Ujinga, maradhi, umaskini, imani za kishirikina na imani za kuamini dini za wakoloni ndio maadui wa Tanzania

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,873
6,283
Hawa ndio maadui wa Taifa letu:

1. Ujinga

2. Maradhi

3. Umaskini

4. Imani za kishirikina yaani ( kuamini uchawi , waganga wa kienyeji na Maustaz wasoma Nyota na kutoa majini )

5. Imani za Dini tulizolotewa na wakoloni ambazo ni ukristo na uislamu.

Hawa watano ndio maadui wa kweli wa Taifa letu.
 
Miaka hii wananchi wameelevuka sana. Unaposema ujinga.. naona kama haupo au umeisha sana. Hapa nazungumzia ujinga wa kutokuwa na elimu. Angalau watu wameelimika kwa kiasi fulani. Kutokana na elimu hiyo hata maradhi yameweza kupungua watu wanatumia chakula dawa na dawa kwa kiasi kikubwa. Hakuna masikini... ni watu tu kutojituma na kukata tamaa. Ushirikina umebaki wa kurithi... Imani za dini zimesaidia sana kutupa elimu ya maisha. Hii ni ukilinganisha ya miaka ya huko nyuma.... huko tunakoenda kuna mwanga zaidi.
 
Hapo namba tano pana shida gani?

ni imani za uongo. Maombi wala sala haziwezi kusolve matatizo yetu.

dini ni nyenzo inayotumiwa na tabaka tawala kuwahadaa na kuwapumbaza watawaliwa.

1. Kwa kuwaaminisha watu kuwa mamlaka yao ya kutawala 'yametoka kwa Mungu'.

2. Kuwataka watu wasiwe na tamaa ya maisha mazuri hapa duniani, wangojee wakifa ndio watafaidi wakienda huko mbinguni 🤣🤣🤣🤣. Wakati huohuo hao watawala wanaishi maisha ya kifahari kwa gharama za watawaliwa hapa hapa duniani.
 
dini zinaleta uvivu wa fikra

kuamini mungu ndo chanzo cha kila kitu kunafanya watu washindwe kuchanganua mambo kwa undani

kwa mtazamo wangu ushirikina na dini vinapaswa kukaa kwenye kundi moja

Dini na ushirikina zinaendana. Na zilitengenezwa kwa dhumuni moja la kumtisha na kumtawala binadamu..

Ili Simba ipate mashabiki lazima na Yanga iwepo.
 
Hawa ndio maadui wa Taifa letu

1. Ujinga

2. Maradhi

3. Umaskini

4. Imani za kishirikina

5. Imani za Dini tulizolotewa na wakoloni ambazo ni ukristo na uislamu.

Hawa watano ndio maadui wa kweli wa Taifa letu.
Unafiki na roho mbaya
Ukabila
Anasa
 
Wakati huo, walioleta dini ndio walioleta elimu mbalimbali ambapo ziliwafungua watu wa enzi hizo ambao walizoea kukaa sehemu moja na hawakuwa na uelewa wa mambo ya sehemu nyingine. Dini zina faida yake na hasara zake ila kwa ujumla zilianza kufanya watu wajue kusoma na wajielewe zaidi. Hapa nazungumzia kabla dunia haijawa kijiji. Dini pia zilisaidia kuunganisha dunia kuelekea kuwa kijiji.
 
sidhani kama elimu dunia ina uhusiano na dini

kiliunganisha dunia kuwa kijiji ni internet na maendeleo ya tehama

dini inachofanya ni kutenganisha dunia
 
sidhani kama elimu dunia ina uhusiano na dini

kiliunganisha dunia kuwa kijiji ni internet na maendeleo ya tehama

dini inachofanya ni kutenganisha d#

Hao walioeleta dini ndio walieleta elimu dunia. Walifungua shule na babu na mabibi zako ndio walisoma huko.
sio internet tu iliunganisha dunia. Unaangalia juu juu tu, hebu jaribu kuchimba chini utaona kulikuwa na barabara za kuunganisha eneo hadi eneo, kulikuwa na wamishenari na watumwa, kulikuwa na biashara za kubadilishana .... watu walisafiri kwa maji na barabara. Hii tehama ya juzi ni matokeo ya elimu baada ya technology kukua.
 
Hawa ndio maadui wa Taifa letu:

1. Ujinga

2. Maradhi

3. Umaskini

4. Imani za kishirikina

5. Imani za Dini tulizolotewa na wakoloni ambazo ni ukristo na uislamu.

Hawa watano ndio maadui wa kweli wa Taifa letu.
Unapinga imani za kishirikiana na bado unapinga dini zilizoenezwa na wakoloni.

Jitafakari.
 
Unapinga imani za kishirikiana na bado unapinga dini zilizoenezwa na wakoloni.

Jitafakari.

Imani za kishirikina nimemaanisha watu kuamini uchawi upo huku uhalisia uchawi haupo na haujawai kuwepo.

Uchawi na dini ni vitu vinavyoendana kama simba na yanga. Maana vitabu vya dini vinaongelea uchawi pia.

MTU ANAEAMINI UCHAWI NI MVIVU WA KUFIKIRI

Watu wanaoamini uchawi na ushirikina kikawaida hupenda shortcut, hawapendi kuumiza akili, kushughulisha ubongo.

Uchawi haupo na haujawai kuwepo. Kama vile Mungu alivyokuwa hayupo
 
Hawa ndio maadui wa Taifa letu:

1. Ujinga

2. Maradhi

3. Umaskini

4. Imani za kishirikina

5. Imani za Dini tulizolotewa na wakoloni ambazo ni ukristo na uislamu.

Hawa watano ndio maadui wa kweli wa Taifa letu.
Taifa limetengeneza kizazi cha wajinga, wavivu kufikiri.
 
dini zinaleta uvivu wa fikra

kuamini mungu ndo chanzo cha kila kitu kunafanya watu washindwe kuchanganua mambo kwa undani

kwa mtazamo wangu ushirikina na dini vinapaswa kukaa kwenye kundi moja
Ushirikina na dini vipo kundi moja mkuu , hauoni taarifa ikitolewa humu "kuna mtu kameza panga huko geita", utasikia " Alafu kuna majinga yanasema hakuna Mungu"

Apo ni pipa na mfuniko.
 
Hawa ndio maadui wa Taifa letu:

1. Ujinga

2. Maradhi

3. Umaskini

4. Imani za kishirikina

5. Imani za Dini tulizolotewa na wakoloni ambazo ni ukristo na uislamu.

Hawa watano ndio maadui wa kweli wa Taifa letu.
Waliozileta ndio wenye dini? Ni dini gani iliyoanzia ulaya, naomba unieleweshe ili tujadiliane vizuri.
 
Back
Top Bottom