Uhuru Kenyatta: Ruksa Watanzania kumiliki ardhi, kufanya kazi, kuishi, kuwekeza na kuhamia Kenya bila masharti

Wazo la kufikirika.Kwenye uchumi/Biashara kuna kitu kinaitwa test market.je tukiitumia hiyo principle .Tufanye kila nchi itoe eneo proportional kulingana na ukubwa wa nchi.Eneo hilo ndio likawa ndiyo la political Federation.tukaliangalia baada ya miaka kadhaa matunda yake.kama benefits zinakwenda proportionally tunaongeza eneo.Najua njia hii itachelewesha lengo, lakini nadhani ni salama zaidi .Wataalam wakikaa bila kuingiliwa na ubinafsi wa wanasiasa labda inawezekana.Nadhani wote Federation tunaitaka ila tunaogopana.
 
kawaulize wachaga waliojaa gikomba market ama wale omba omba waliojaa barabarani Nairobi.
Hakuna ombaomba wa Kitanzania nchini Kenya, hili kila mara huwa nalirudia. Kuna matapeli wa Kitanzania huko, wakifanya utapeli kwa njia ya "ombaomba" wengi wao wanatokea ukanda wa ziwa na zaidi ni wasukuma tena wakinyantuzu, hakuna mnyantuzu masikini wa kutupwa huku.

Nawajua baadhi yao, hadi makazi na maisha yao ya huku, wana vipato kuliko hata hao wanaowapa vijisenti huko.
 
Mtu kama wewe unafaa ubaki huko huko Kenya, unajua maana ya mteja?.. mteja ni mtu anayependa kununua na mwenye uwezo wa kununua bidhaa husika, sasa kama kila mtu anapenda kuwa na ndege yake lakini hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kununua, hilo kampuni la kutengeneza ndege lazima litakufa, hapo kutakuwa hakuna accessibility ya hiyo bidhaa kwa wananchi.

Ardhi ya Kenya haipo accessible kwa wananchi wa kawaida, ni sawa na kufungua kiwanda cha kutengeneza ndege hapa East Afrika then tukajisifia kwamba tumewasogezea karibu upatikanaji wa ndege hapa hapa EA, hakuna haja ya kwenda Europe au USA.
Na ni sawa pia na unyonyaji wa chumi za kibepari kwa mgongo wa globalisation, Mwalimu alishawahi Kuuliza,, "je NMB inaweza ikafungua branch New York na kuopareti"? Wajinga ndio waliwao.
 
Mtu kama wewe unafaa ubaki huko huko Kenya, unajua maana ya mteja?.. mteja ni mtu anayependa kununua na mwenye uwezo wa kununua bidhaa husika, sasa kama kila mtu anapenda kuwa na ndege yake lakini hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kununua, hilo kampuni la kutengeneza ndege lazima litakufa, hapo kutakuwa hakuna accessibility ya hiyo bidhaa kwa wananchi.

Ardhi ya Kenya haipo accessible kwa wananchi wa kawaida, ni sawa na kufungua kiwanda cha kutengeneza ndege hapa East Afrika then tukajisifia kwamba tumewasogezea karibu upatikanaji wa ndege hapa hapa EA, hakuna haja ya kwenda Europe au USA.
rais hajasema mtoe mashamba yenu nyie wachawi:D
 
Unajua bei ya ardhi ya Kenya wewe?.Serikali ya Kenya haina ardhi.Ardhi ni mali ya matajiri akina Uhuru Ruto Raila na wengine.Ubavu huo wa watz kuinunua ardhi hiyo watautoa wapi?
 
Ww jamaa utakuwa unaishi Kisarawe Dar na hujawahi kutoka nje ya dar, nenda saiti kijana

Kuna watanzania wengi sana wanamiliki ardhi nchini kenya, ana Wapo Watanzania wengi sana wamekodi mashamba nchini Kenya kwaajili cha Mahindi na Maharange

Vichwa vyenu sijui vipoje, wakenya wengi sana hasa wakamba ni wavivu kulima na yale mashamba yao wamewauzia Watanzania na mengine wameyakodisha kwa Watanzania......

Tembeeni
Acha uongo wewe, kwanini mamilioni ya wakenya wamevuka mpaka kuja kutafuta ardhi ya kilimo na malisho ya mifugo huku Tanzania?, Ukubwa wa nchi ya Kenya ni sawa na nusu ya ukubwa wa Tanzania, na idadi ya watu ni karibu inalingana, na 2/3 ya ardhi ya Kenya haifai kwa kilimo, na hiyo 1/3 inayofaa kwa kilimo 50% inamilikiwa na matajiri na wanasiasa, hiyo ardhi unayosema wewe ni ipi?
 
Danganya toto ili nasisi tuwaruhusu waje wamiliki ardhi na wafanye kazi huku. Kwa ardhi gani ya kupata kenya kama wenyewe tu wanastruggle kumiliki. Kazi ndo usiseme ajira finyu, Magufuli usiruhusu hii bongo tuendelee tu na utaratibu wa sasa.
 
rais hajasema mtoe mashamba yenu nyie wachawi:D
Sisi tunajua ni njia moja wapo ya kutaka wananchi wa Kenya waweze kuruhusiwa kwenda nchi yoyote kuanzisha makazi, hapo utaona makundi kwa makundi ya wapokot, na Turkana wakihamisha mifugo yao na kuvuka mpaka kuja huku, kule kaskazini wameshatengeneza jangwa, mapigano ya kule ni kwa ajili ya malisho na maji ya mifugo, wakisikia wanaruhusiwa kuja Tanzania, nchi ambayo eneo lake sawa na size ya nchi ya Kenya limehifadhiwa kama mapori ya taifa, ni green throught a year, wapokot wataacha kuja?
 
Shida ya viongozi wa waafrica kujifanya miungu watu, sasa uhuru kwani yeye Kenya ni mali yake, kuruhusu watu wamiliki ardhi ya watu wa Kenya akumbuke anapita tu, na kenya itadumu milele.

Wanatakiwa kuamua mambo yanayoweza kubadirika what if anakuja mwingine hataki watu wamiliki ardhi, hili suala lazima liwe na mjadala wa kitaifa.
 
Mkuu kwa hili hapana. Kenyatta ardhi yote asilimia kubwa ni ya familia yake. Hii hapana Tanzania hatutakuwa na wema huo kabsaaa. Ardhi yetu hakuna kutoa kwa wasio watz.
Ardhi yenyewe ya Tanzania pia INA mazonge kibao.sidhan kama mtanzania billionaire ataweza wekeza hapa kwa system hii iliyopo,system ya kipuuzi hii.
 
Acha uongo wewe, kwanini mamilioni ya wakenya wamevuka mpaka kuja kutafuta ardhi ya kilimo na malisho ya mifugo huku Tanzania?, Ukubwa wa nchi ya Kenya ni sawa na nusu ya ukubwa wa Tanzania, na idadi ya watu ni karibu inalingana, na 2/3 ya ardhi ya Kenya haifai kwa kilimo, na hiyo 1/3 inayofaa kwa kilimo 50% inamilikiwa na matajiri na wanasiasa, hiyo ardhi unayosema wewe ni ipi?
Kamani%2B3.jpg
 
Ukiwa na pesa yako tu unanunua ardhi Kenya na ipo ya kutosha.
Hiyo ardhi ya kutosha mbona haijawatosha wakenya!
Hawa wametega! Sehemu kubwa ya ardhi Kenya inamilikiwa na wachache sana! Halafu ni ghali sana kiasi hakuna mkenya wa kawaida anaweza kununua!
Hiyo kauli ingetolewa na Tanzania kungekuwa na mass exodus toka Kenya Uganda na Rwanda kuja kujipatia ardhi Tanzania ambayo ni nyingi sana na bei rahisi sana!
 
Serikali ya Kenya haimiliki ardhi kwa hiyo haina uhalali wa kuisemea ardhi! Ardhi ya Kenya inamilikiwa na watu binafsi! Kenyata hawezi kuisemea ardhi ya Kenya, ni uongo!
Sisi Tanzania ardhi inamilikiwa na serikali! Kwa hiyo kauli ya serikali kwa ardhi ni ya kuaminika!
 
Mi hata nawashangaa mkiongelea kuhusu ardhi kenya ilhali wengi wenu hamjawahi kanyaga Kenya na hamjui lolote,uliza yeyote, Kenya ni ndogo kwa map lakini ni kubwa sana ukiwa hapo, ardhi zinauzwa kila Mahali. Hata leo leo ukitaka ardhi by jioni ukilipa deposit utapata shamba, huku kenya ardhi ni kama vile kununua gari
 
Back
Top Bottom