Ni nani muasisi wa huu udhalilishaji wa Wahitimu wa Vyuo Vikuu (Graduates) unaoendelea? Hiki kidonda tukikilea kitaleta shida mbeleni

Tausi Rehani

Member
Aug 29, 2020
20
40
Wasaalam,

Hivi karibuni humu kumekuwa na ongezeko kubwa la nyuzi(threads) zenye mlengo wa kuwadhalilisha wahitimu wa vyuo vikuu (graduates) na wanafunzi waliopo vyuoni kwamba ni useless na hawana uwezo wa kujitegemea kabisa.

Kwa utafiti nilioufanya, hii kampeni inaendeshwa kwa asilimia kubwa na watu ambao hawakubahatika kabisa kufika ngazi ya chuo kikuu ( Yaan Form Four Failures) na baadhi yao Ni walifika ngazi ya chuo kikuu lakini walitoka patupu. Maana siku zote asiyesoma ndo anayemsema aliyesoma. Huwezi mkuta aliyesoma anamsema asiyesoma.

Nadhani wahusika wa hii kampeni iwe kwa makusudi au bahati mbaya wanasahau kuwa lengo kubwa la elimu ni kutoa ujinga na kujaza maarifa ambayo yatamsaidia mlengwa kuendesha maisha ya kila siku.

Level ya chuo kikuu Ni tofauti na level za chini ambako unajiendea kama garii bovu. Ukishafika chuo kuna specialisation mfano mtu anaspecialize kwenye Mining Engineering, Pharmaceutical sciences au IT.

Na Lengo la Elimu hiyo Ni kumpa mtu maarifa ya kama Ni pharmacy akigraduate ajue jinsi ya kutumia hiyo pharmaceutical science aliyosomea kujikwamua kimaisha iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri na Si vinginevyo.

Unaposema unataka kuona wahitimu wanaendesha bodaboda au wanakaanga chipsi unaondoa lile lengo la specialisation aliyoipata chuoni. Hapa unalazimisha tuwe na taifa la ovyo lisilo na wataalamu miaka kadhaa ijayo.

Kutangatanga kama kuku wa kienyeji ni Kwa aliyekosa hiyo specialization mostly wenye ajenda hii ovu , kama hukusoma mpaka kuspecialize kwenye kitu kimoja basi endelea kutanga usilazimishe kila mtu atange mtaani. It does not make sense kumlazimisha mtu awe muuza matunda au boda Kwa kigezo cha kujiajiri.

Ukiona kobe ameinama ujue anatunga sheria.Graduates hawataki kufanya hizo Kazi zenu za rat race maana zinaingilika kirahisi kwasababu Hakuna kigezo chochote kinachohitajika kufanya hizo Kazi mnazolazimisha watu wajiajiri.

Mfano, leo hii nikiamka asubuhi Nataka niwe Boda ntakutana na kizuizi kipi? It's just a wake up and do job , na mmejazana kama fungu za nyanya.

Kila mtu asimame na taaluma yake. Kama hauna taaluma endelea kuranda kama ng'ombe aliyepotea mnadani.

Nawasilisha.
 
Muilaumu serikali ya ccm ndio imeamua kuwabania msitoboe sio sisi ni jambo la kushangaza miaka zaidi ya 10 umekuwa darasani lakini ukirudi mtaani unakuwa boda mmeshasahau enzi hizo ajira bwerere wasomi walivyokuwa wanavimba mtaani kukosoa wasioenda shule utasikia alimbia umande huyu
Ni kweli serikali ina mchango mkubwa katika janga hili.

Lakini mkuu suluhisho sio kuendeleza kuwananga vijana. Hii ndiyo inapelekea sasa matatizo ya afya ya akili yanakuwa mengi katika jamii.

Vijana wanapambana na sonona kutokana na kuandamwa kila sehemu huku kiini cha tatizo ambacho ni serikali inasahaulika.
 
Hahahaha Guerilla wars zitaibuka Mda sio mrefu. Watu wanaendelea kujazana mtaani hamna Kazi. Ni kushika mtutu
Ni suala la muda serikali si vipofu na wanadharau machalii na wazidi kujazana tu mtaani hata hizo boda boda na saidia fundi itafika muda watakuwa wengi kuliko kazi zenyewe moto utaanza kuwaka.

Wanasahau kuwa njaa haivumiliki.
 
Ila kuna kaukweli, graduate anamuomba pesa ya kula darasa la saba kweli!!! Ndio maana huyo darasa la saba anashangaa na kutoa hayo maneno. Ni kwa nini asitumie hiyo elimu yake ya juu kupata pesa?
 
Ila kuna kaukweli, graduate anamuomba pesa ya kula darasa la saba kweli!!! Ndio maana huyo darasa la saba anashangaa na kutoa hayo maneno. Ni kwa nini asitumie hiyo elimu yake ya juu kupata pesa?
Mkuu, wanavyuo wengi huandaliwa kukabiliana na mazingira ambayo kiuhalisia hayapo , ni mazingira ya kufikirika . Wakija kwenye mazingira halisia sasa inakuwa mtiti.

Mazingira halisia yanahitaji uzoefu sio elimu ya nadharia, Ni vigumu kutoboa, Huyo darasa la Saba tayari ana uzoefu elimu yake kaipata kupitia experience. Changamoto alizokuwa anakutana nazo ndo amezigeuza fursa kwake.

Kwa huyu wa chuo Ni suala la Mda naye atapata uzoefu then atayamudu mazingiria , so tuwape muda sio kuwasema vibaya. Hata waliofanikiwa mtaani hawakufanikiwa moja Kwa moja.
 
Back
Top Bottom