Ni kweli Tff imeshindwa kudili na Imani za Kishirikina Michezoni.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Hapa nazungumzia mpira wa miguu, siku hadi siku Imani za kishirikina zinazidi kushika kasi kwenye michezo mbalimbali ya ligi kuu ya NBC, Kwa sisi wapenzi wa mpira hatuvutiwi na matukio hayo yanapunguza utamu wa ligi yetu pamoja na ubora wa timu zetu.

Zamani matukio haya yalikua yakifanywa kwa kificho kwa zile walizokuwa wanaziita kamati za Ufundi za timu ila siku hizi matukio haya yapo wazi wazi kabisa.

Rejea tukio la mchezo wa Tabora Utd Vs Simba, wanaosadikika kuwa mashabiki wa Simba wanaonekana wakimwaga vitu uwanjani tena mchana kweupe kabisa sasa unajiuliza nani aliwaruhusu kwenda kwenye eneo la kuchezea na kufanya yale madudu?

Hapa ndio unafahamu mpira wa Tz unachezwa sana nje ya uwanja sio ajabu meneja wa uwanja wa Tabora ni mwanasimba hivyo hakuona shaka kuwaruhusu kufanya ule Ujinga.

Kuna mchezo ulifanyika Kilimanjaro Gadiel Michael alionekana naye akiwanga mchana kweupe kwa kumwaga dawa za kishirikina kiwanjani.

Kuna gemu za klabu Bingwa kama sikosei ni Simba vs Al Ahly Simba walifanya uchawi wa mapaka kweupe mpira ukiwa unaendelea.

Kubwa kuliko ni ile gemu Afrika Kusini ambayo wachezaji wa Simba walikoka moto kabisa kiwanjani kwa Imani za kishirikina lakini bado walipigwa kitofali, Hakika matukio ni mengi mnoo.

Swali la kujiuliza Je Tff wameshindwa kuja na Muarobaini kabisa wa haya mambo, kwanini wasitengeneze sheria kali kudhibiti haya matukio ya kishirikina viwanjani.

Bila kusahau uchawi wa vitaulo uzuri kwa hili Yanga wamekuja na Antidote yake sio ajabu kuona baada ya vitaulo vyao kutolewa Yanga inafunga japo mimi sio muumini wa Ndumba.
 
Na hii ndo inayofanya wachezaji wa ndani wasifike mbali, vijana wanavipaji ila jinsi wanavyopotea kwenye game utawaonea huruma kwa kuendekeza ushirikina yani kutumia uchawi ni sawa na kuingia na nondo kwenye mtihani huwezi kufanya maandalizi mazuri
Mbona mbele wachezaji unaona kabisa wanacheza kwenye mifumo anachofanyia zoezi anakionesha ndani ya pitch

Sent from my motorola one macro using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom