A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkazi wa Mwanza, Wilaya ya Ilemela naomba msaada kwa mamlaka zinazohusika kuhusu ndugu yetu.
Kuna ile habari ya yule kijana aliyekamatwa Namtumbo (Ruvuma) kwa kosa la kuhubiri watu wasisome ili wajipange kumpokea Yesu, Mtumishi wa Mungu Erick Manyanya ( 33) Mwinjilisti wa Kanisa la Country Living, huyo mtu ni ndugu yangu hata mimi sikubaliani naye kuhusu hizo hoja zake, lakini kuna jambo limenifanya niandike hapa.
Taarifa ni kuwa yule bwana kapigwa sana na baadhi ya Askari Polisi, hata kutembea hawezi na tangu kashikwa sasa anamaliza zaid ya zaidi ya wiki bila kupelekwa Mahakamani na haruhusiwi kupewa mdhamana mpaka itoke Shilingi laki mbili (Tsh. 200,000).
Pia kijana huyo kiukweli baada ya kumaliza form six, mwaka 2019 alikuwa kama hayuko sawa kiakili hasa katika mambo ya dini, maana alikuwa Roman Katoliki, baadaye akahamia kwa Walokole, akataka kuingia kwa Waislam ila hakufanikiwa.
Nilipojaribu kumhoji akasema anataka kujua dini ya kweli ni hipi.
Sasa baadaye aliingia Sabato ila hakuwa kama alivyo sasa, ila alivyofika chuo huko UDOM ndIo mambo yakawa mabaya zaidi.
Maana alikutana na Mwanafunzi mwenzie mwenye imani ya Wasabato Masalia, ndio akamrubuni waache chuo wakamsubiri Yesu huko vijijini.
Ombi langu kubwa ni juu ya Afya ya ndugu yetu, maana tunaambiwa mgonjwa kwa sababu ya kipigo na hakuna dhamana, Je, kosa hilo halina dhamana? au asipelekwe Mahakamani hadi leo, ikiwa ni wiki hadi sasa imepita.
Naomba msaada kwa mamlaka…
Pia soma:
= Namtumbo: Wazazi waacha kupeleka Watoto Shuleni wakiaminishwa Yesu Kristo anakaribia kurudi
= Ruvuma: Polisi yasema Muinjilisti aliyezuia Watoto kwenda shule bado anashikiliwa na hajapigwa na Askari