Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,240
- 12,762
Katika historia ya Tanzania kuna mtu aliyeitwa Kisabengo. Kisabengo alikuwa ni mtumwa wakati ambapo Sultani wa Zanzibar anatawala Zanzibar na pwani ya Afrika mashariki. Alikuwa ni mtu mwenye nguvu sana. Baada ya muda akatoroka atumwa akiwa na watumwa wengine akiwa kiongozi wao.
Baada ya kutoroka akaanza kuwa mbabe wa kivita, akivamia na kupora maeneo ambayo leo ni mikoa ya Pwani na Morogoro. Kokote lilikosikika jina Kisabengo watu waliingiwa na hofu kuu. Baadaye akaanzisha mji. Aliuita mji huo Simbamwenni/Simbamwene. Mji aliojenga leo ndiyo Moro Town. Ulikuwa mji wa maana sana. Ulikuwa na Kuta za mawe. Minara miine ya ulinzi iliyojengwa kwa mawe na ulilindwa na maaskari wenye magobole. ulijengwa kando ya mto na ulikuwa na milango minne ya mpingo kila pande, milango yake ilipambwa vizuri sana. Mji ulikuwa moja ya vituo muhimu ya misafara kutoka bagamoyo kwenda Ujiji kituo.
Huyu Kisabengo alikuwa na binti yake ambaye alimwita Simbamweni. Alimpenda sana binti yake. Hata alipokufa alimuachia usultani wa mji ule. Kipindi H. M Stanley anapita kwenda unyanyembe aliweka kambi Simbamwene. Alistaajabu uzuri wa mji ule uliokuwa ukiongozwa na mwanamke. Askari wakakamavu wenye silaha wakimtii.
Stori hii inaonyesha jinsi Waafrika hatukua na habari za ubaguzi wa kinjinsia wala kuwadharau wanawake. Ushahidi mwingine ni lugha. Lugha yetu haina habari za She/He/Her/Him. Haibagui jinsia.
Ushahidi mwingine ni uwepo wa Matrineal Societies. Huko mikoa ya kusini urithi ulikuwa unapita kwa mwanamke, hata jamii nyingine kama wanyakyusa utakuta ni semi -matrineal. Na hii habari ya matrineal ipo sehemu nyingi africa.
Sasa zikaja dini za kutoka Mashariki ya kati na utamaduni wa watu wa eneo hilo kudogosha na kudharau mwanamke. Wakatulisha maneno kibao kibao na kutufanya hata sisi tuanze kufikiri kama wao. Hizi dini za middle east ndiyo zimefanya muafrica aanze kudharau mwanamke.