Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 286
- 582
UTANGULIZI
Maandiko matakatifu yanasema mwili wa mwanadamu hauwezi kumpendeza Mungu, maana mwili hauokoki na hauna ajenda za kwenda mbinguni ndio maana waufuatao mwili wamefarakana na Mungu
Njia za Kuushinda Mwili
Mithali 29:18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
Njia ya Kwanza
Kuwa Mtu Mwenye maono,maono ni picha ya ndani ambayo Mtu anakuwa nayo juu ya kesho yake
Sifa za maono
Maono yanasifa zifuatazo :-
Maono yanatengeza Sheria, Sheria ni taratibu ambazo zinaweka Kwa lengo la kutengeneza aina flani ya Maisha ambayo mtunga Sheria anataka
Maono yoyote lazima kulindwa na Sheria, ili yawe maono Kwa sababu pasipo Sheria watu uhacha kujizuia maana yake watu wanakwenda pasipo utaratibu
Sheria ya mwili
Ili uweze kuhushinda mwili lazima uwe na Sheria ambayo itasimama Kwa lengo la kulinda maono yako ya kutokumtenda Mungu dhambi
Sheria ambayo unatakiwa kuwa nayo moyoni mwako Kwanza weka Sheria ya kutokumtenda Mungu dhambi kupitia mwili wako
Ukiwa na Sheria ndani ya Moyo wako kutakapo tokea kishawishi cha kukushawishi kumtenda Mungu dhambi kwakupitia mwili wako utajikuta ndani yako unabanwa na hiyo Sheria
Wakati Yusufu anabembelezwa na mke wa potifa alale naye Yusufu alikumbuka ile Sheria ambayo aliweka moyoni mwake ya kutokumtenda Mungu dhambi , na hiyo Sheria ikamkumbusha Moyo wake Akamwambia Yule mama kwamba hawezi kumtenda Mungu dhambi Kwa kulala naye
Sheria ya pil
Weka Sheria ya kutokumkosea mwenzi wako, Biblia inasema hauwezi kumpenda Mungu kama haumpendi jirani yako, Kwa hiyo ili upendo wako kwa Mungu uonekana Kwanza lazima kumpenda jirani yako Kwanza
Unapokutana na jaribu la kumtenda Mungu dhambi Kwanza mkumbuka mkeo au mumeo na ufikiria kwamba mke/Mume wako kapewa taarifa kwamba umemsaliti
Weka picha Kwa mkeo ataskiaje kwamba umemsaliti ? Fikiria Kwa habari za mashemeji , mawifi na wakwe zako wakiskia tabia yako Kwa mkeo utajiskiaje? Watoto wako je ,? Au wazazi wako ,? Watajiskiaje kwamba kijana wao amekwenda kuwaaibisha?
Sheria ya Tatu
Kataa Imani potofu, kuna Imani ambazo ni Imani potofu kuna watu wanaamini kwamba mwanaume hawezi kuwa na mke mmoja ,we jisemehe moyoni kwamba Mimi sitakuwa kundi la hao Ambao hawawezi kuwa na mke mmoja
Maandiko matakatifu yanasema Imani huja Kwa kusikia, ukiamini kwamba mwanaume hawezi kuwa na mke mmoja utajikuta umehanguka kwenye Hilo kundi la wanaume wenye michepuko
Unapoweka Imani moyoni mwako Mungu anakutengenezea mazingira ya kukutenga na watu, utakuwa katika mazingira ambayo yatakubana uingie kwenye michepuko utashangaa Mungu anakutetea
Ulishawai kwenda Katika maeneo ambayo uko mbali na familia na hakuna ambaye anakuona na uko na wenzako wanakushawishi Kwa kila njia na michepuko ghafla unaskia mmoja wao anakwambia mwacheni huyo ni mlokole? Ujue Mungu anaingilia Kati kwenye majaribu ambayo yangekuangusha Ila Mungu anakutetea ? Mungu ni mwaminifu Sana weka Imani kwake
MBINU 2
Mathayo 26:41Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Omba msaada wa Mungu kukusaidia kushinda tamaa za mwili, maandiko matakatifu yanasema hatuwezi Kuushinda Mwili Kwa Sheria pekee yake tunaitaji msaada wa Mungu
Yesu wakati anaelekea msalabani akimwomba Mungu msaada Kwa sababu mwili ukikataa kwenda msalabani Akamwambia Mungu Roho I radhi Ila mwili ni dhaifu
Unapokutana na vita vya mwili mwambie Mungu kwamba umefika mahali unaona kabsa tamaa za mwili zinaelekea kukushinda omba msaada wa Mungu kwa sala hii mwili ni dhaifu Ila roho I radhi Mungu akushindie vita vya mwili
MBINU 3
2 Timotheo 2:22 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Kukimbia Tamaa za Mwili
Hepuka watu , makundi au mazungumzo mabaya, maandiko matakatifu yanasema mazungomzo mabaya uharibu tabia njema, chumba hunoa Chuma ndivyo MTU anoavyo uso wa rafiki yake
1 Wakorintho 15:33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.