'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi

Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

Punguza jazba!

Kwanza nakupa pole kama ulianzisha kijishule ukidhani ni mradi wa kujipatia kipato. Elimu ni huduma kwa jamii na ndivyo ilivyo ktk nchi zote duniani. Hapa kwetu hao wanaojiita wenye shule binafsi wamekimbilia wakidhani ni biashara na wanajaribu sana kuendesha elimu kama biashara. Ada za kipuuzi kabisa, au ada wastani na kuongeza mambo ya kipuuzi.

Mara mchango wa maktaba, mara mchango wa gari la shule, mara mchango wa masomo ya kompyuta, nk.

Usilaani maamuzi ya ikulu. ukitaka biashara fungua guest house au restaurant. Pamba utakavyo, pika na weka viungo utakavyo kuvutia wateja. Elimu, Hapanaaa! lazima iongozwe na serikali. Kama unataka kuwachezea disco wanafunzi wako kila siku jioni kwa gharama za wazazi, acha! hao ni vijana wa Taifa la Tanzania.
 
Mi nimemuelewa mtoa mada,japo nnaukakasi kidogo juu ya hoja yake ila nipo upande wake, kiufupi serikali inataka kujificha nyuma ya shule binafsi ili ionekane inajali elimu kwa ada elekezi, iboreshe shule zake hizo zenyewe zitakufa kifo cha asili kama yalivokufa mashirika ya umma na mengne yamebaki kwa mwendo wa jongoo..Nenda posta huwa nacheka mpka.. walivokuwa na jeur enzi zao hata siamini
 
Bila shaka ww ni mnufaika... kazi moja wapo ya serikali ni kuwa regulator kwamba matendo ya watu binafsi kwenye secta zenye public interests lazima yatazamwe kwa undani hasa athari zake kwa jamii
Hivyo basi ni jukumu la serikali ku regulate elimu kwasababu ni jukumu lake ku assure elimu bora kwa jamii
Ukija kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa sealing and floating prices kwahiyo lazima ada ziwe regulated wala siyo ombi kwakua elimu ni public interest
NB: shule za serikali zita compete vp na private wkt private wanatoza bei za ajabu na kupora walimu wote wazuri toka serikalini kwakua wana uhakika wa kuwamwagia mapesa?
 
Duh huyu jamaa anatukana taasis ya rais sijui jeuri anatoa wapi.
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za Walipa kodi. Porojo hatutaki!

Mleta mada Ubongo wako hauna mawasiliano na ulichokiandika.Ugolo mtupu.
 
We sema2 kama unataka kuendelea kukuza ada ya shule yako maake unajua wanafunz hawawez kuama baada ya kuanza
 
Hii tabia ya serikali kuanza kuirudisha nchi kwenye mfumo wa ujamaa, ambao ulithibitika kwa vitendo kuwa mfumo wa kijinga, usiotekelezeka, unaogandisha mawazo na unaowafanya viongozi kuwa watawala pekee na siyo viongozi kweli; ni upotofu na udikteta wa hali ya juu. Serikali yoyote inayopanga bei ni serikali ya wajinga, wenye mawazo mgando na madikteta!

Hivi karibuni serikali ya ccm na magufuli wametangaza kuzuia shule binafsi kupandisha ada eti wangoje kile ambacho ikulu walikiita "ada elekezi".

Nasema huu ni ujinga kwa sababu kinachopaswa kuihusu serikali katika shule binafsi ni kuhakikisha wanafuata mtaala wa nchi tu. Tofauti na hapo hakuna kingine. Kumbukeni hakuna kodi yoyote ya mtu iliyotumika kujenga ama kugharamia chochote kwenye hizi shule!

Sasa kwa nini waingiliwe?! Hivi serikali haitupi ujumbe kwamba kwenye shule binafsi ndiko kuliko na elimu bora na kwa hiyo haki ya kupata elimu bora maana yake ni haki ya kusoma kwa bei ndogo kwenye shule binasi?!

Boresheni shule za walipa kodi. Porojo hatutaki!

Hili nalo ni Jipu linaloanza kuiva!....
Akiri za Nyumbu wa Ufipa hizi!...
 
Kama Serikali inatoa waraka juu ya bei elekezi katika bidhaa kama mafuta au kwenye vyombo vya usafiri kwanini isiwe kwenye shule? Jiandae kisaikolojolia na kishule chako hicho
 
Kwenye suala la ada elekezi kwa shule binafsi hata sikubaliani naye Dr Magufuli,hizi shule zina miundombinu mizuri,zinaajiri mpaka wafanyakazi wa kawaida wasio na utaalamu wowote kama vile watunzaji mazingira na wapishi.Pia zinajitahidi kuajiri Walimu wazuri kwa malipo mazuri.Isitoshe hizi shule haziwalazimishi wazazi au walezi kuwapeleka vijana wao huko,ni utashi wao tu ndio unaowapeleka huko.
 
Shule sio biashara wewe kama mnataka biashara kafungueni mabelo ya mitumba
 
Na sasa tutaangalia ulipotoa pesa ya kuanzishia hiyo shule yako.
 
subiri hayo maelekezi ndo ujue una hoja ya kuanzisha uzi au la. Ewura na sumatra hulalamiki. Hapa umeguswa nini ?

nakemea mifumo yote ya kupanga bei. Ewura na sumatra wakiwemo pia. Makampuni binafsi ya maji na umeme yakianzishwa na kutoa huduma zile zile hakuna atakayeteswa na ukiritimba wa mamlaka za maji na tanesco. Hivyo hivyo katika usafiri: Reli, majini, na angani.
 
Hivi vituo vya mafuta kumbe vyote vimejengwa na serikali ndiyo maana vimeundiwa EWURA???.
Wewe mdau wa shule kajipange upya ila kwa sababu hiz ulizotoa kwenye thread yako hazina mashiko.
Kila jambo linahitaji mwongozo na taratibu zake.
 
Hiz shule ni za kufuta kabisa, zmesababisha matabaka katika jamii alafu zilikuwa zinachangia kwa watumishi wa umma kupiga madili ili waweze kumudu hizo ada ili watutambie sisi masikini kwamba watoto wao wanasoma shule za gharama.
 
hivi watanzania mnataka nn jamani? Mbebwe migongoni na raisi ndo muone serikali inafanya kazi, mshatunyonya sana na upandishaji wenu wa ada kiholela mmefanya shule kuwa biashara, hizo ada elekezi zitasaidia sana, tulipokuwa tunaelekea ada za nursery tu zingefika 5ml

idai serikali yako ikupe mrejesho wa kodi yako kwa kukujengea shule na kuajiri walimu wenye sifa na viwango. Wapewe pia maslahi mazuri na dhana za kufundishia .kwa ujumla mazingira ya kujifunzia na kufundishia yawe mazuri.
 
Ukimkimbiza chini uchi kunakuwa hakuna tofauti yako na huyo chizi. Hata mumueleweshe vp hataelewa.anawaza kufilisika tu huyo baada ya bei elekezi .
 
Ujinga ni kuanzisha mada ya jambo usilo na weledi nalo. Hakuna taifa lisilo na mfumo wa Bei elekezi kwa kuwa wafanyabiashara by nature ni Profit maximizer. lengo la serikali ni kulinda na kutetea maslahi ya Raia na ndio sababu utakuta wakati mwingine inatoa ruzuku mpaka kwa taasisi binafsi kama shule na hospital ili kuboresha huduma zao, Hutoa misamaha ya kodi kwa taasisi hizo n.k ndio sababu kwny uchumi unaambiwa hakuna pure capitalist state or pure socialist state kazi ya serikal ni kuingilia ili kulinda maslahi ya Raia wakati wowote. Mbona hulalamiki wakipanga bei elekezi ya Fuel, nauli n.k Ile tabia yenu ya kujipandishia ada kama vile Nchi haina serikal ilifika mwishi siku jk alipokabidhi madaraka nov 5. mnawatoza wazazi na walezi ada halafu ikitokea mnataka kuongez Madarasa mnaitisha michango ya ujenzi kama vile ni shule ya serikal mbona Bakhresa au Mengi akitaka kutanua biashara zao wanaenda benk au ku issue share badala ya kutembeza bakuli kwa wateja? mnataka mruhusiwe mcharge gharama kibiashara lakin hamuendeshi kazi zenu kibiashara kutwa mko wizarani kuomba ruzuku na misamaha ya kodi, wazazi wanalipa kodi lakin kila mpango wa kuendeleza shule lazima mkamue wazazi nje ya ada wanayolipa. Hili jipu lishatumbuliwa kazi iliyobaki ni kusafisha tu kidonda. Jk alipelekewa hiyo sera muda mrefu akawa anawaonea aibu sasa kazi kapewa Kauzu zaidi ya Dagaa mwendo wa sura ya mbuzi hakuna kuchekeana

naunga mkonyo hoja! Gamba
 
Back
Top Bottom