Wana JF,
Naona wengi wamekereka na matokeo ya F4, na kwa kweli ni aibu ya taifa kuonyesha kwamba karibia wanafunzi wote wamefeli (kwani mimi nasema ukipata Division IV umefeli). Na pia, naona wengi mnatafuta chanzo cha matokeo haya.
Ukitaka kujua kwa nini elimu ya TZ inaendelea kushuka chini, hapa nitakupa jibu kamili: ni kwa sababu serikali ilikuwa na mpango wa kijinga kujenga hovyo hizi shule za kata.
Zamani, watanzania wachache kabisa walikuwa wanamaliza elimu ya sekondari. Lakini wale walioingia sekondari walikuwa na uhakika zaidi kwamba watafundishwa vizuri na walimu ambao ni wataalamu.
Shida ni kwamba baadaye, serikali imeletewa presha kutoka nje kwamba ni lazima watoto wote wasome (hiki kitu kinaitwa Universal Education au Education For All).
Sasa serikali ya nchi hii ilichukua hatua ya kujenga shule kwanza, na kutafuta walimu baadaye. Yule aliyeamua hivyo alifanya kosa kubwa sana, kwa sababu katika elimu KITU CHA MSINGI KABISA NI WALIMU, SIYO MAJENGO.
Bora uwe na mwalimu ambaye anapenda kufundisha na ambaye anajua vizuri sana masomo anayofundisha halafu yule mwalimu awafundishe watoto chini ya mti, kuliko kuwa na majengo ambayo walimu wanaofundisha ndani ni wajinga (au hakuna walimu kabisa).
Nchini huku unaweza kuta shule ya kata ambayo ina wanafunzi 600 na walimu 3. Je, katika shule kama hii wanafunzi watafundishwa nini? Halafu hiyo shule haina maabara, haina maktaba, na haina kompyuta.
Kwa hiyo naomba niwape huu ujumbe kwamba kujenga shule bila kuwa na walimu wa kutosha na wenye vigezo vinavyostahili kunasababisha matokeo kama ya mwaka 2012.