Ukikutana na kikwete, utamshauri nini?

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
298
Naona hali ya utawala wa JK inazidi kuwa mbaya, mambo haendi, mfumuko wa bei uko juu, viongozi wanalipuka, askari wanaua, wanafunzi wanafeli masomo, mishahara inachelewa. wafanyakazi hawajitumi, rushwa inazidi kuota mizizi, viongozi ni waongo,

Ikitokea ukapata nafasi ya kuonana na JK katika hali hii utamshauri nini.
 
Aachie ngazi haraka sana yeye na viongozi wake wakuu wote. Turudi kwenye drawing board tufanye uchaguzi mpya!!!
 
Asije akapendekeza mafisadi papa kugombea uraisi 2015 ataua chama kwani kiko icu
 
ajihuzulu.Rais anashindwa hata kutoa pole kwa watz wenzake anaowaongoza wa tarime!.urais aliupata kwa bahati mbaya ndo maana hajui kwanini watz ni maskini.
 
Apunguze sifa, majivuno na kuuza sura. Nitamshauri pia akunje uso wa mbuzi achape kazi, ushwahiba sio deal then safari zake zisizo na tija kwa taifa aachane nazo! Watanzania tushapevuka, we don't need Artists in serious issues!
 
Naona hali ya utawala wa JK inazidi kuwa mbaya, mambo haendi, mfumuko wa bei uko juu, viongozi wanalipuka, askari wanaua, wanafunzi wanafeli masomo, mishahara inachelewa. wafanyakazi hawajitumi, rushwa inazidi kuota mizizi, viongozi ni waongo,

Ikitokea ukapata nafasi ya kuonana na JK katika hali hii utamshauri nini.
Akae chini na apige hesabu ya gharama za ahadi zake zinafikia Tshs. ngapi na atueleze lipi linawezekana na lipi haliwezekani....................
 
Naona hali ya utawala wa JK inazidi kuwa mbaya, mambo haendi, mfumuko wa bei uko juu, viongozi wanalipuka, askari wanaua, wanafunzi wanafeli masomo, mishahara inachelewa. wafanyakazi hawajitumi, rushwa inazidi kuota mizizi, viongozi ni waongo,

Ikitokea ukapata nafasi ya kuonana na JK katika hali hii utamshauri nini.

Jambo kubwa ambalo nitamshauri yeye akiwa kama amiri jeshi mkuu wa majeshi yote likiwemo jeshi letu la polisi amfukuze kazi IGP Mwema kwa kutowachukulia hatua viongozi wa kisiasa wanaovunja amani na kuhubiri siasa za chuki wakiwemo viongozi waandamizi wa CHADEMA.

Ningemtolea mfano wa mwenzake Yoweri Kaguta Museveni anavyowashughulikia viongozi wakorofi kule Uganda.
 
nitamshauri ahachie ngazi/ang'atuke kuanzia kesho jioni. pia nitamueleza makosa yake ya kujibu the heague.
 
Back
Top Bottom