Ukiacha wale Maadui Pendwa wa Taifa wa toka kale, Uchawa ndio adui namba moja kwa Taifa kwa sasa

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
5,050
5,078
Ujinga, Maradhi na Umasikini vilitajwa kama maadui wakuu wa Taifa letu. Sijui watu walioorodhesha hawa maadui walitumia vigezo gani lkn ndio wimbo tumeimbishwa zaidi ya nusu karne sasa lkn bahati mbaya hatujaweza kuwaondoa hawa maadui.

Kama Ujinga ndio kama umeota mizizi, Umasikini ndio kabisaa umeunga udugu na Watz na Maradhi ndio usiseme.

Bahati mbaya sana pamoja na hawa maadui kua hawajatoka, kaibuka ADUI mwingine wa Taifa ambaye anaitwa UCHAWA. Na bahati mbaya bwana huyu adui ndio anaongoza hawa maadui wengine.

Yaani Taifa sasa ili uonekane unafaa lazma uwe chawa, ubaya sana wale wanaoitwa nguvu kazi ya Taifa, kwa maana ya Vijana tena Wasomi ndio MACHAWA wakuu. Yaan unamsikiliza kijana awe kiongozi au nje ya uongozi akiongea unatamani kumzaba kelebu, yaani ataongea dakika 20 lkn hana hoja ya maana atakayojenga zaidi ni kusifia watu (personality) na hapo kama atakua hatafuti teuzi basi anatetea uteuzi wake.

Sikuhizi vijana wanapewa sana nafasi iwe ktk chama au Serikali lkn ajabu badala waoneshe tofauti ktk kaz wanazofanya aisee kila akiinuka ni kusifu watu na sio kuzungumzia hoja. Unabakia kujiuliza hivii hawa wangekua na jukumu la kupambana na Ukoloni tungekaa tupate uhuru?

Bahati mbaya sahii hatupo kwenye mapambano ya kutafuta Uhuru wa kisiasa bali uhuru wa kiuchumi ambao kama Taifa hii vita inapaswa kuongozwa na Think Tank ambao wana maarifa na mbinu tunduizi lkn ajabu kabisa wale kina nyerere wa zama hizi hawana uwezo wa kujenga hoja ktk vikao, hawana uwezo wa majadiliano, hawana uwezo wa kupambana na wataalam wa Mikataba je Kama Taifa tutashinda hii vita?

Tutafakari kama Taifa na kuchukua hatua
 
Uchawa na kuimba mapambio kidwanzi ni janga kwa kweli,

kipengele ni kuwa kwenye kupaza ukweli kichwa kinafutikwa chini ya mchanga ikitumainiwa mwili mzima hauonekani kama fikra za mbuni na kisha kuendekeza hiyena hiyena
 
Ujinga, Maradhi na Umasikini vilitajwa kama maadui wakuu wa Taifa letu. Sijui watu walioorodhesha hawa maadui walitumia vigezo gani lkn ndio wimbo tumeimbishwa zaidi ya nusu karne sasa lkn bahati mbaya hatujaweza kuwaondoa hawa maadui. Kama Ujinga ndio kama umeota mizizi, Umasikini ndio kabisaa umeunga udugu na Watz na Maradhi ndio usiseme.
Bahati mbaya sana pamoja na hawa maadui kua hawajatoka, kaibuka ADUI mwingine wa Taifa ambaye anaitwa UCHAWA. Na bahati mbaya bwana huyu adui ndio anaongoza hawa maadui wengine. Yaani Taifa sasa ili uonekane unafaa lazma uwe chawa, ubaya sana wale wanaoitwa nguvu kazi ya Taifa, kwa maana ya Vijana tena Wasomi ndio MACHAWA wakuu. Yaan unamsikiliza kijana awe kiongozi au nje ya uongozi akiongea unatamani kumzaba kelebu, yaani ataongea dakika 20 lkn hana hoja ya maana atakayojenga zaidi ni kusifia watu (personality) na hapo kama atakua hatafuti teuzi basi anatetea uteuzi wake. Sikuhizi vijana wanapewa sana nafasi iwe ktk chama au Serikali lkn ajabu badala waoneshe tofauti ktk kaz wanazofanya aisee kila akiinuka ni kusifu watu na sio kuzungumzia hoja. Unabakia kujiuliza hivii hawa wangekua na jukumu la kupambana na Ukoloni tungekaa tupate uhuru?
Bahati mbaya sahii hatupo kwenye mapambano ya kutafuta Uhuru wa kisiasa bali uhuru wa kiuchumi ambao kama Taifa hii vita inapaswa kuongozwa na Think Tank ambao wana maarifa na mbinu tunduizi lkn ajabu kabisa wale kina nyerere wa zama hizi hawana uwezo wa kujenga hoja ktk vikao, hawana uwezo wa majadiliano, hawana uwezo wa kupambana na wataalam wa Mikataba je Kama Taifa tutashinda hii vita?
Tutafakari kama Taifa na kuchukua hatua
nadhan unyumbu, mihemko, malalamiko crew, puppet elements zimetuchelewesha na kuturudisha nyuma sana sana 🐒
 
Inategemea MTU na MTU Ila taifa linasumbuliwa na UJINGA maana ukiushinda UJINGA hauwezi kuwa chawa .
 
Uchawa nitatizo kama ushoga... Tusiwazingatie kitaifa ila tuwasaidie wasimame kama wanaume maana wengi jinsia ni me LAKINI wanajibebisha kwa wenye vihela
 
Back
Top Bottom