Ujenzi wa daraja la Kigamboni sasa kuanza mwakani

Raia Mwema

JF-Expert Member
Jun 30, 2008
535
79
Hatimaye ujenzi wa daraja la Kigamboni lililokuwa likisubiriwa na wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam, unatarajia kuanza mapema mwakani.
Daraja hilo linatarajia kujengwa eneo la Kurasini ambapo litaunganisha mji wa Kigamboni na sehemu zingine za jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza katika maonyesho ya wiki Mashirika ya Hifadhi za Jamii, yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Ofisa Mkuu wa miradi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), John Ndazi, alisema tenda zilizotangazwa kwa ajili ya kupata kampuni itakayojenga daraja hilo zitafunguliwa mwezi ujao.
Ndazi alisema baada ya kupata kampuni moja, kazi ya ujenzi itaanza mapema mwaka ujao ambao utagharimu dola za Marekani milioni 130. Alisema serikali itatoa asilimia 40 ya fedha hizo na NSSF itatoa asilimia 60 na kwamba baada ya ujenzi wake kukamilika, magari yatakayokuwa yanapita katika daraja hilo yatakuwa yanalipia.
“Magari yote yatakuwa yanalipia wakati yanapita katika daraja hilo kwa kipindi cha miaka 25 na baada ya hapo daraja litakuwa mali ya serikali,” alisema. Daraja hilo ni miongoni mwa miradi mikubwa ya NSSF ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na wananchi wengi lakini kwa bahati mbaya uanzishwaji wake umekuwa kitendawili.
Aidha, NSSF imesema inatarajia kujenga nyumba 18,000 za bei nafuu ambazo itaziuza kwa wanachama wake.
Maonyesho hayo ya wiki ya mifuko ya hifadhi yalifunguliwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali.
 
Politics zikizidi hata mambo yenye ukweli yanaonekana ni uwongo. Binafsi siamini bila kuona kwa macho yangu mambo yanaanza.
 
yani after a decade of longolongo....! je hizo flyovers si zitajengwa baada ya yesu kurudi...!
 
Nje ya muda coz ile project ilikuwa ianze mwaka huu 2011 bt sidhan hata mwakani kama litajengwa hilo daraja!
 
Yetu macho, hili daraja limekuwa kwenye midomo ya viongozi wa Tanzania kwa miaka mingi, lakini hakuna kitu kimeonekana mpaka sasa.
 
Ah tumeshawazoea hao,vya uongo kwao ni 80% na vya ukweli 20%.Nasikia ktk kampeni za 2010 waliahidi Meli kubwa Morogoro,sasa sijui itakua pale MINDU....Tehe...tehee...teheee....!
 
daraja likijengwa Kurasini,kama awakupanua barabara ile ya pale BP ni kazi Bure.
 
Kekundu kekundu alitokea rais m1 akawaidi wananchi wake atawajengea madraja na kuwaletea meli na machinga complex kumbe ni kekundukekunduuuuu
 
Politics, kwa nini watangaze kweny manyesho, au ni kwasababu wangekosa cha kusema? Mpaka waanze ndo nitaamini. vinginevyo ni uhuni tu/
 
Miaka yote ina namba zake......2011,2012, 2013.......... hakuna mwaka unaitwa "Mwakani" maana huo hauatafika. Lakini vipi kuhusu Mabasi yaendayo kasi? Mbona kimya?
 
longo longo tupu, halafu wanchofanya ni ujinga wa mwisho, hivi na hizo gari zitapita kwenye ile barabara ya BP? Au wanataka kuongeza msongamano wa magari?
Kwanini hiyo pesa isitumike kuleta vivuko vipya na vya kisasa kabisa au hiyo pesa ipelelekwe kwenye miradi ya umeme itasaidia.
 
regime change haiwezi kufanya haya mambo kwa usiku mmoja lakini inaweza kupunguza hii mida yao kwa zaidi ya asilimia 95%, kwa hiyo pale waliposema miaka 10 yaweza kuwa miezi sita!
yani after a decade of longolongo....! je hizo flyovers si zitajengwa baada ya yesu kurudi...!
 
Kwani Mbowe alisharudisha zile fedha za NSSF, yeye ndiye anaechelewesha huu ujenzi kachota mamillioni ya mkopo hataki kuyarudisha, au ilikuwa ni mabillioni?
 
Kila mwaka huwa linaanza kujengwa mwakani kwa hiyo hata wakianza kulijenga mwakani ya mwakani ni sawa tu.
 
serikali hii magirini kweli,fix kibao je mnakumbuka mradi wa mji wa kisasa pale kibamba uko wapi?
 
nasikia kizunguzungu bin kichefuchefu! watu kulipia kuvuka daraja ndani ya nchi yao? kwani hilo daraja ni ferry? linatumia mafuta kiasi gani? kwa hiyo mtu anaekaa kigamboni na shughuli zake zipo kariakoo akiwa na gari lake itabidi agharamie mafuta kwa ajili ya gari lake na pia itabidi alipie
kuvuka daraja, na yule anaekaa ubungo na shughuli zake zipo kariakoo akiwa na gari lake atagharamia mafuta kwa gari lake tu! sasa hapo usawa uko wapi? kosa ni kukaa kigamboni? mbona daraja la mtambaswala linalounganisha TZ na Msumbiji watu hawalipii kuvuka? madaraja is just part ya miundombinu ya barabara kuna nini cha ajabu? daladala zipitazo njia hiyo nazo zitaongeza nauli kufidia gharama hizo! kulipia kuvuka daraja kwa miaka 25 ni aibu! madaraja mangapi magari yanapita bila kulipia iwe la kigamboni tu! au kwa kuwa linavuka bahari? vipi kuhusu madaraja yanayovuka mito n.k mbona hayalipiwi!?
 
Kwani Mbowe alisharudisha zile fedha za NSSF, yeye ndiye anaechelewesha huu ujenzi kachota mamillioni ya mkopo hataki kuyarudisha, au ilikuwa ni mabillioni?
Mabilion wanapewa hata kina mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangwala au vipi mbona humsemi huyo?????????
 
Back
Top Bottom