Uhusiano wa Leo yako na kesho

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Utangulizi
Watu wengi tumekuwa na tabia ya kuangalia Leo yetu kuliko kesho yetu, umeshawai kujiuliza ni kijana msomi tena mzuri kapewa ofisi ya serikali au ya binafsi anafika ofisini badala ya kuzalisha Mali za ofisi yake anakuwa ni mmoja ambaye anachangia ofisi kufirisika au kufungwa

Unamkuta mbaba wa watu ana mke mzuri wa sura na umbo lakini Mzee wa watu anamwacha mke wake na kujiushisha na mahusiano na wanawake wengine na wakati mwingine na watoto washule au wafanyakazi za ndani ?

Unamkuta dereva mzuri Sana wa mitambo amepewa mitambo kuendesha badala ya kutunza mitambo anakuwa sehemu ya kuhujumu mitambo na mwishoe inakufaa

Ni baadhi Tu ya matukio ambayo tunakutana nayo kwenye jamii ya kwetu, Biblia inasema pasipo maono watu huacha kujizuia.

Kwanini lakini Mambo kama haya yanatokea kila siku ya Maisha ya wanadamu.

Sababu ya Kwanza

Maono
Watu wengi wanaotenda wanayoyatenda kwa sababu hawana maono, maono ni picha ya Kesho Yako , ni vile unavyoiona kesho yako ukiwa Leo.

Mithali 29:18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia;
Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

Maono yanakupa kujua kesho yako jinsi itakavyokuwa hata kama Leo yako ni nzuri au ni Mbaya kiasi gani?

Umeshajiuliza uko kwenye eneo la ofisi za umma au binafsi lakini Kwa sababu umepewa nafasi unawadharau watu wengine na haujui kesho yako hao unawadharau watakuwa wakina Nani?

Umeshawai kujiuliza, unatembea na house girl wako au ps wako ulishawai kujiuliza na kutafakari ndugu zako wakijua? Ulishawai kuwaza hizo taarifa zikifika mitaani au ofisini kwako ? Je ulishawai kuwaza jinsi heshima yako ulivyoijenga kwa miaka mingapi unataka kuharibu Kwa tukio la usiku mmoja? Je mke wako je? Maamuzi ambayo atayachukua juu yako? Watoto wako watakuchukuliaje?

Kama hakuna maono hakuna Sheria?

Kazi ya Sheria kwenye maono ni kulinda maono, ukiwa na maono ya kuwa Baba au mama wa mfano utahakikisha unajiwekea Sheria ambazo zitahakikisha kwamba hauta haribu sifa yako ya Baba Bora?

Maono yanalinda kesho yako

Watu wengi Kwa sababu ya njaa au shida wanayasariti maono Yao? Ulishawai kujiuliza kwanini mwanafunzi anakubali kutoa mwili wake Kwa ajili ya mwalimu Kwa ajili ya matokeo? Ujue huyo mwanafunzi hajui kesho yake ? Kama angekuwa anajua sidhani kama alifikira kesho yake juu ya watoto wake ? Usalama wa Maisha yake ?


Yesu wakati anatesa msalabani maandiko yanasema alitazama ushindi ambao ataupata baada ya msalaba , yaani wakati wamateso yeye aliona namna gani atakapopewa heshima duniani na mbinguni ambayo hakuna ambaye atakuwa naye hisopokuwa yeye ndio maana hakukata Tamaa

1 Petro 2:22-23Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.

Ukiona shetani anapiga vita Maisha yako ujue ameiona kesho yako iliyobora amehamua kukuwai ili kuhakikisha kwamba haufiki kesho yako?

Ushawai kujiuliza ni binti mdogo Tu mrembo anajiingiza kwenye mahusiano na kupiga picha za ajabu? Unajiuliza anajua kesho yake kweli? Anajua ni namna gani picha hizo zinaweza kuharibu kesho yake Kwa sababu Tu ya furaha ya kitambo

Unamkumbuka Yusufu , Yusufu alipokutana na Yule mama mke wa Bosi wake licha ya ahadi ya malupulupu na vinono ambavyo mke wa Bosi wake alimrubuni lakini Yusufu akikubali? Leo ni vijana wangapi wako tayari kukataa fedha kutoka kwenye wamama wenye fedha Zao ili Tu wawafurahishe?

Unamkuta kijana ana umri wa 20's ana mahusiano na mama ambaye umri ni Sawa na mama yako? Unajua kesho yako wewe kijana? Unajua uthamani wa Maisha yako ? Unajua Mungu alivyopanga kesho yako ilivyokuwa njema ? Unaupoteza ujana wako kwa furaha ya Leo na siku utakapo tafuta afya yako ili Mungu akupeleke viwango ndio utatambua umuhimu wa kutunza ujana wako
 
Kesho Yako imetunzwa na kufichwa ndani ya Leo yako , usijesema najutia maamuzi yangu nikiwa kijana kwamba labda ningefanya hivi na vile nisingekuwa hapa
 
“Nayajua mawazo ninayo wawazia asema bwana, ni mawazo ya amani kuwapa ninyi tumaini siku zenu zote”

Barikiwa mwalimu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom