Uhusiano Na Hizbu-ccm Vs Cuf Nani Mkweli?

mahazibu si waarabu tu mahizibu kwa mkukusudia ZNP ni wale ambao wanajiita wazalendo wa zanzibar au maalwatwan wao wanaamini kuwa wao ndio wenye haki ya zanzibar na ASP wengi wao ni watwana wakuja na si wenye asili ya Zanzibar na ndio maana watu wanasema CUF ni mahizbu kwa kuwa wao wanasimamia sera zao mfano tokea kuundwa CUF kuna wazanzibari na wazanzibara kwa maana wale wazalendo wa zanzibar na wale wageni.

niliwahi sikia kuwa HIZBU ni wale wote wanaoishi unguja mitaa ya shangani,mji mkongwe,malindi,vikokotoni,mbuyuni fuoni,mwera.
jee hili ni kweli mkuu????
jee HIZBU inauhusiano gani na watu weupe weupe hapa nakusudia wenye maji ya kunde(mfano MSISITIZO :ALLY JUMA SHAMHUNA),waarabu n.k
 
niliwahi sikia kuwa HIZBU ni wale wote wanaoishi unguja mitaa ya shangani,mji mkongwe,malindi,vikokotoni,mbuyuni fuoni,mwera.
jee hili ni kweli mkuu????
jee HIZBU inauhusiano gani na watu weupe weupe hapa nakusudia wenye maji ya kunde(mfano MSISITIZO :ALLY JUMA SHAMHUNA),waarabu n.k

hizbu ilikuwa maeneo mengi, mfano tumbatu, nungwi, bumbwini mkwajuni na sehemu nyenginezo.

hizbu walikuwapo na weusi pia kwani Abrahman Babu alikuwa mweupe au maji ya rangi? au Kwacha nadhani unamjua alikua maji ya kunde mkuu hizbu ilikuwa mchanganyiko na hata nnasikia huyu waziri wetu alikuwa Hizbu sasa yeye umaji wa kunde uko wapi?


Juma Shamhuna tukia asili wao ni ASP piga ua, Donge ni ngome ya ASP tokea zama na hadi leo ni ngome ya CCM.


nimekutosha hapo?

nilisahau na wangazija wengi walikuwa mahizibu zamani
 
hizbu ilikuwa maeneo mengi, mfano tumbatu, nungwi, bumbwini mkwajuni na sehemu nyenginezo.

hizbu walikuwapo na weusi pia kwani Abrahman Babu alikuwa mweupe au maji ya rangi? au Kwacha nadhani unamjua alikua maji ya kunde mkuu hizbu ilikuwa mchanganyiko na hata nnasikia huyu waziri wetu alikuwa Hizbu sasa yeye umaji wa kunde uko wapi?


Juma Shamhuna tukia asili wao ni ASP piga ua, Donge ni ngome ya ASP tokea zama na hadi leo ni ngome ya CCM.


nimekutosha hapo?

nilisahau na wangazija wengi walikuwa mahizibu zamani

sijafahamu hapo,unaposema waziri wetu umekusudia NANI??? mhe mohammed aboud au...????

hilo la wangazija,mie silijui.ahsante kwa kunifahamisha.
 
The story is full of speculations and conspiracy theories, we need more facts. While CUF and CCM keep playing one point game, another child in Pemba is dying because of Malaria or malnutrition.

CUF and CCM needs to stop that stupid game and concentrate on Pemba, we don't care who is affiliated with who.
 
Mwendelezo wa back n forth...


Khatib akana kuhusika na Hizbu

na Tamali Vullu



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Muhammad Seif Khatib, amekanusha shutuma zilizoelekezwa kwake na Chama cha Wananchi (CUF) kuwa ana unasaba na chama cha kisultani cha Hizbu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Khatib alisema wanaomzushia suala hilo hawafahamu historia yake katika masuala ya siasa.
Alisema wakati wa utawala wa serikali ya Hizbu, alikuwa mdogo, na kwamba mwaka 1978 hadi 1982, alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM taifa.
Alisema baada ya hapo, mwaka 1982 hadi 1986, alikuwa Katibu Mkuu wa UVCCM taifa.
“Wanaosema nilikuwa mwanachama wa Hizbu wamechanganyikiwa na ninawapa pole. Pia wanasumbuliwa na uzee,” alisema.
Mwanzoni mwa wiki hii, akitoa tamko la CUF, Katibu Mwenza wa Kamati ya Pamoja (na CCM) ya Mazungumzo ya Muafaka, Ismail Jussa Ladhu, alisema yupo waziri mmoja katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Zanzibar ambaye amekuwa akiandika makala katika magazeti kuiponda CUF, alipata kuwa mwanachama wa Umoja wa Vijana wa Hizbu uliokuwa ukijulikana kama Youth Own Union (YOU).
Ingawa hakumtaja kwa jina, waziri anayetoka Zanzibar ambaye amekuwa akiandika makala kuiponda CUF kupitia magazetini ni Waziri Khatib.
Khatib aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha pamoja kujadili masuala ya Muungano, ambacho sasa kinawahusisha mawaziri wote wa serikali zote mbili.
Mawaziri hao walikutana kutokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete, alilolitoa baada ya kuvunja baraza la mawaziri Februari mwaka huu.
Awali, vikao vya kujadili masuala ya muungano vilikuwa vikizihusisha ofisi za Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi, kabla Ofisi ya Makamu wa Rais haijapewa jukumu la kusimamia na sasa limepanuliwa zaidi na kuhusisha mawaziri wote.
Akifungua kikao hicho jana, Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, alisema baada ya rais kuvunja Baraza la Mawaziri Februari mwaka huu, alibadili mfumo wa kikao hicho.
Akizungumzia kikao hicho, alisisitiza masuala manne ambayo mawaziri hao wanapaswa kuyazingatia wakati wa kikao hicho. Nayo ni kuwa na dhamira ya kweli katika kujadili suala hilo, ili kuleta ufumbuzi kwa lengo la kuimarisha muungano. Alisema dhamira ya serikali hizo mbili ni kuondoa vikwazo, ili muungano uendelee kuwa imara. Pia alisema wanapaswa kuelewana na kuziheshimu katiba na sheria mama zilizopo katika kujadili suala hilo na hatimaye kupata mafanikio mazuri.

Hoja ya kipuuzi ya kujitetea kwai wao wanapowahusisha wenzao na Uhizbu walikuwa tayari watu wazima anajua yeye na Seif wanatafautiana miaka mingapi na mbona wanamhusisha na Hizbu?
 
Wakuu naona mjadala umepamba moto na kwakweli nakiri kuwa tunajifunza mengi!
 
tulichanganya baada ya mapinduzi
sasa ndio makosa ya watu wa mtendeni kulazimisha uhizibu baada ya mapinduzi
 
CUF yatibua mambo

na Waandishi Wetu



KUKWAMA kwa mazungumzo ya kusaka suluhu ya mpasuko wa kisiasa Zanzibar, na matukio ya hivi karibuni yaliyohusisha kukamatwa kwa watu kadhaa wakazi wa Pemba wakihusishwa na uhaini, yamezidi kuleta msukosuko wa kisiasa nchini.
Katika mwendelezo wa matukio hayo, Chama Cha Wananchi (CUF) kimejikuta katikati ya lawama, kikituhumiwa kuhusika na watu hao ambao waliachiwa jana, huku kwa upande mwingine, kikituhumiwa kuchochea vurugu visiwani Zanzibar kwa sababu za kisiasa.
Matukio kadhaa yaliyotokea jana, yaliyafanya masuala hayo kuchukua sura mpya, na kuonyesha kuwa mwisho wake haupo karibu.
Kutoka Zanzibar, Saada Said anaripoti kuwa, hatimaye watu saba waliokuwa mikononi mwa polisi kutokana na kitendo chao cha kupeleka barua Umoja wa Mataifa kutaka kuundwa kwa serikali ya shirikisho, waliachiwa huru jana na kusafirishwa hadi makwao kisiwani Pemba.
Watu hao walikamatwa usiku wa kuamkia Mei 12, mwaka huu na maofisa wa usalama, na kuchukuliwa hadi Unguja walikoshikiliwa katika vituo kadhaa vya polisi kwa mahojiano.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Khamis Mohammed Simba, alithibitisha kuachiwa watu hao na kusema wameridhika na uchunguzi walioufanya.
Alisema baada ya kukamilisha uchunguzi wa awali, wameamua kuwaachia kwa dhamana watuhumiwa hao, huku Jeshi la Polisi likiendelea kuwasaka watu wengine, kwa tuhuma za kuhusika na suala hilo.
Alisema sambamba na kuwaachia huru, pia Jeshi la Polisi litagharamia safari za watu wote saba hadi nyumbani Pemba.
Kamishna Simba alisema taarifa za kutokea tukio la kutaka kujitenga kwa wananchi wa kisiwani Pemba, ziliandikwa kupitia vyombo vya habari, na tangu hapo walianza kufuatilia taarifa hizo kwa umakini kwa kuzingatia suala hilo linajumuisha masuala ya usalama katika nchi.
“Jeshi la Polisi lilishtushwa sana kusikia jambo geni ambalo hapa kwetu halijawahi kutokea kabisa,” alisema.
Akielezea zaidi alisema, jambo lolote linalotendeka Zanzibar linaweza kuathiri Tanganyika kwa kuwa nchi ya Zanzibar na Tanganyika ziliungana na kuifanya Tanzania, hivyo Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa maslahi ya Tanzania.
Hata hivyo, Kamishna Simba hakuwa tayari kuelezea kile kinachotendeka kutokana na utaratibu wa kazi zao, kwa kuwa kueleza mambo kunaweza kuhatarisha upelelezi na mambo yanayofuatiliwa na jeshi hilo.
Alisema kwa kuwa suala hilo ni kubwa na upelelezi wake unahitaji umakini, wataficha taarifa hizo hadi uchunguzi utakapokamilika, kwani wapo baadhi ya watu waliokuwa wamekamatwa, lakini hawahusiki na tuhuma hizo, na pia wapo wengine ambao hawajakamatwa ambao wanahusika.
Kamishna Simba alisema watu wote watakaopatikana na hatia watashitakiwa chini ya sheria ya makosa ya jinai kwa kutaka kuunda Jamhuri ya Kisiwa cha Pemba na kujitenga na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, jambo ambalo ni makosa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ingawa Kamishna Simba hakutaka kusema watu hao watashitakiwa katika mahakama gani, aligusia kwamba upelelezi utakapokamilika na polisi kuridhishwa na ushahidi walioupata kutoka kwa watu hao, watalifikisha suala hilo mahakamani ili watuhumiwa hao wajibu mashtaka chini ya sheria za makosa ya jinai.
“Bado ni mapema kujua watashitakiwa katika mahakama gani kama ya Dar es Salaam au hapa Zanzibar… bado tunakusanya ushaidi,” alisema.
Hata hivyo, waandishi wa habari hawakupewa fursa ya kuonana au kuzungumza na watu hao walioachiwa.
Awali, habari za kuachiwa kwa watu hao, zilitangazwa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, katika mkutano wake na waandishi wa habari.
George Maziku na Elihuruma Kaguo wanaripoti kuwa, katika mkutano huo, Mwema alisema kuwa kuna uwezekano watu wengine wakakamatwa kuhusu sakata hilo.
Alisema wanaowindwa sasa ni wale ambao walitajwa na watu walioachiwa jana, wakati wa mahojiano na polisi.
Kwa upande mwingine, Mwema aliihusisha CUF na harakati za wananchi hao wa Kisiwa cha Pemba kutaka kujitenga.
Alisema upelelezi uliofanywa na jeshi lake umebaini kuwa wahusika wote wa harakati za kutaka Pemba ijitenge ni wafuasi wa CUF, na kwamba harakati hizo zimechochewa zaidi na uamuzi wa hivi karibuni wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwamba suala la kuundwa kwa serikali ya mseto Zanzibar liamuliwe na wananchi kwa kura ya maoni.
Alibainisha kuwa kitendo cha wananchi wa Pemba kutaka kujitenga kutoka Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, ni uvunjaji wa katiba na sheria za nchi, na kwamba hiyo ndiyo sababu ya msingi ya jeshi lake kuwakamata baadhi ya wananchi kisiwani humo, kwa kuwa kazi ya jeshi lake ni kulinda katiba na sheria za nchi.
Alisema kwamba jeshi lake litawaachia kwa dhamana watuhumiwa saba waliokuwa wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukamilisha kuwahoji na kupata ushahidi wa kutosha ambao utawezesha kukamatwa kwa watuhumiwa wengine muhimu.
“Maofisa wa upelelezi wa makao makuu kwa kushirikiana na wenzao wa Zanzibar wamekamilisha kuwahoji wale watuhumiwa saba tuliokuwa tukiwashikilia, hivyo kwa sasa tutawaachia kwa dhamana, lakini tutawakamata watuhumiwa wengine waliotajwa kwa mahojiano zaidi,” alisema Mwema.
Katika hali ya kushangaza na kutia shaka uwezo na umakini wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini, Mwema alikiri kuwa jeshi lake halijajua kosa wanalotuhumiwa kutenda watu hao saba, na kwamba litajulikana baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma nchini (DPP) kuchambua ushahidi wa polisi na kuamuru watuhumiwa wapelekwe mahakamani.
Akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua kama ule ulikuwa ukamataji wa watuhumiwa kisheria au utekaji nyara, kutokana na kuwepo taarifa kuwa ulifanyika usiku wa manane, huku watuhumiwa wakifichwa mahali kusikojulikana kwa zaidi ya saa 24 zinazoruhusiwa kisheria, Kamanda Mwema alisema Jeshi la Polisi lina utaratibu na sheria zake katika kukamata watuhumiwa na kuwahoji.
Aidha, alishindwa kueleza lengo la polisi kuwahoji watuhumiwa hao saba juu ya ufuasi wao wa kisiasa, huku akikana wasiwasi wa baadhi ya waandishi kuwa jeshi lake linatumiwa na watawala kupambana na chama cha CUF.
“Si nia ya Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye malumbano ya kisiasa yanayoendelea hapa nchini, na wala hayo siyo majukumu yake. Hata hivyo, malumbano yoyote ya kisiasa yanatakiwa yawe ya kistaarabu, ya kuvumiliana, ya kupingana bila kupigana na yasiyo na mwelekeo wa kuchochea vurugu au uvunjaji wa amani,” alisema Mwema.
Watu hao saba walikuwa miongoni mwa 12 kutoka Kisiwa cha Pemba, waliowasilisha barua yao hivi karibuni kwenye ofisi za UNDP jijini Dar es Salaam, wakitaka Umoja wa Mataifa kuishinikiza Serikali ya Tanzania kukipa uhuru Kisiwa cha Pemba.
Kitendo hicho kilielezewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Rais (Muungano), Muhammed Seif Khatib, kuwa ni uhaini dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo, Salehe Mohamed anaripoti kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza kuwa CUF imeamua kutumia hali ya mambo visiwani Zanzibar hivi sasa ili kuchochea vurugu.
Kauli hiyo ya CCM ilitolewa jana Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Propaganda Idara ya Itikadi na Uenezi, Tambwe Hiza, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matamshi ya viongozi wa CUF juu ya mazungumzo ya muafaka, na kauli za kashfa wanazozitoa kwa viongozi wa CCM.
Alisema CUF, imekosa mwelekeo wa kisiasa visiwani Zanzibar baada ya kushindwa kuingia serikalini, hivyo inatafuta ajenda ambayo itawafanya wasikike katika masikio ya jamii, ndiyo maana wameamua kudai kuwa kuna machafuko au yatakuja katika visiwa hivyo.
Aidha, Hiza alisema chama hicho kimekuwa kikiwashinikiza wanachama wake kujitenga, kuandaa mazingira ya kuanzisha vurugu Zanzibar, kutupa vikaratasi vya uchochezi vyenye lengo la kuishinikiza serikali kukubaliana na matakwa yao.
Alisema mazunguzo ya muafaka yanatokana na vyama vya siasa, na hivyo kupanga kuanzisha machafuko kwa kutumia kisingizio cha wananchi si jambo la busara. Hiza alisema tatizo kubwa lililopo hivi sasa ni CUF kukataliwa kuhusishwa kwenye serikali, hivyo kuamua kutoa kauli za uchochezi za kutaka kuleta machafuko nchini bila sababu yoyote. Alisema CUF walikuwa wakiomba angalau wachaguliwe mawaziri wawili au watatu kutoka chama chao kabla ya kuelekea katika uchaguzi ujao, lakini ombi hilo lilikataliwa na Rais Aman Karume kwa madai ya kufanywa hivyo ni kinyume cha katiba.
 
Heshima mbele,
Tusizunguke kichaka
Ukweli ni kwamba majority ya wazenj na waislamu wanapenda kuona zanzibar ikirudi ktk tamaduni za kiarabu.
La Pemba kutaka kujitenda,CUF kuhusiana na Hz,au CCM!!ni usanii mtupu.
Naomba tuelewe wenye mapenzi na hao Hz(waarabu) ni wazenj(majority) na waislamu wengine waliomo Tanganyika.
Neno"CCM ni waasisi wa mahusiano na Hz" si sahihi kabisa,kwani wakristo(tulio ndani ya CCM)hatuna mahusiano na mwarabu(Hz) wala mkoloni yeyote.
 
Heshima mbele,
Tusizunguke kichaka
Ukweli ni kwamba majority ya wazenj na waislamu wanapenda kuona zanzibar ikirudi ktk tamaduni za kiarabu.
La Pemba kutaka kujitenda,CUF kuhusiana na Hz,au CCM!!ni usanii mtupu.
Naomba tuelewe wenye mapenzi na hao Hz(waarabu) ni wazenj(majority) na waislamu wengine waliomo Tanganyika.
Neno"CCM ni waasisi wa mahusiano na Hz" si sahihi kabisa,kwani wakristo(tulio ndani ya CCM)hatuna mahusiano na mwarabu(Hz) wala mkoloni yeyote.

Mambo yaenda yakiongezeka!
 
Hakuna mwenye maoni juu ya haya aliyoyasema ndugu yetu Mukombosi?
 
niliwahi sikia kuwa HIZBU ni wale wote wanaoishi unguja mitaa ya shangani,mji mkongwe,malindi,vikokotoni,mbuyuni fuoni,mwera.
jee hili ni kweli mkuu????
jee HIZBU inauhusiano gani na watu weupe weupe hapa nakusudia wenye maji ya kunde(mfano MSISITIZO :ALLY JUMA SHAMHUNA),waarabu n.k

Rangi ya Shamhuna kaipata kwa baba yake naskia ni mtoto wa nje wa Othman Sharrif. Sijui ukweli wa haya lakini wazee walokuwa wanamjua Othman Shariff wanakubali kuwa kalandana ( ni copy) ya Shamhuna.
 
Back
Top Bottom