Ujuaji wa CHADEMA wawafanya wawe vipofu !

Wadau wapenda haki. Katika harakati za sasa zinazotokea Bungeni za Chadema kuwakataa CUF ukweli umebainika na hivyo msishangae. Jueni aliyenyuma ya yote haya ni Kanisa katoliki ambalo limeapa kuwa lazima Litawale nchi hii daima na ni marufuku imani yoyote ile kutawala.
Tusiwabeze wanaolalamika hapa Tanzania kuwa kuna UDINI. Ni kweli upo na ni SUMU kubwa.
Oneni wenyewe Programu ya kanisa katoliki kuhamisha MAFISADI KUTOKA CCM NA KUIBUKIA CHADEMA.
Wale wanaodhani kanisa lipo kupambana na Ufisadi si kweli. Bali lipo kufuga na kulea mafisadi ili waendelee kulitumikia. Hubadili tu TACTICS kila mara hasa wanapoona wanaelemewa. Ukweli ndio huo.
 

Attachments

  • waraka.pdf
    1.1 MB · Views: 82
Baada ya Bunge la JMT kutoa tafsiri ya maana ya ‘Kambi ya upinzani bungeni’ ambapo lengo lake kuu lilikuwa ni kujali maslahi ya kitaifa zaidi na si ubinafsi wa watu wachache wenye uchu na uroho wa madaraka. Kamati mbali mbali za bunge jana zilifanya chaguzi zao za viongozi wa kamati hizo, ambapo CDM walipata kamati moja , UDP kamati moja na TLP kamati moja. Hili kwa kweli laonyesha ni mwanzo mzuri kwa wapinzani kuimarisha kambi yao, na si chama kimoja kuhodhi/kupora madaraka ya kambi nzima.
Kwa maana hiyo basi, CDM sasa wanauwezo wa kuchagua kutoka kambi yao tu mawaziri vivuli au kuchagua kutoka vyama vingine pia, kwa mie naona mawaziri vivuli ni kama wabunge wa viti maalum tu. Yale macho (kuongoza oversight committees zote 3) ambayo CDM walitegemea kuyapata hawana tena, hivyo basi watakuwa watazamaji zaidi kuliko watekelezaji zaidi.

Kama wewe ni mtanzania halisi huoni kwamba CDM kukosa kamati hiyo ni hasara kwa taifa.Walitaka wazimulike sio kwamba wana uchu wa madaraka bali ni wapinzani wa kweli .Na ndio maana wabonge wa CCM wameona ni faraja kuwaweka watu kama Mrema na Cheyo kwana wataweza kucompromise nao.Ni kosa kubwa sana kwa usalama wa fedha zetu
 
Any person who thinks objectively will tell you CHADEMA are very right to refuse to cooperate with CUF.
 
Baada ya Bunge la JMT kutoa tafsiri ya maana ya ‘Kambi ya upinzani bungeni’ ambapo lengo lake kuu lilikuwa ni kujali maslahi ya kitaifa zaidi na si ubinafsi wa watu wachache wenye uchu na uroho wa madaraka. Kamati mbali mbali za bunge jana zilifanya chaguzi zao za viongozi wa kamati hizo, ambapo CDM walipata kamati moja , UDP kamati moja na TLP kamati moja. Hili kwa kweli laonyesha ni mwanzo mzuri kwa wapinzani kuimarisha kambi yao, na si chama kimoja kuhodhi/kupora madaraka ya kambi nzima.
Kwa maana hiyo basi, CDM sasa wanauwezo wa kuchagua kutoka kambi yao tu mawaziri vivuli au kuchagua kutoka vyama vingine pia, kwa mie naona mawaziri vivuli ni kama wabunge wa viti maalum tu. Yale macho (kuongoza oversight committees zote 3) ambayo CDM walitegemea kuyapata hawana tena, hivyo basi watakuwa watazamaji zaidi kuliko watekelezaji zaidi.

1. Kama lengo la kubadili kanuni ni kujali maslahi ya kitaifa, kwa nini utata wa tafsiri kuhusu Kanuni za Bunge utokee tu pale ambapo Chadema wameweza kupata wabunge wengi zaidi na hivyo kustahili kuunda kambi ya upinzani bungeni na siyo wakati CUF ilipokuwa na haki hiyo?

2. Mimi naona ni heri wakose hizo kamati na "wawe wasikilizaji zaidi kuliko watendaji" kama unvyosema kuliko kukubali mbinu chafu wanazotendewa na CCM pamoja na washirika wao.

3. Wananchi ndio wanaoona mambo wanayosimamia na siyo lazima washikilie hizo nafasi nyeti bungeni.

4. Sijawahi kuona CCM wakishangilia vyama vya upinzani kuungana kwa namna yoyote ile. Na kwa vile kwa kubadili Kanuni za Bunge CCM walishangilia zaidi kuliko wapinzani wenyewe, ni dhahiri kuwa mwungano ulipo sasa hauna maslahi yoyote ya kitaifa bali kudhoofisha Kambi ya Upinzani.

5. Kwa sasa hivi CUF si chama pinzani tena bali 'quasi-opposition' party kwa vile kule Zanzibar wanaungana na CCM kuunda serikali ya mseto. CUF ina national chairman mmoja na secretary general mmoja tu. Kwa hiyo, kuungana na CUF (quasi-opposition party) kwa nia ya kuwa na Kambi imara ya Upinzani ni kujidanganya tu.
 
Kama hivi karibuni umetafuta nyumba ya kupanga ama kununua katika jiji la Dar basi lazima ulikutana na dalali. Huyu lazima alikaa kati yako na mwenye nyumba na sifa yake kubwa ni kujiona anajua sana masuala ya nyumba na makazi. Dalali ni msumbufu sana hujidai anajua sana sheria na mara nyingine huongea hata kumshinda mwenye nyumba. Nahisi CUF itakua imeanza udalali wa siasi za TZ, ikulu patamu na mtaani patamu. Kwa utashi wangu naamini wao ni dola, kama ilivyo CCM sasa kujiita wapinzani what do they want to achieve. Nadhani ni vema wakashirikiana na ccm kutekeleza ilani ya ccm itasaidia sana kuiongezea nguvu ccm visiwani. Nasikitika kuna sheria inatungwa kuhukumu kosa ambalo mtuhumiwa wake tayari yupo kizimbani! Ushauri wa bure kwa ccm, isijikite sana kwenye matokeo ya muda mfupi...iangalie matunda ya kiburi chake siku za mbeleni!
 
Naomba kuuliza CUF katika hizo kamati hawajapata mwenyekiti? kama itakuwa vita yote ile ni kwa ajili ya vyama vidogo vya upinzania basi nawapongeza sana CUF kwa hilo. Ifike wakati kwa CDM kujenga vyama vidogo vya upinzani kama walivyojengwa wao ndani ya bunge. Labda tuwe wachoyo wa fadhila au wepesi wa kusahau hawa CUF wanaoonekana wabaya ndio waliofanikisha kina Slaa kuwika ndani ya bunge kupitia hizi kamati. Mtakumbuka kuwa CUF haikuongoza hata kamati moja kati ya zile tatu ambazo mbili walipewa CDM na Slaa na Zitto kuziongoza na moja walipewa UDP ikaongozwa na Cheyo. Ingekuwa CUF wanataka uongozi au ni waroho wa posho wasingeziachia hizi kamati! na kwa ninavyosoma comments za wengi watu hapa inaonesha kuwa CUF wanaelewana sana na CCM kama CUF wangekuwa hawaangalii maslahi ya taifa nina imani wangetumia fursa hii kuzichukua na kuzihodhi kamati zote tatu kwa maana CCM wasingewatosa! Ila ninachokiona ni kinyume chake.

Huu ni mtazamo wangu tu..................

Hivi hizi kamati wanapeana tuuuu bila kuangalia uwezo wa mtu!

Kumbe kamati ni posho....!

Tanzania zaidi ya tuijuavyo!



 
Back
Top Bottom