Ukipeleka shitaka Polisi kuna ulazima wa kupeleka na mshahidi?

Kijukuu

Member
Feb 2, 2014
39
12
Habari zenu ndugu, kwa wale wenye uzoefu pamoja na elimu ya SHERIA, naomba kuuliza

=>Unapopeleka kesi polisi kabla ya kwenda mahakamani, kuna ulazima wa polisi kuonana na mashahidi au mashahidi wanatakiwa waonekane mahakamani tu. Maana nimekuwa na wasiwasi kidogo.
 
Acha kimdanganya mwenzio mashtaka anandaa nani?
polisi sio sehemu ya kushitaki ni ya kulipoti na upelelezi.hili ni tatizo ni sawa na wale wanaomkamata mwizi na kumpeleka polisi alafu wanapotea bila kufungua kesi mahakamani alafu akiachiwa wanalalamika. polisi kazi yao ni kumshikilia mtuhumiwa ili asitoroke wakati haki inatafutwa.
 
iko hivi, kuna tukio ambalo nimeenda kuriport polisi na mtuhumiwa yupo ndani tayari tunasubir file liende mahakamani, ila leo siku kama ya 3 file halijafika alaf na polise anaomba aonane na hao mashahidi, ss ndio nikawa najiuliza ni sahihi police kuonana na mashahid kabla ya mahakama (au kuna mchezo tofauti)?
 
Ni sahihi maana kama ni jinai anayepeleka kesi mahakamni ni polisi (jamhuri), hivyo lazima awaone mashahidi, ila kama ni madai hiyo ni wewe ndo unapeleka mahakamani na hauna haja ya kupita polisi.
 
Habari zenu ndugu, kwa wale wenye uzoefu pamoja na elimu ya SHERIA, naomba kuuliza

=>Unapopeleka kesi polisi kabla ya kwenda mahakamani, kuna ulazima wa polisi kuonana na mashahidi au mashahidi wanatakiwa waonekane mahakamani tu. Maana nimekuwa na wasiwasi kidogo.
Wewe sio mimi kweli,yaani hili swali nilijiuliza jana
 
polisi unaenda kulipoti sio kushitaki. mashahidi na mashitaka hayo ni ya mahakamani.
Sasa je mlalamikaji na mashahidi zake wote wanakokwenda kituo cha polisi na kuchukuliwa maelezo ina shida yeyote kisheria?hili limetokea ndo maana nkauluza
 
Ipo hivi kuna kijana ni mtumishi wa uma alikuwa anashukiwa kwa wizi, ijapokuwa ushahidi wote uliotolewa polisi ulithibitika hakuhusika, polisi wali amuru kesi hiyo itolewe polisi ipelekwe halmashauri ambako mshukiwa ameajiriwa, wazee wetu mnawajua, wakamshauri na kumlazimisha akubali kulipa yaishe ili asije kurudishwa rumande, kutokana na woga na kutokujuasheria yule kijana alikubali kwakuweka sahihi ya malipo katika barua iliyo andikwa na afisa mmoja pale almashauri, sasa imefika hatua yule kijana ameshindwa kulipa na mdai wake anamsumbua sana, pindi anapopeleka huo ushaidi kwenye kituo chochote nchin yule kijana hukamatwa na kuwekwa ndani popote anapokuwa, sasa amechoka na anateseka, Mimi nilikuwa pamoja nae mwanzo wa hili jambo hadi sasa na niko tayari kusimamia mahakaman kam shahidi wake maana nashuhudia hakika hakutenda ilo tukio sasa yeye ameamua kwenda mahakamani maana mdai wake hataki kwenda, Anaomba msaada kwenu wana JF manguli wa sheria je afanyeje au apitie hatua gani ili kufungua madai yake?
maana anaamini kabisa ushahidi anao wakumvusha kwenye hili jaribuuu!
 
Back
Top Bottom