Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,255
- 19,100
- Thread starter
- #61
Swali limeulizwa hapa mara kadhaa, kwa nini wanaoona kero za muungano iwe ni Zanzibar peke yake? Kuna uratatibu gani wa kukusanya kero za muungano za Watanzania bara ili nazo zishughulikiwe, au haiwezekani kwa sababu bara hawana serikali?Muungano uboreshwe hapo tunaongea lugha moja. Na ndiyo maana kuna Wizara inayoshughulikia kero za Muungano chini ya Makamu wa Rais. Halafu kuna Tume ya Fedha ya pamoja ndani ya Wizara ya Fedha ya JMT.
Na pia, kwa nini utatuzi wa hizo kero 18 zilizoshughulikiwa hauwekwi wazi - je ni hofu ya kwamba hizo kero zimeshughulikiwa kwa namna ambayo watu wa bara wakijua kilichofanyika watachukia na kuona kuna upendeleo zaidi unafanywa kwa Zanzibar, au kwamba kero zimetatuliwa kwa namna ambayo inazidi kudhoofisha muungano? Na watu wanauliza, kwa nini kero za muungano zimeshughulikiwa nyingi na kwa kasi katika kipindi cha Raisi Samia, na huko nyuma marais toka bara walisita kuwakubalia Zanzibar juu ya kuondoa kile wanachoita kero za muungano?
Kwa mfano kero moja ya muungano upande wa bara - ni kitendo cha watu wa bara kutozwa umeme kwa bei ambayo inalenga kufidia hasara wanayopata Tanesco kwa sababu Zanzibar siku zote hawataki kulipia umeme. Lini hili litaisha? Kwa nini nilipishwe umeme kwa bei ya kuwabeba Zanzibar?