Uhusiano wa ccm na wananchi ni wa kuku wa kienyeji na mfugaji

wagagagigikoko

Senior Member
Dec 5, 2010
163
49
uhusiano wa CCM na WANANCHI ni sawa na ule wa mfuga kuku wa kienyeji na kuku wake, Mfugaji ukiona anawapa pumba au nafaka kuku wake basi ujue kuna mgeni anakuja na kuku anaandaliwa kuchinjwa.

ukiona CCM iko karibu na wananchi basi ujue UCHAGUZI uko mlangoni.. hapo utawaona wanaojidai makada wa CCM wakiwatembelea wananchi na fulana, kofia chumvi na kanga kuonesha mapenzi yao kwa wananchi. lakini baada ya uchaguzi imekula kwako huwaoni tena mpka baada ya miaka mitano.

Lakini sasa wananchi wamegundua janja ya Chama cha Mafisadi (CCM) vitu vyao wakileta vinapokelewa lakini kura ng"ooooooooooooo hatuwapi maana hivyo wanavyohonga wametuibia wenyewe, ni vyetu.

hatukubali tena kuwa kuku wa kienyeji wa kufrahia tshirt na kofia halafu baadaye tunajutia, SEMA NO KWA CCM...UKOMBOZI KAMILI 2015
 
Si ndo maana mpka leo wanapata kura vijijini ambako sio wasomi. Mjini hawatapata watu tena... Watapata kuku wa kienyeji wa vijijini
 
Back
Top Bottom