Uhusiano Na Hizbu-ccm Vs Cuf Nani Mkweli?

taratibu mkuu bi kirembwe shamuna tunakujua mpaka kwao Eneani Donge na ndugu zake wengi wako kama vile sasa wote watoto wa Othman Shariff?

mtake radhi mheshimiwa ana mapungufu yake mengi lakini msimjazie na yasio yake.
 
Mkuu na mimi namjua na ndugu zake na watoto wake na jamaa zake wengine, lakini kuwa kwao ni Donge Eneani karibu na Kipange najua wana mji wao pale na kaka yake Mzee Khatibu anaishi pale lakini hiyo haifuti hoja kuwa ni mtoto wa nje na hilo si kosa lake - mimi nimesema nimesikia tu na kutoa ushahidi wa wazee wanaosema kweli kafanana na huyo jamaa(unajua haramu haijifichi).

Mkuu na wewe ulizia hii habari mimi sio kuwa nimiamini bila ya kutia shaka na wewe kuikana kwako una hakika?
 
bi kirembwe sasa mbona kuna ndugu zake wamefanana mpaka rangi, jee wote ni wa mzee othman sharrif?

halafu mzee othman sharrif mtu wa wapi?

nimekukubali kuwa mkuu utakuwa unamjua maana ulivyoyataja maelezo nimekuamini mkuu.

unajua mie niliwahi kusikia ila nnajua zanzibar ukiwa watu hawakupendi huachi kuzuliwa maana nimesikia Rais Karume si mtoto wa Karume mkubwa na Waziri wetu Kiongozi sie baba yake huyo alienasibishwa nae na tena hii niliisikia kwa wamakunduchi wenyewe nikapigwa na butwaa

mwisho nikaona kwa umbea tumezidi
 
Mkuu ni kweli ndugu zake wamefanana lakini wote hawakuambiwa haya iwe Bwana Ali tu au kwa sababu ni "public figure" inawezekana anasingiziwa kwani kama ulivyosema Zanzibar umbea mwingi

Kuhusu Othman Shariff(hana uhusiano na Seif Sharrif) huyu ni Mpemba na alikuwa ni ASP damu alikuwa na ndugu yake anaitwa Ali Shariff kama uliwahi kusikia ASP wakati wa uchaguzi wa 63 walipata kiti Pemba basi kilitoka kwa huyu Ali Shariff alipounganisha nguvu zake na ASP kutoka ZPPP.

Kwa hivyo hiyo ya Shamhuna mimi naiwekea alama ya ? na wewe Mkuu msimamo ni wa kwako - sote tumo katika kutafuta usahihi.
 
mhhh una visa utafikiri mzee wa miaka 100.
 
Sasa kama wote wana uhusiano na HIZBU NCHI TUMPE NANI SASA?

Hizi hoja za kuhusisha chama fulani na Hizbu and then somehow that becomes a scandal is pure racism.Watu wa Zanzibar ndio watakaopiga kura kuamua nani aongoze Zanzibar na kuelekea wapi.Mushi wewe kama mtanzania kura yako ni moja na hakuna kitu kama "sisi" katika upigaji kura kwa sababu viongozi Tanzania hawachaguliwi kwa mtindo wa caucus.
 
Ninaposema sisi ninamaanisha sisi wananchi wa TANZANIA!
Na wananchi licha ya kwamba kila mtu anaenda kivyake kwenye kupiga kura...Kimawazo wako pamoja..Ama pia inawezekana wasiwe pamoja kutegemea na Party afilliations zao ama neutrality which is the same as independent! Hivyo mimi kusema sisi" sikumaanisha nikiwa napiga kura,bali "sisi" kama tulioko oraganized kupiga kura kwa malengo baada ya kupata sera na kukubaliana nazo!
Na kama unadai hii hoja ya Hizbu ni pure racism..Then waulize CUF ni kwanini wao wanasema CCM ndio wana uhusiano na HIZBU..Pia vile vile waulize CCM kwanini wao wanasema ni CUF ndio wenye uhusiano na HIZBU!
Sasa kunikomalia mimi unakosea!
 
Hapa tunachotakiwa ni kuendelea na mjadala wenye nia ya kusonga mbele!
 
Ninaposema sisi ninamaanisha sisi wananchi wa TANZANIA!
Na wananchi licha ya kwamba kila mtu anaenda kivyake kwenye kupiga kura...Kimawazo wako pamoja..Ama pia inawezekana wasiwe pamoja kutegemea na Party afilliations zao ama neutrality which is the same as independent! Hivyo mimi kusema sisi" sikumaanisha nikiwa napiga kura,bali "sisi" kama tulioko oraganized kupiga kura kwa malengo baada ya kupata sera na kukubaliana nazo!
Na kama unadai hii hoja ya Hizbu ni pure racism..Then waulize CUF ni kwanini wao wanasema CCM ndio wana uhusiano na HIZBU..Pia vile vile waulize CCM kwanini wao wanasema ni CUF ndio wenye uhusiano na HIZBU!
Sasa kunikomalia mimi unakosea!

Hii ya racism sikuwa "nakukomalia" wewe Mushi,ila nilikuwa nawakumbusha wanasiasa wanaoona kuwa ni scandal kuhusiana na viongozi wa chama kilichokuwa cha sultan which is perceived to be chama cha waarabu ni racism. Siku zote huwa nasema kuwa sio sahihi kwa Tanzania kuwa mstari wa mbele kupinga apartheid Afrika kusini na kwingineko Afrika huku Zanzibar apartheid inakumbatiwa kama ushujaa.
 
Ni kweli usemayo lakini hii issue ya uhusiano na HIZBU ndiyo imekuwa ikiwasaidia CCM mara zote pale wanapojitetea dhidi ya CUF kwa bwana wakubwa!
 
Na sasa CUF wanapinga hilo na kusema kama ni uhusiano si hata CCM wanao?
 
Mjadala naona uendelee lakini mwishowe tunataka hiyo hoja ya UHUSIANO isije kuwa sababu ya namna ya kutatua mgogoro wa Zanzibar!
 
So far inaonekana ni wote ccm na cuf wana uhusiano ama waliwahi kuwa na uhusiano na hizbu..So cha msingi hapo ni vyama vyote kukubaliana kwa pamoja kuwa hilo lisiwe issue tena ya kumkandamiza mwingine wakati wa mjadala wa namna ya kumove forward huko visiwani!
Wapigiane saini kuwa hii issue iwekwe kando!
La sivyo ubaguzi utaendelea kuneemeka!
 
Ama kama kuna chama chenye nia mbaya then watu waweke wazi hapa na tujadili!
 
Kibunango ni lazima mkae chini mkubaliane kuidropu hii issue la sivyo itaongeza uchochezi tuu!
Sasa wewe una vithibitisho kuwa ccm hawana uhusiano na hizbu?
 
Si unaona hii habari Kibunango?
Especially pale nilipo highlight?

Sakata la mwafaka Zanzibar

2008-05-18 11:44:05
Na Simon Mhina

Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kukitaka chama hicho kurejea kwenye meza ya mazungumzo na CCM, wanaichukulia kama porojo, vinginevyo ayatoe kimaandishi.

Kadhalika, Chama hicho kimesisitiza kuwa hakitakubali kamwe kukaa meza moja tena na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba kuzungumzia Mwafaka.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni Bw. Hamad Rashid Mohamed, alisema habari za Rais kuwaomba CUF warejee kwenye mazungumzo wamezisikia kwenye Redio na magazeti, hivyo hawajazitilia maanani.

Alisema hivi sasa CUF imeshachoka `kutapeliwa` kisiasa na CCM hivyo hawakubali maneno yoyote yasipopelekwa kwao kwa maandishi.

Alisema akiwa Mkuu wa Nchi, inashangaza kuona anatoa maagizo mazito yanayogusa ustawi wa Taifa, kupitia mlango wa nyuma.

Alisema Rais alikuwa na uwezo wa kuwasiliana nao moja kwa moja, badala ya kutoa maagizo hayo wakati anazungumza na Waziri anayeshughulikia mambo ya kimataifa wa Serikali ya Ufaransa aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

``Anavyosema CUF na CCM tukutane, wakati anazungumza na mfaransa huyo, alikuwa anamtuma aje atuambie au vipi?``alihoji.

Bw. Mohamed alisema kwa kiasi kikubwa CUF wanamheshimu mno Rais Kikwete na hawakusudii kupuuza wala kudharau mawazo yake.

Alisema ni kweli Rais akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu, anao wajibu wa kuhangaika ili kuhakikisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakuwa ya amani.

``Tunamheshimu Rais Kikwete, lakini anapotoa maagizo makubwa kama hayo katika vyombo vya habari, kwa kweli tunabaki tunashangaa, maana hata majibu tunashindwa kutoa,``alisema.

Alisema angalau wakishapata waraka wa maandishi kutoka kwa Rais Kikwete wanaweza kujibu.

Hata hivyo, Bw. Mohamed alisisitiza kwamba mazungumzo hayo katika kiwango cha Makatibu wakuu, yameshapita.

Alisema Makatibu wakuu, wa CUF na CCM wamekaa mezani na kuchukua muda mrefu wa miezi 14, hivyo kikao chao hakiwezi tena kuwa na jipya.

Alisema japokuwa wakipata taarifa ya maandishi kutoka kwa Rais wataijadili, lakini ni wazi kwamba CUF haitakubali tena mazungumzo ya makatibu wakuu wa vyama hivyo.

``Iwapo atatuandikia, barua yake tutaitafakari vema, iwapo tu itataja watu wengine wakukutana na kuzungumza lakini si Seif na Makamba,``alisema Bw. Mohamed.

Alisema CUF kinaamini kwamba maelekezo atakayoyatoa Rais sasa ni Bw. Seif kukutana na Rais Karume.

Kuhusu madai ya CUF kuhusika na wananchi wa Pemba wanaotaka kisiwa hicho kijitenge, Bw. Mohamed alisema wananchi wote wana haki ya kutoa maoni yao.

Alisema eneo la Pemba pia kuna wanachama wa vyama vingine, kwa hiyo anaamini kati ya wananchi hao waliopeleka barua Umoja wa Mataifa kutoa madai hayo, wamo pia wanachama wa CCM.

Hata hivyo, kiongozi huyo alimshangaa Kada wa CCM Bw. Hiza Tambwe aliyekaririwa akisema wapemba hao ni wahaini, na wanapewa msukumo na CUF.

``Nataka umuulize Tambwe hivi wale wabunge 55 waliotaka iundwe Serikali ya Tanganyika walikuwa wa Chama gaini? Walikamatwa na kufikishwa Mahakamani?``alihoji.

Alisema kama kuna mtu ambaye ameigawa Zanzibar hadi hivi sasa ni Rais Aman Karume, ambaye ameunda Serikali ya upande mmoja.

Bw. Mohamed alisema hata katika ajenda namba tatu ya mazungumzo, wajumbe wote walikubaliana kwamba Karume ameigawa Zanzibar.

Alisema madai ya Tambwe kusema CUF ni chama cha vurugu, sio ya kujenga na wala maneno hayo hayana faida kwa CCM zaidi ya kuleta utengano.

``Kwanza hatujui hayo yalikuwa maneno ya CCM au ya Tambwe Hiza, sisi tumekaa na CCM meza moja kwa miezi 14, kwanini walijadiliana nasi mambo muhimu kama sisi ni magaidi?``alihoji.

Alisisitiza kwamba CUF kimeandikishwa kwa mujibu wa sheria, na hakijapata onyo lolote toka kwa Msajili wa vyama vya siasa kutokana na kukiuka misingi na kanuni za vyama vingi.

Aliionya CCM kwamba Tambwe atawafikisha pabaya kutokana na maneno yake yakufufua shari.

``Huku wanadai turejee kwenye meza ya mazungumzo, huku wanasema sisi ni magaidi, sasa tushike lipi?``alihoji.
  • SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom