Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 15,877
- 20,730
Published Oktoba 21, 2022
Najaribu kulizungumzia hili kwa sauti kubwa niwezavyo ili watu wanielewe.Ni kwamba mikakati imeshabuniwa na imeshawekwa ili uhaba wa chakula 2023 na kuendelea uwe mbaya zaidi kuliko wakati wowote katika Historia ya Wanadamu,kwa hiyo ni lazima tujiandae.
Kwa wenye akili na macho ya uchunguzi,uhaba wa chakula duniani unaendelea kushika kasi, na mambo yatakuwa mabaya sana mwaka wa 2023 na kuendelea.
Kama inavyofahamika ni kwamba,theluthi mbili ya uzalishaji wa mbolea ya Ulaya tayari umesitishwa.Yapo pia matatizo ya kupungua kwa thamani ya Fedha, ambayo yanasababisha ugumu wa kuagiza bidhaa kwa mataifa maskini yanayohitaji kuagiza mbolea na chakula kutoka nje.Mifumo ya hali ya hewa ya kimataifa nayo inaendelea kuharibika, na mafua ya ndege yanaua mamilioni kwa mamilioni ya kuku na bata mzinga katika sayari nzima. Mbaya zaidi,vita ya Ukraine itazuia uuzwaji wa mazao ya kilimo na mbolea kutoka sehemu hiyo ya dunia kwa muda mrefu ujao, kwa sababu dalili za kwisha kwa Vita hiyo haionekani. Kimsingi, tunakabiliwa na "dhoruba kamili" kwa ajili ya uzalishaji wa chakula duniani, na "dhoruba hiyo kamili" itazidi kuwa mbaya zaidi katika miezi na miaka ijayo.
Njaa ya kimataifa imekuwa ikiongezeka kwa miaka mingi sasa kwa kasi. Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa umeonya kwamba tunaelekea “mwaka mwingine wa njaa usio na rekodi."Dunia iko katika hatari ya mwaka mwingine wa njaa ambayo haijawahi kurekodiwa,huku mzozo wa chakula duniani ukiendelea kusababisha watu wengi zaidi kuingia katika viwango vya njaa vinavyozidi kuwa vibaya," limeonya Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) katika wito wa kuchukua hatua za haraka kushughulikia chanzo cha njaa.
Mgogoro wa chakula duniani ni muunganiko wa migogoro shindani inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, migogoro ya nchi na nchi na matatizo ya kiuchumi,ambayo yametengenezwa.Haya yote yamesababisha idadi ya watu wenye njaa kali kote ulimwenguni kuongezeka kutoka milioni 282 hadi milioni 345 katika miezi ya kwanza tu ya 2022.
Kwa sababu hii, Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa umeongeza shabaha za usaidizi wa chakula kufikia rekodi ya watu milioni 153 katika mwaka wa 2022. Kufikia katikati ya mwaka,mpango huo tayari ulikuwa umetoa msaada kwa watu milioni 111.2.Naomba nionye hata hivyo kwamba , huu ni mwanzo tu. Hatimaye, kutakuwa na mabilioni ya watu ambao hawana chakula cha kutosha mara kwa mara Dunia nzima. Katika miaka ya maisha yangu yote, sijawahi kuona njaa ikienea kwa kasi hivi. Kwa hakika, kuna idadi kubwa ya watu ambao sasa wanakabiliwa na njaa Tanzania na duniani kote.
Umoja wa Mataifa unaonya kuwa nchi za Haiti,Ethiopia na Somalia zipo katika viwango vya maafa, huku ghasia za magenge na mizozo ya kiuchumi ikisukuma nchi Kama Haiti kufikia "hatua ya kusambaratika". "Takriban watu 20,000 katika eneo maskini kabisa la mji mkuu wa Haiti uitwao Cité Soleil wana uwezo mdogo sana wa kupata chakula na wanakabiliwa na njaa," Umoja wa Mataifa unasema. Kote Haiti, karibu milioni tano wanapambana na utapiamlo. "Haiti inakabiliwa na janga la kibinadamu," Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema. Lakini watu wengi katika ulimwengu wa magharibi hawatajali hadi watakapokuwa na njaa wenyewe,ingawa nako hali si shwari. Kwa bahati mbaya, siku hiyo inaweza kuwa karibu sana kuliko watu wengi wanavyodhani.
Kwa sasa, theluthi mbili ya uwezo wote wa kuzalisha mbolea barani Ulaya tayari umepotea kwa sababu ya kupanda kwa bei ya gesi asilia.Uhaba wa mbolea barani Ulaya unazidi kuongezeka huku zaidi ya theluthi mbili ya uwezo wa uzalishaji wa mbolea ukisitishwa kwa sababu ya kupanda kwa gharama ya gesi na hivyo kutishia wakulima na watumiaji mbali zaidi ya mipaka ya eneo hilo. Kusitisha kwa Urusi usafirishaji gesi kufuatia mzozo wa Ukraine kunaathiri viwanda kote Ulaya. Lakini makampuni ya mbolea yanaathirika zaidi kwa sababu gesi ni nyenzo muhimu na chanzo cha nishati kwa sekta hiyo. Hii Ina maana kwamba hakutakuwa na mbolea ya kutosha kwa wakulima wa Uropa na Dunia mnamo 2023 na kuendelea.Hili ni jambo la hatari sana na baya, kwa sababu bila mbolea wakulima wa Dunia wanaweza tu kulisha takriban watu billion 3.8.