Ujio wa Kamala Tanzania na viongozi wengine wa Marekani waliowahi kufika Tanzania

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,035
Hii ni orodha fupi ya baadhi ya viongozi wa Marekani ambao wamewahi kutembelea Tanzania kwa nyakati mbalimbalu.

1. Rais Barack Obama: Aliitembelea Tanzania mwaka 2013 akiwa madarakani na kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete

2. Rais Bill Clinton: Aliitembelea Tanzania mara kadhaa wakati wa utawala wake, ikiwa ni pamoja na ziara yake ya kihistoria mwaka 1998 ambapo alizungumza na wakazi wa jijini Dar es Salaam baada ya kutokea kwa mashambulizi ya bomu katika ubalozi wa Marekani.

3. Rais George W. Bush: Aliitembelea Tanzania mwaka 2008, ambapo alikutana na rais wa Tanzania wakati huo, Jakaya Kikwete na kutia saini makubaliano ya MCC

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris anatarajiwa kuanza zaira nchini Tanzania Jumatano tarehe 29/03 hadi 31/02/2023

Kwa mliokuwepo zamani kipi mnakumbuka katika ziara hizi, mimi nakumbuka barabara zilivyopigwa deki na lile lindege la Rais
 
Wenyeji walipaswa kutambua umuhimu wa kupatiwa elimu iliyo bora toka kwa hao wageni(Marekani), tunahitajia elimu iliyo bora sana ili kuweza kupata maendeleo katika nyanja zote kwani elimu zote ziko kiwango cha chini sana.

Mh Raisi Samia ebu weka mkakati wa kupeleka vijana kupata elimu iliyo nzuri kwa manufaa ya taifa letu hapo baadae na isiwe kuja kwao ni kuwekeza tu, hayo tunaweza waruhusu watufanyie kwa baadae tukiwa na ufahamu wa kinachofanyika haswa kwa kuwa na elimu yenye tija.

Nchi iko na vitu vingine vidogo ambavyo ni muhimu kwa mustakabali wa nchi lakini kwa ufinyu wa elimu tunashindwa viendea kwa weledi na kutupa pesa nyingi kwa kampuni za kigeni ambazo zimechota utaalamu toka kwa marekani .
 
Back
Top Bottom