Ujuaji wa CHADEMA wawafanya wawe vipofu !

ThinkTwice Bro............. soma historia ya maana ya Kambi Rasmi halafu fikiria mara mbili kwa kilichotokea na what CHADEMA anachosimamia na kulilia on the same line.... sio kuropoka tu...............

Wakati Chadema imewatoa Zitto na Slaa kuongoza kamati za bunge wakati waliposhirikishwa na CUF kwenye kambi ya upinzani CDM hawakukiona hicho kifungu wamekuja kukiona baada ya kupata asilimia 12.5 za wabunge? Nadhani kuna vitu vingine vinawafanya sasa hivi watu waanze kuwasema vibaya chadema hii 12.5% imewatia kiburi hivi ikija kushika nchi kutakalika kweli? anyway tumbe kheri.
 
MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!

22.JPG

525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

(1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

(2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

(3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.

Mkuu tusiwe vipofu hawa NCCR wanaongoza moja ya halmashauri za kigoma unataka kuniambia wasiwe na uwakilishi ndani ya kamati za bunge? mimi hii nakataa na naona ni uroho na ubinafsi chama kunga'ng'ania na kuhodhi kila kitu! Au mimi nina matatizo ya kufikiri? ina maana wale wananchi wanaotoka kwenye ile halmashauri wasiwe na uwakilishi kwenye kamati hata moja kwenye bunge? huyo mbunge wao anafanya nini sasa ikiwa yupo bungeni kuangalia maslahi yao! fikirieni jamani tuache mapenzi na ushabiki wa kijinga hauendelezi ina unadumaza maendeleo yetu ya hivyo vyama tunavyovishabikia. Fikiria.
 
Wana JF hamjajua what is behind the scene! Sasa hivi CCM inahaha kuhakikisha kuwa nguvu ya CDM inapungua kila kukicha. Inapunguaje basi? Ni kwa kushawishi kila jambo wanalofanya CDM kuwa ni kibinafsi zaidi ili chama hicho kionekane ni chama cha watu wabinafsi wasiojali maslahi ya taifa. Hii ni baada ya kuonekana udini haujawashika ipasavyo japokuwa umewasumbua kiasi.
Kampeni hii inafanya na watu makini chini ya UWT kwa kucheza na loopwhole za sheria na kanuni mbali mbali mfano ni hii majuzi tu ilikuwaje bunge litoe tasfiri ya neno kambi rasmi ya upinzani wakati kanun yenyewe ukiisoma hadi mwisho inajieleza lakini ina mapungufu kwa kutokuwa wazi zaidi. Walijua wazi CDM ni lazima wangekataa kwa tafsiri ya mazoea waliyokuwa nayo.
Halafu CCM imechafuka sana kitaifa na kimataifa kutokana na kelele za CDM sasa nao wanalipa kisasi. Kila mbunge wa CDM ukimtoa Zitto ambacho kitakuwa kinasemwa kitaonekana ni kitu feki, kisicho na macho na ikibidi kuzomewa kichini chini ili kuwavunja nguvu wabunge wake.
Ni mtazamo tu.
 
Naomba kuuliza CUF katika hizo kamati hawajapata mwenyekiti? kama itakuwa vita yote ile ni kwa ajili ya vyama vidogo vya upinzania basi nawapongeza sana CUF kwa hilo. Ifike wakati kwa CDM kujenga vyama vidogo vya upinzani kama walivyojengwa wao ndani ya bunge. Labda tuwe wachoyo wa fadhila au wepesi wa kusahau hawa CUF wanaoonekana wabaya ndio waliofanikisha kina Slaa kuwika ndani ya bunge kupitia hizi kamati. Mtakumbuka kuwa CUF haikuongoza hata kamati moja kati ya zile tatu ambazo mbili walipewa CDM na Slaa na Zitto kuziongoza na moja walipewa UDP ikaongozwa na Cheyo. Ingekuwa CUF wanataka uongozi au ni waroho wa posho wasingeziachia hizi kamati! na kwa ninavyosoma comments za wengi watu hapa inaonesha kuwa CUF wanaelewana sana na CCM kama CUF wangekuwa hawaangalii maslahi ya taifa nina imani wangetumia fursa hii kuzichukua na kuzihodhi kamati zote tatu kwa maana CCM wasingewatosa! Ila ninachokiona ni kinyume chake.

Huu ni mtazamo wangu tu..................

JAMANI NANI KAKUAMBIA CUF SIO WAROHO WA MADARAKA???? SOMA ALAMA ZA NYAKATI - MBONA ZINZIBARI WAMEKUBALI SERIKALI YA MSETO NA CCM???? WAKATI ZAMANI WALIKUWA WAPINZANI WAKUBWA?? CUF NI WAROHO WA MADARAKA NA WAMEONA KUISHINDA CCM SIO RAHISI KWA WAO ILA WANAJIFANYA WEMAAAAAAA ILA YAMKINI SIKU MOJA WAUNDE SERIKALI YA MSETO HATA HUKU TZ BARA - WAFUNGE NDOA WAO + CCM - WABARA TUKO MAKINI SANA NA HATUDANGANYIKI................. kabla hawajafanya - tushaona mbali sana ............... CUF SIO WAPINZANI WA KWELI ......WAMESHANUNULIWA NA CCM - na mimi huo ndio Mtazamo wangu
 
"Kwa maana hiyo basi, CDM sasa wanauwezo wa kuchagua kutoka kambi yao tu mawaziri vivuli au kuchagua kutoka vyama vingine pia, kwa mie naona mawaziri vivuli ni kama wabunge wa viti maalum tu. Yale macho (kuongoza oversight committees zote 3) ambayo CDM walitegemea kuyapata hawana tena, hivyo basi watakuwa watazamaji zaidi kuliko watekelezaji zaidi."

sawa, lakini maneno yako yatapimwa na muda. Kujenga nchi hii maana yake ni kuachana kwa aslilimia 80% ya mawazo yaliyopo sasa. Ukilijua hilo utakuwa katika nafasi ya kubadilisha statement hii. ....likini nakuwa na wasiwasi na matamshi yako (see the highlighted and red) maana inafanana na watu fulani fulani
 
Naomba kuuliza CUF katika hizo kamati hawajapata mwenyekiti? kama itakuwa vita yote ile ni kwa ajili ya vyama vidogo vya upinzania basi nawapongeza sana CUF kwa hilo. Ifike wakati kwa CDM kujenga vyama vidogo vya upinzani kama walivyojengwa wao ndani ya bunge. Labda tuwe wachoyo wa fadhila au wepesi wa kusahau hawa CUF wanaoonekana wabaya ndio waliofanikisha kina Slaa kuwika ndani ya bunge kupitia hizi kamati. Mtakumbuka kuwa CUF haikuongoza hata kamati moja kati ya zile tatu ambazo mbili walipewa CDM na Slaa na Zitto kuziongoza na moja walipewa UDP ikaongozwa na Cheyo. Ingekuwa CUF wanataka uongozi au ni waroho wa posho wasingeziachia hizi kamati! na kwa ninavyosoma comments za wengi watu hapa inaonesha kuwa CUF wanaelewana sana na CCM kama CUF wangekuwa hawaangalii maslahi ya taifa nina imani wangetumia fursa hii kuzichukua na kuzihodhi kamati zote tatu kwa maana CCM wasingewatosa! Ila ninachokiona ni kinyume chake.

Huu ni mtazamo wangu tu..................

Chadema haijajengwa na CUF bungeni. Katika bunge la 9 hotuba zote za mawaziri vivuli zilikuwa zinaandaliwa na Chadema na kuandikwa na Chadema. Mawaziri vivuli wa Cuf walikuwa wanasoma tu hata walikuwa hawajui wanasoma nini. Semina elekezi za CHadema walialikwa Cuf vilevile kuja kujifunza. Na tumewafundisha sana tu. Wabunge wa Cuf wana uelewa mdogo wa mambo ya bara ndio maana wanaogopa kugombania uenyeviti wa hizi kamati hata ukiwasikia bungeni wanaongelea mambo ya muungano tu au mambo ya zanzibar. Na wanajua fika bila msaada wa Chadema hamna lolote watakaloweza kufanya bungeni. Mark my words na uangalia perfomance yao bunge hili.
 
Think Twice think twice mkuu kabla hujakurupuka. Usikae upande kwa watu wanaotawala kwa hila. Walichokuwa wanataka CHADEMA ni kufuata sheria na taratibu, lakini ccm fitna nyingi.
 
Kwa nini CCM wasiweke japo Naibu Waziri mmoja tu kutoka Vyama vya upinzani kama uchyo na Uroho wa madaraka unawahusu CHADEMA tu??
CCM wanagawiana vyeo kwa Chupi kila kona ya nchi wewe bado unawaona wachoyo ni Chadema tu??

Tangu lini Hoja ya CCM ikalenga kujenga Kambi ya upinzani???

Kupora na kuhodhi maana yake nini??

Zengwe likipigwa siku zote ni Suckers tu wanaoshangilia.

Baada ya Bunge la JMT kutoa tafsiri ya maana ya ‘Kambi ya upinzani bungeni’ ambapo lengo lake kuu lilikuwa ni kujali maslahi ya kitaifa zaidi na si ubinafsi wa watu wachache wenye uchu na uroho wa madaraka. Kamati mbali mbali za bunge jana zilifanya chaguzi zao za viongozi wa kamati hizo, ambapo CDM walipata kamati moja , UDP kamati moja na TLP kamati moja. Hili kwa kweli laonyesha ni mwanzo mzuri kwa wapinzani kuimarisha kambi yao, na si chama kimoja kuhodhi/kupora madaraka ya kambi nzima.
Kwa maana hiyo basi, CDM sasa wanauwezo wa kuchagua kutoka kambi yao tu mawaziri vivuli au kuchagua kutoka vyama vingine pia, kwa mie naona mawaziri vivuli ni kama wabunge wa viti maalum tu. Yale macho (kuongoza oversight committees zote 3) ambayo CDM walitegemea kuyapata hawana tena, hivyo basi watakuwa watazamaji zaidi kuliko watekelezaji zaidi.
 
Wabunge wa CUF hawana uzalendo kwa issue zinazoihusu Tanzania bara ikilinganishwa na wanavyo komaa kwa issue za zanzibar
 
Tatizo la CUF na CCM Wabunge wao wengi Shule ni za kuunganisha.

uelewa umejaa viraka vya kila aina.

Hapa kiraka cha Kanga ya Mwatex pale kiraka cha Madurufu huku makalioni kiraka cha Crimplin kwa mbele kiraka cha Gome la mnazi ili mradi kujaribu bila mafaniko kuficha uchi wa akili zao.

Chadema haijajengwa na CUF bungeni. Katika bunge la 9 hotuba zote za mawaziri vivuli zilikuwa zinaandaliwa na Chadema na kuandikwa na Chadema. Mawaziri vivuli wa Cuf walikuwa wanasoma tu hata walikuwa hawajui wanasoma nini. Semina elekezi za CHadema walialikwa Cuf vilevile kuja kujifunza. Na tumewafundisha sana tu. Wabunge wa Cuf wana uelewa mdogo wa mambo ya bara ndio maana wanaogopa kugombania uenyeviti wa hizi kamati hata ukiwasikia bungeni wanaongelea mambo ya muungano tu au mambo ya zanzibar. Na wanajua fika bila msaada wa Chadema hamna lolote watakaloweza kufanya bungeni. Mark my words na uangalia perfomance yao bunge hili.
 
Siasa ni mchezo,kuna wanaocheza kwa akili na wengine kwa hisia zao!!!mtabaki kulia tu wenye akili zao wanazitumia.:laugh::laugh:
 
Mkuu tusiwe vipofu hawa NCCR wanaongoza moja ya halmashauri za kigoma unataka kuniambia wasiwe na uwakilishi ndani ya kamati za bunge? mimi hii nakataa na naona ni uroho na ubinafsi chama kunga'ng'ania na kuhodhi kila kitu! Au mimi nina matatizo ya kufikiri? ina maana wale wananchi wanaotoka kwenye ile halmashauri wasiwe na uwakilishi kwenye kamati hata moja kwenye bunge? huyo mbunge wao anafanya nini sasa ikiwa yupo bungeni kuangalia maslahi yao! fikirieni jamani tuache mapenzi na ushabiki wa kijinga hauendelezi ina unadumaza maendeleo yetu ya hivyo vyama tunavyovishabikia. Fikiria.

Umeanza hoja vizuri lakini unaitetea katika namna ya hatari sana.

Kila jimbo linaloongozwa na chama tofauti wakitaka uwakirishi katika kamati za Bunge shughuli itakuwa pevu.

Kwa approach yako sidhani kama unaweza kujenga utetezi kiasi cha kutufanya sisi Tuwe na ushabiki wa kijinga.
 
Jana nilipata nafasi ya kuongea na kiongozi mmoja wa CDM, Taifa ambaye nilisoma nae. Kwa ujumla alikubaliana na mimi kwamba spidi waliyonayo wabunge wa CDM ukiondoa wale wazoefu kama Zitto, Mbowe na wengine kuna hatihati ya chama kupoteza umaarufu na imani hasa kwa watu makini na hivyo kuiachia CCM kuzidi kutamba katika ulimwengu wa siasa za Tanzania.
 
JAMANI NANI KAKUAMBIA CUF SIO WAROHO WA MADARAKA???? SOMA ALAMA ZA NYAKATI - MBONA ZINZIBARI WAMEKUBALI SERIKALI YA MSETO NA CCM???? WAKATI ZAMANI WALIKUWA WAPINZANI WAKUBWA?? CUF NI WAROHO WA MADARAKA NA WAMEONA KUISHINDA CCM SIO RAHISI KWA WAO ILA WANAJIFANYA WEMAAAAAAA ILA YAMKINI SIKU MOJA WAUNDE SERIKALI YA MSETO HATA HUKU TZ BARA - WAFUNGE NDOA WAO + CCM - WABARA TUKO MAKINI SANA NA HATUDANGANYIKI................. kabla hawajafanya - tushaona mbali sana ............... CUF SIO WAPINZANI WA KWELI ......WAMESHANUNULIWA NA CCM - na mimi huo ndio Mtazamo wangu

Usijibu kwa wahka mkuu, siasa za zanzibar zinahitaji mjadala mpana ila kwa ufupi wazanzibari walipiga kura ya maoni hao wazanzibari inainclude wana jahazi asilia, cdm, si unakumbuka matokea ya 2010 slaa alipata kura kadhaa zanzibar? basi hao waliompigia nao walipiga hiyo kura ya maoni kupendekeza serikali ya umoja wa kitaifa! Na sheria ikabadilishwa kuwa chama chenye uwakilishi zanznibar kitaunda serikali ya umoja wa kitaifa na chama kitakachoshinda hicho kifungu cha sheria hakikusema ni CCM na CUF peke yao wanaoruhusiwa kwa hiyo ni jukumu la CDM kuhakikisha wanakuwa na mipamngo ya kukubalika Zanzibar ili na wao waone watakataliwa?

Tusipende kujadili mambo kishabiki tujaribu kujadili nje ya mapenzi yetu ya kivyama tuweke utaifa mbele angalia wewe unafaidikaje kwa fulani kupata ulaji na unadhalilika vipi kwa fulani kukosa kuongoza kamati!
 
Jana nilipata nafasi ya kuongea na kiongozi mmoja wa CDM, Taifa ambaye nilisoma nae. Kwa ujumla alikubaliana na mimi kwamba spidi waliyonayo wabunge wa CDM ukiondoa wale wazoefu kama Zitto, Mbowe na wengine kuna hatihati ya chama kupoteza umaarufu na imani hasa kwa watu makini na hivyo kuiachia CCM kuzidi kutamba katika ulimwengu wa siasa za Tanzania.
Unamaana gani unaposema spidi waliyonayo, ni spidi ipi na itawapotezea vipi umaarufu
 
Kwa nini CHADEMA hawataki ushirikiano ? hapo ndipo watanzania hawawaelewi CHADEMA

Watanzania gani unaowaongelea na ni %? Labda wewe na wenzio wa CCM na CUF, naona na NCCR nao wamewajoin. Lakini wananchi tulio wengi tunaielewa vizuri CHADEMA
 
Chadema haijajengwa na CUF bungeni. Katika bunge la 9 hotuba zote za mawaziri vivuli zilikuwa zinaandaliwa na Chadema na kuandikwa na Chadema. Mawaziri vivuli wa Cuf walikuwa wanasoma tu hata walikuwa hawajui wanasoma nini. Semina elekezi za CHadema walialikwa Cuf vilevile kuja kujifunza. Na tumewafundisha sana tu. Wabunge wa Cuf wana uelewa mdogo wa mambo ya bara ndio maana wanaogopa kugombania uenyeviti wa hizi kamati hata ukiwasikia bungeni wanaongelea mambo ya muungano tu au mambo ya zanzibar. Na wanajua fika bila msaada wa Chadema hamna lolote watakaloweza kufanya bungeni. Mark my words na uangalia perfomance yao bunge hili.

HAtaka kama hotuba ziliandaliwa na Chadema lakini CUF ndio waliowapa fursa ya kuwa mawaziri vivuli na kupelekea kuandaa hizo hutuba.
 
Wekeni maslahi ya kitaifa mbele na acheni ubinafsi , hilo ndilo la kufanya

Hivi maslahi yakitaifa yangekuwa yamewekwa mbele na CCM toka enzi hizo tungekuwa hapa tulipo kweli, USD/TZS=1600/1, no umeme, fuel bei juu, watu wanaishindia mlo mmoja kwa siku 3, acha dharau zako wewe, nina uhakika iko siku lazima utajutia unayoyatetea jipe muda.
 
Back
Top Bottom