Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 1,448
- 1,003
KIGOMA WAMPA MAPOKEZI YA KIHISTORIA RAIS SAMIA SULUHU, ANATAJWA KUWA NDIO KIONGOZI ALIYEVUTA WATU WENGI ZAIDI LAKE TANGANYIKA
Wananchi wa mkoa wa Kigoma wampa mapokezi makubwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan uwanja wa CCM Lake Tangayika.
Mapenzi haya makubwa kwa Rais Samia yanahusishwa na jitihada zake kupitia serikali anayoiongoza ya kuifanya mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha biashara ukanda wa Magharibi.
Serikali ya awamu ya sita anayoiongoza Rais Samia inakamilisha ujenzi wa barabara za lami zinazouunganisha mkoa wa Kigoma na mikoa ya Tabora, Kagera na Katavi.
Inatekeleza pia miradi ya ujenzi wa meli kubwa mbili kwa ajili ya abiria na mizigo, inakamilisha ujenzi wa bandari ya Ujiji na Kibirizi, inakamilisha ukarabati wa meli ya kubeba mafuta ya MT Sangara, imeuunganisha mkoa huo na umeme wa Gridi ya Taifa pamoja na uimarishaji mkubwa wa hospitali ya rufaa ya mkoa huo Maweni.
Naye Mzee Ali Msaze wa Buzebazeba anasema tangu awe na akili za kujitambua hujawahi kuona watu wengi Kama hawa," Huyu mama ni mpango wa Mungu "
Hakika wanakigoma #Tunaridhika #HakunaKilichosimama #KaziIendelee