Ugali ni chakula ambacho hakijawahi tengwa mahsusi kwenye meza kuu za Wafalme na Masultani, kinahusishwa na uduni wa kiuchumi

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,234
4,761
Wadau wenzangu wa JF & Watanzania wote

Naandika haya nikiongozwa kwa dhamira nzuri ya kueleza ukweli bila kuwa na nia ya kuwakera baadhi yenu

Sikusudii kupotosha, kukashfu, kudharau historia yetu, au makuzi yetu, au aina fulani ya chakula, kikundi fulani
kwenye jamii yetu n.k

Nazungumza chakula maarufu duniani kinachotokana na mahindi almaarufu Ugali

Nitazungumzia kwa ufupi kuhusu Ugali Chakula ambacho;

Kwa asili hakijawahi kuwa sehemu ya vyakula vinavyote gwa kwenye meza kuu ya Wafalme au Masultani!

Hakijawahi kuwa Maalumu au mahsusi kwa ajili ya wageni

Hakijawahi kuwa Maalumu au Mahsusi hata kwa ajili ya wagonjwa au walio na njaa kali

Ni chakula kinachohusishwa na Utwana au Utumwa au hali ya umasikini

Kimekosa ufahari mbele ya jamii hasa baada ya kukitumia

Kinahusishwa na udumavu wa maendeleo ya taaluma kwa wanaokitumia kwa muda mrefu tofauti na wanaotumia vyakula vinginevyo kama mpunga, ngano, shayiri, mtama, ulezi au hata ndizi n.k

Naomba kuwasilisha

Karibuni kwa mjadala

Aksanteni

Nakala: Paschal Mayala
 
Ni kweli na nimependa sana hapo mwishoni ulipotaja aina ya vyakula.

Ila sasa nakuomba tuachie wenyewe huu ugali asee ugali ni kitu kingine kabisa, yaani ugali kwa samaki, losti ya dagaa kwa mbogamboga, asee!.

Acha tu hao wafalme waendelee kula wali na ulojo, kuna time inafikia huwa kuna kazi tunawasaidia.
 
Mahindi ni chakula cha mifugo sisi tunakula kama mazoea tu. Hakina faida yoyote kwa mwili hasahasa ubongo. Kuna utafiti ushafanyika unaonesha Mediterranean diet ni bora kuliko zote. Kile chakula wanachokula wanawaizrael wa kwenye biblia ni bora. Wanakula ngano isiyokobolewa (mkate), samaki, mafuta ya mizeituni (olive oil) na zabibu.

Hiyo milo ni bora kwa afya na hasa ubongo kwakuwa kuna omega 3 ambayo inaongeza uwezo wa ubongo kufikiri na kubuni. Ndio maana huku sisi akili zetu zimeathiriwa na ulaji mbovu tunakuwa na akili za kmhdijeiehduhrrjrokuruheueu. Inatakiwa tule mlo mzuri wenye omega 3.
 
Ugali ni mtamu sana kutegemea unakula na mboga gani. Mchicha na samaki wa kukaanga, bamia na kuku wa kienyeji wa kuchoma au nyama ya kuchoma. Ugali na dagaa na mboga za majani au bamia. Ugali oyeeeee! Mie naula sana tena naupenda sili ugali for the sake ya kula ugali tu bali naufurahia sana. 😋😋😋
 
Sherehe haimaanishi Ubora, Sherehe mara nyingi ni utofauti wa siku baada ya siku...

Mimi kama kila siku nakula keki siku ya sherehe nikipiwa ugali itakuwa na maana kuliko kula hizo keki...

Pili ni urahisi wa kupata kitu kwahio mfano Kimchi ambayo imekaa mwaka mzima ikiletwa kwenye sherehe huenda ikawa bora kuliko chakula cha kupika kwa dakika au take away hata kama imecost pesa nyingi

Nikipeleka mihogo ya Kuchemsha kwenye Party huko Saskatchewan huenda nikawa a Star of the Party kila mtu kunifuata na kuonja...

Au kwenye Party ya Wabongo huko Russia nikatokea na Vitumbua vyangu na mabumunda na Kashata huenda kila party nikawa napewa kadi ili nisikose....
 
Wadau wenzangu wa JF & Watanzania wote

Naandika haya nikiongozwa kwa dhamira nzuri ya kueleza ukweli bila kuwa na nia ya kuwakera baadhi yenu

Sikusudii kupotosha, kukashfu, kudharau historia yetu, au makuzi yetu, au aina fulani ya chakula, kikundi fulani
kwenye jamii yetu n.k

Nazungumza chakula maarufu duniani kinachotokana na mahindi almaarufu Ugali

Nitazungumzia kwa ufupi kuhusu Ugali Chakula ambacho;

Kwa asili hakijawahi kuwa sehemu ya vyakula vinavyote gwa kwenye meza kuu ya Wafalme au Masultani!

Hakijawahi kuwa Maalumu au mahsusi kwa ajili ya wageni

Hakijawahi kuwa Maalumu au Mahsusi hata kwa ajili ya wagonjwa au walio na njaa kali

Ni chakula kinachohusishwa na Utwana au Utumwa au hali ya umasikini

Kimekosa ufahari mbele ya jamii hasa baada ya kukitumia

Kinahusishwa na udumavu wa maendeleo ya taaluma kwa wanaokitumia kwa muda mrefu tofauti na wanaotumia vyakula vinginevyo kama mpunga, ngano, shayiri, mtama, ulezi au hata ndizi n.k

Naomba kuwasilisha

Karibuni kwa mjadala

Aksanteni

Nakala: Paschal Mayala
hata aliyeandika amekula ugali tena wa mahindi tu;
katika kufikiria lazima ujue unasema ugali wa nafaka ipi,mfano mimi natumia ugali wenye ngano,ulezi,shayiri,ufuta,mtama kasoro mahindi ndio siweki,halafu anatokea mtu anapata wazo la kusema ugali tu;
ugali wa mahindi tena haya meupe haufai,ila ugali wenye nafaka zingine tule kwa furaha,hivi tumeshindwa kujua kuwa mkate ni advanced ugali?,
tule ugali;
 
Ugali ni mtamu sana kutegemea unakula na mboga gani. Mchicha na samaki wa kukaanga, bamia na kuku wa kienyeji wa kuchoma au nyama ya kuchoma. Ugali na dagaa na mboga za majani au bamia. Ugali oyeeeee! Mie naula sana tena naupenda sili ugali for the sake ya kula ugali tu bali naufurahia sana.
Uwe siku ukila huo ugali mchana basi Usiku kula vitu laini Ili huo ugali uyeyuke na uondoke kwenye ubongo wako.
 
Hivyo eh!? Ugali umenikuza mimi siyo kwamba nilikuwa sili vyakula vingine la hasha! Bali nilikuwa naufurahia hata usiku udogoni nimekula mara nyingi tu na hadi hii leo sioni shida kula ugali usiku.

Uwe siku ukila huo ugali mchana basi Usiku kula vitu laini Ili huo ugali uyeyuke na uondoke kwenye ubongo wako.
 
Back
Top Bottom