Ugonjwa wa Ngiri (Hernia), Dalili na tiba yake

Habari wanajamvi! Samahani kama hii mada ilishawa ongelewa kabla. Naomba nipewe elimu kuhusu ugonjwa wa CHANGO na NGIRI. Ni nini kinachosababisha, nini madhara kiafya, pia ni nini madhara ktk mapenzi? Pia tiba inakuwaje? Asanteni!
 
jamani naombeni mnisaidie dawa ya mships wangiri, hii kitu inanitesa sana, kama kuna mtu ana uelewa kidogo juu ya hili naomba msaada wake kwanzia mudaa huu iliniweze kufanyia kazi mara moja..
 
Mkuu.@DelvisKuhusu tiba ya ngiri inatakiwa ufanyiwe upasuaji Operesheni inategemea Ngiri zipo za aina 2 ya kwanza ni ya ndani inaitwa kwa kiingereza ( Hernia)


Na Ngiri ingine ni ya Mshipa wa Kushuka ni hii hapa Mabusha kwa lugha ya kiswahili






I
Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu. Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani.
Inakadiriwa kuwa karibu asilimia moja ya wanaume wote kote duniani huathiriwa na tatizo hili. Kwa hapa nchini, tatizo hili ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kiasi cha kuhusishwa na imani kadhaa.

Mojawapo ya dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wa mwambao ni kuwa mabusha yana uhusiano mkubwa na unywaji wa maji ya madafu. Aidha, tatizo hili limekuwa likichukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni hali ya kudhalilisha ingawa kwa wengine huonekana ni hali ya kuwa ‘mzee wa heshima' au ‘umwinyi'.


Ifahamike pia kuwa, tatizo la mabusha halitokei kwa wanaume watu wazima tu. Watoto wa kiume hususani katika mwaka wa kwanza (infants) pia ni waathirika wakuu wa tatizo hili.


Kwa kawaida mabusha hayana maumivu na wala hayaleti madhara, isipokuwa kama yatapata uambukizi kwa sababu nyingine yeyote ile, hali inayowafanya wengi wa waathirika, hasa wa mwambao, kuwa wagumu kutafuta ufumbuzi wa tiba.


Hata hivyo, ni vyema kama mtu ana uvimbe wowote kwenye pumbu zake, kutafuta msaada wa kitabibu ili kuweza kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa mengine ya sehemu za siri kama vile saratani ya korodani (testicular cancer) n.k.

Mabusha husababishwa na nini?

Sababu za kutokea kwa mabusha hutofautiana kati ya watoto wa kiume na wanaume watu wazima.



Kwa watoto wa kiume
Kwa watoto wa kiume, mabusha huweza kuanza kutokea kipindi cha ujauzito.
Wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea kwenye mapumbu. Wakati wa ushukaji huo, kifuko kinachozunguka korodani kinachoitwa processus vaginalishushuka sambamba na kurodani hizo na kufanya korodani kuzungukwa na maji.

Kwa kawaida, ndani ya muda wa mwaka mmoja, kifuko hiki hufunga na maji hayo yanayozunguka korodani yote hufyonzwa na kurudishwa kwenye tumbo la mtoto. Iwapo baada ya kifuko kufunga na maji yaliyomo kushindwa kufyonzwa kurudishwa kwenye tumbo la mtoto, mtoto hupata busha lijulikanalo kitaalamu kama busha lisilo na mawasiliano (non-communicating hydrocele).


Hali kadhalika, wakati mwingine inawezekana kifuko kikashindwa kufunga na hivyo maji yakaendelea kujaa ndani ya kifuko kuzunguka korodani. Aina hii ya mabusha kwa watoto ujulikana kama busha lenye mawasiliano (communicating hydrocele).


Kwa wanaume watu wazima

Kwa wanaume watu wazima, mabusha husababishwa na mambo makuu mawili; Kwanza, kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida, na njia ya pili ni kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system).

Ongezeko la uzalishaji wa maji linaweza kutokana na


  • Maambukizi au/na majeraha katika korodani (testicular inflammation auorchitis) au maambukizi katika mshipa ujulikanao kamaepididymisyanayoweza kusababishwa na kifua kikuu (tuberculosis) cha makende, au maambukizi yanayosababishwa na vimelea wa filaria(filariasis) wanaosababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.
  • Kujinyonga kwa korodani (testicular torsion) kunakoweza kuzifanya korodani kutenda kazi zaidi ya kiwango chake (hyperactive testis).
  • Uvimbe katika korodani (testicular tumors) ambao husababisha uzalishaji wa maji kupita kiasi.

Kupungua kwa ufyonzaji wa maji hutokana na

  • Kufanyiwa upasuaji kipindi cha siku za nyuma katika eneo la kinena, au operesheni ya upandikizaji figo ambazo zinaweza kuathiri mfumo wa lymph na vena na hivyo kupunguza ufyonzaji wa maji kutoka kwenye mapumbu.
  • Kuwahi kufanyiwa tiba ya mionzi kipindi cha nyuma nayo uhusishwa na kutokea kwa mabusha.

Kwa hapa kwetu Tanzania, kung'atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha na matende hususani maeneo ya Pwani na mwambao.

Dalili za Mabusha

Katika hatua za awali, mabusha huwa hayana dalili zozote (asymptomatic).
Hata hivyo, baada ya muda fulani, mapumbu hujaa na uvimbe huweza kuonekana hata kwa nje. Kwa kadiri uvimbe unavyozidi kuongezeka, dalili zifuatazo zaweza kujitokeza pia;

  • Muhusika kujihisi hali ya uzito na kuvuta sehemu za siri kutokana na kujaa na kuongezeka kwa uzito wa mapumbu.
  • Mgonjwa huweza kujihisi hali ya usumbufu na kutojisikia vizuri maeneo ya kinena mpaka mgongoni.
  • Kwa kawaida mabusha hayana maumivu yeyote. Hata hivyo, iwapo mgonjwa ataanza kujihisi maumivu, hiyo ni dalili ya kuwepo kwa uambukizi katika mshipa wa epididymis (acute epididymitis)
  • Uvimbe huwa na tabia ya kupungua iwapo mgonjwa atakaa kitako na huongezeka pindi anaposimama.
  • Iwapo mgonjwa atajisikia homa, kichefuchefu na kutapika, hizo ni dalili za kuwepo kwa uambukizi katika mabusha.
  • Kwa kawaida mabusha hayana muingiliano na uwezo na ufanisi wa utendaji wa ngono. Hata hivyo kuna taarifa tofauti za kitafiti kutoka bara Asia na Afrika Magharibi kuwa mabusha yanaweza kuathiri ufanisi wa ngono na kwa kiasi fulani kusababisha mhemko au msongo wa mawazo kwa muathirika.

Uchunguzi na Vipimo

Uchunguzi mzuri wa kitabibu (physical examination) huwezesha kugundua uwepo wa mabusha kwa kiasi kikubwa bila hata kuhitaji vipimo vya ziada. Vipimo uhitajika tu kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha mabusha, madhara yaliyoletwa na mabusha au kujua hali ya korodani.

Vipimo ni pamoja na

  • Kupima damu (Full Blood Count) na mkojo (Urine Analysis) kuchunguza uwepo wa maambukizi kama vile vimelea wafilaria na mengineyo.
  • Ultrasound ya kinena pamoja na mapumbu: Aina hii ya kipimo hufanywa ili kuchunguza uwepo wa matatizo mengine tofauti na mabusha. Matatizo hayo ni kama vile ngiri, uvimbe, kujinyonga kwa korodani (testicular torsion), majeraha katika korodani, damu kuvuja kwenye kwenye korodani (traumatic hemorrhage) au maambukizi.


Matibabu ya Mabusha


Kwa watoto wadogo, kwa kawaida mabusha hupotea yenyewe ndani ya mwaka mmoja. Iwapo hayajapotea, mtoto uhitaji kufanyiwa upasuaji kama tiba.

Kwa wanaume watu wazima, mabusha pia huweza kupona yenyewe bila kuhitaji tiba. Iwapo mabusha hayajapotea na yanamletea mgonjwa usumbufu (discomfort) au hali mbaya ya kiumbo (disfigurement) hayana budi kufanyiwa upasuaji ili kuyaondoa.
Njia za tiba ni

  • Upasuaji: Upasuaji wa mabusha huweza kufanyika bila ya mgonjwa kuhitaji kulazwa (outpatient). Madhara yanayoweza kutokea wakati wa upasuaji wa mabusha ni pamoja na damu kuganda (blood clots), maambukizi au majeraha kwenye korodani. Hii ndiyo njia maarufu zaidi na ya kuaminika ya matibabu ya mabusha duniani kote.



  • Kunyonya maji kwa kutumia sindano maalum (Needle aspiration): Njia nyingine inayotumika kutibu mabusha ni kuyanyonya maji kwa kutumia sindano maalum (needle aspiration). Hata hivyo njia hii haitumiki sana sehemu nyingi duniani kwa sasa kwa sababu maji ya mabusha huwa yana tabia ya kujirudia baada ya muda mfupi hata kama yatanyonywa.

Baadhi ya matabibu hupendelea kudunga dawa maalum za kuzuia maji yasijae tena (sclerosing agents) mara baada ya kunyonya na kuyaondoa maji yote.
Njia hii ya kunyonya maji ya mabusha, hufaa zaidi kwa wagonjwa wasioweza kuhimili upasuaji. Madhara yanayoweza kusababishwa na tiba ya namna hii ni pamoja na maambukizi na maumivu kwenye korodani.
Hata hivyo wakati mwingine, bila kujali ni tiba gani imetumika, mabusha huweza kujirudia baada ya matibabu.

Madhara ya Mabusha

Kwa kawaida mabusha hayana madhara yeyote. Aidha mabusha hayawezi kuathiri uwezo wa mtu kuzaa. Hata hivyo mabusha yanaweza kuleta madhara iwapo tu kama yakiambatana na magonjwa mengine kwenye korodani.
Kwa mfano, kama mabusha yataambatana na maambukizi (testicular infection) au uvimbe kwenye korodani (testicular tumor), yanaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji na utendaji kazi wa mbegu za kiume (sperms) na kupelekea tatizo la ugumba kwa wanaume.

Hali kadhalika, iwapo sehemu ya utumbo mkubwa au mdogo imebanwa katika upenyo fulani kwenye sehemu ya ukuta wa tumbo, huweza kusababisha ngiri (strangulated hernia), hali ambayo ni hatari kama isipotibiwa haraka.

Mkuu ninakushauri utumie Asali kijiko kimoja na na pilipili mtama kijiko kidogo kunywa itakusaidia kutuliza hayo maumivu yako na uwe kila siku unakunywa maji ya uvuguvgu kila asubuhi unapo amka glasi 3 na ukae saa moja kabla ya kunywa chai na

wakati wa mchana uwe unakunywa maji ya uvuguvugu glasi moja na ukae saa moja bila ya kula na wakati wa usiku unywe maji ya uvuguvugu glasi 1 kisha ukae saa moja pasipo kula kisha waweza kula chakula cha usiku na wakati wa kulala wa kulala unywe

glasi moja kisha ulale fanya hivyo kila siku itakusaidia haya maji ya uvuguvugu kwa Afya yako inshallah. Na pia uende kufanya Oparesheni ya upasuaji sio kubwa ni ndogo tu.Mkuu.@
Delvis

 
Last edited by a moderator:
Mkuu Polisi Kwa Maelezo yako uliyoyatoa hapo juu matatizo yako yote yanasababishwa na hiyo GERD 2" HIATAL HERNIA fuatilia kwa makini ushauri wa Ma-Daktari utafanikiwa kupona inshallah.


Hiatal Hernia

Any time an internal body part pushes into an area where it doesn't belong, it's called a hernia.​
The hiatus is an opening in the diaphragm -- the muscular wall separating the chest cavity from the abdomen. Normally, the esophagus (food pipe) goes through the hiatus and attaches to the stomach. In a hiatal hernia (also called hiatus hernia) the stomach bulges up into the chest through that opening.​
There are two main types of hiatal hernias: sliding and paraesophageal (next to the esophagus).​
hiatal_hernia_hiatal_hernia.jpg

In a sliding hiatal hernia, the stomach and the section of the esophagus that joins the stomach slide up into the chest through the hiatus. This is the more common type of hernia.​

The paraesophageal hernia is less common, but is more cause for concern. The esophagus and stomach stay in their normal locations, but part of the stomach squeezes through the hiatus, landing it next to the esophagus. Although you can have this type of hernia without any symptoms, the danger is that the stomach can become "strangled," or have its blood supply shut off.​

Many people with hiatal hernia have no symptoms, but others may have heartburn related to gastroesophageal reflux disease, or GERD. Although there appears to be a link, one condition does not seem to cause the other, because many people have a hiatal hernia without having GERD, and others have GERD without having a hiatal hernia.​
People with heartburn may experience chest pain that can easily be confused with the pain of a heart attack. That's why it's so important to undergo testing and get properly diagnosed.


What Causes a Hiatal Hernia?

Most of the time, the cause is not known. A person may be born with a larger hiatal opening. Increased pressure in the abdomen such as from pregnancy, obesity, coughing, or straining during bowel movements may also play a role.

Who Is at Risk for Hiatal Hernia?


Hiatal hernias occur more often in women, people who are overweight, and people older than 50.
How Is a Hiatal Hernia Diagnosed?

A hiatal hernia can be diagnosed with a specialized X-ray (using a barium swallow) that allows visualization of the esophagus or with endoscopy.

How Are Hiatal Hernias Treated?


Most people do not experience any symptoms of their hiatal hernia so no treatment is necessary. However, the paraesophaeal hernia (when part of the stomach squeezes through the hiatus) can in some cases cause the stomach to be strangled, so surgery is sometimes recommended. Other symptoms that may occur along with the hernia such as chest pain should be properly evaluated. Symptoms of GERD should be treated.

When Is Hiatal Hernia Surgery Necessary?


If the hiatal hernia is in danger of becoming constricted or strangulated (so that the blood supply is cut off), surgery may be needed to reduce the hernia, meaning put it back where it belongs.
 
Nakumbuka nilikuja humu jf na kueleza tatizo langu na mchangiaji mmoja nadhani ni Riwa (sijui kama yupo huyu ndugu, sijamwona siku nyingi) alionesha wasiwasi wake kama kweli ilikuwa bado ULCERS kwa jinsi nilivyotumia dawa mbalimbali

Nipo ndugu yangu, majukumu tu ya kikazi hupelekea kuwa vijijini huko nikijali afya za waTanzania wa 'kweli' hasa watoto na kina mama...na huwa napotea hapa JF from time to time. Pole sana kwa tatizo! Mimi bado nadhani una tatizo zaidi ya ulcers...na pengine zaidi ya 'Hiatal Hernia'. Nadhani tatizo lako kubwa (narudia...nadhani) ni la kisaikolojia kutokana na trauma ya kisaikolojia uliyopata kwa miaka minne (FOUR YEARS!)...si mchezo! Na nadhani hiyo imepelekea tatizo huwa tunaita ' Somatoform Disorder'

In psychology, a somatoform disorder is characterized by symptoms that suggest physical illness that cannot be explained fully by a general medical condition or by the direct effect of a substance, and are not attributable to another mental disorder (e.g., panic disorder). The symptoms of a somatoform disorder are considered to be due to a hard wiring problem within the brain where thoughts are sent down into the body through the Autonomic Nervous System to become symptoms instead of being sent up into the conscious area of the brain.

In people who have a somatoform disorder, medical test results are either normal or do not explain the person's symptoms, and history and physical examination do not indicate the presence of a medical condition that could cause them. Patients with this disorder often become worried about their health because doctors are unable to find a cause for their symptoms. This may cause severe distress. Preoccupation with the symptoms may portray a patient's exaggerated belief in the severity of their ill-health.Symptoms are sometimes similar to those of other illnesses and may last for several years.

Nadhani mental trauma ambayo ulipata ulipodhani una HIV na ukaanza ishi hivyo, na series ya dalili ambazo umekuwa ukizipata (kweli una ulcers na hiatal hernia) haziwezi elezea kwa ujumla nini ni taizo au ugonjwa wako. Ila hiyo historia ya 4 years of mental trauma na kwa dalili ulianza kuzisikia baada ya kupata hiyo mental trauma...zinanifanya niamini kuwa tatizo lako kubwa (zaidi ya ulcers na hiatal hernia) ni somatoform disorder. Ni vizuri kupata matibabu ya hayo matatizo mawili yaliyoonekana (japo sidhani kama hiatal hernia yako inahitaji upasuaji), lakini ni vizuri pia ukamuona psuchologist/psychiatrist akuevaluate zaidi. kwani kama ni somatoform, hata ukifanyiwa upasuaji wa hiatal hernia bado utaendelea kujisikia una tatizo la kiafya.
 
Nadhani tatizo lako kubwa (narudia...nadhani) ni la kisaikolojia kutokana na trauma ya kisaikolojia uliyopata kwa miaka minne (FOUR YEARS!)...si mchezo! Na nadhani hiyo imepelekea tatizo huwa tunaita ' Somatoform Disorder'

Patients with this disorder often become worried about their health because doctors are unable to find a cause for their symptoms. Ni vizuri kupata matibabu ya hayo matatizo mawili yaliyoonekana (japo sidhani kama hiatal hernia yako inahitaji upasuaji), lakini ni vizuri pia ukamuona psuchologist/psychiatrist akuevaluate zaidi. kwani kama ni somatoform, hata ukifanyiwa upasuaji wa hiatal hernia bado utaendelea kujisikia una tatizo la kiafya.
Mkuu Riwa, kwanza nikupongeze kwa kuonesha umahili wako hapa kwa sababu baada ya kwenda kuonana na daktari alionekana kutoshtuka kabisa as if ni mgonjwa mdogo sana. Amenipa dawa ya miezi miwili (opromazole) nirudi mwezi julai.

Nalinganisha na kauli yako hapo kwenye blue; Je, hao psychiatrist wanapatikana hospitali zipi?
 
Back
Top Bottom