwa macho yangu.

Pia bei ya magari si kubwa kama Tanzania.

Kutokuwepo kwa malengo mazuri imesababisha watu kulalamika kila siku maisha magumu nina ndugu zangu wengi ni waajiriwa kwa miaka 30 sasa lakin wanalalamika life ngumu.

Hikifika kuanzia tarehe 15 watu wako hoi pesa zishaisha. Mshahara ukichelewa kidogo utaona topic za kulalamika umu JF.

Maisha ni kuchagua. Ni ushauri tu si lazima ukubali.
 
Nikweli mkuu, au mtu kapanga chumba kimoja halafu kanunua gari lake na yeye anazunguka mjini. Ni vizuri kuanza na kitu kinachokuingizia kipato japo kidogo kwa siku.
 
Nimependa sana ushauri wako, ni kweli kabisa, Kuanza kwa kujenga nyumba ya kuishi ni sawa na kuzika pesa, ila watu wengi hili hawalijui kabisa na kuna baadhi ya nchi kisheria huruhusiwi kujenga nyumba kwa pesa yako mwenyewe kwa sababu wanafahamu madhara yake.

nIMEPENDAS
mi naona kuanza kwa kujenga nyumba ni muhimu sana, nyumba ni asset. kuliko kuendelea kupata gharama za kulipa wenye nyumba kodi bora uwe na kwako uokoe gharama za kodi.
 
hivi umemuelewa mtoa mada? yeye anakwambia ukianza kwa kujenga utaishia kuwa middle class, maisha hayana formular. mbona wapo walioanza na biashara na matokeo yake biashara zimekufa na nyumba za kuishi hawana. hii kitu haina guarantee bali ni wewe mwenyewe utakavyojipanga kukabiliana na maisha.

achana nae..hawa wamekariri maisha...!!yani mie na degree yangu nliyosotea kwa tabu nikae nakimbizana na bodaboda na daladala...wakat kuna vitz za milioni 4?aka mie!!!nyumba nitajenga tu kwani nalala nje?anipishe huko......kazi nafanya na biashara nafanya..ana jingine?
 
mi naona kuanza kwa kujenga nyumba ni muhimu sana, nyumba ni asset. kuliko kuendelea kupata gharama za kulipa wenye nyumba kodi bora uwe na kwako uokoe gharama za kodi.

wenzio wananunua gari na nyumba inaanzia apo apo......chezea mishahara ya 5m !!mkopo milion 100........
 
Back
Top Bottom