Dodoma: Rais Samia Afungua Mkutano wa Tisa wa Chama cha Makatibu Mahsusi (TAPSEA). Ahimiza Utunzaji Siri za Serikali, Maslahi na Fursa Kuzingatiwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais Samia akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Makatibu Mahsusi Jijini Dodoma.



ENG. ZENA AHMED SAID, KATIBU MKUU KIONGOZI – ZANZIBAR

Tunatambua umuhimu wa Makatibu Mahsusi, kwakweli wanafanya kazi za viongozi wao kuwa rahisi kwa jinsi wanavyowasaidia kazi. Sasa, ili waweze kufanya kazi hizo vizuri, wanatakiwa kujengewa uwezo na mafunzo haya ambayo wamepitia siku mbili, tatu hizi pamoja na mkutano huu – ni moja ya mambo ambayo yanajenga sana.

Nitoe wito serikalini na sekta binafsi muwe mnawapa fursa makatibu hawa mahsusi wawe wanajengewa uwezo.

Uongozi wa TAPSEA ulitushauri kule Zanzibar tuangalie uwezekano wa mafunzo ya Uhazili katika vyuo vyetu kule Zanzibar yawe yanafanywa yakiwa yanafanana na haya yanayotokea huku Bara.

Hilo ni jambo jema, tunalizingatia na tunalifanyia kazi. Umuhimu wake ni kwamba utatoa fursa kwa watu kutoka Zanzibar kuajiriwa Bara na wa Bara kuajiriwa Zanzibar bila kuwa na shida kwamba elimu aliyopata ni tofauti.

BI. ZUHURA SONGAMBELE MAGANGA, MWENYEKITI – TAPSEA

Mh. Rais, tumekuwa na tatizo la Waajiri kutokupanga bajeti za mafunzo kwa watumishi wa kada hii. Wizara ya Utumishi imetusaidia tukapata elimu ya Digrii lakini mwitikio naona ni mdogo kwa waajiri kutokutaka kuwapa elimu ya kutosha. Lakini tumekuwa tukilalamikiwa kuwa hatufanyi vizuri. Utafanyaje vizuri wakati hujawezeshwa kufanya vizuri?

Kwa heshima na taadhima Mh. Rais, tunaomba tuweze kupangiwa bajeti za mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi – hususani hii ya Digrii kwa wale wenye sifa ya kusoma. Wapangwe kwenda kusoma, Mh. Rais.

TAPSEA imepata kiwanja ambapo patajengwa makao makuu jijini Dodoma. Jengo hilo litaitwa TAPSEA Tower na litakuwa kitega uchumi cha chama.

TAPSEA inaiomba Serikali kukipandisha hadhi na kukijengea uwezo Chuo cha Uhazili Tabora kiwe chuo pekee cha Serikali kitakachoendesha mafunzo ya Uhazili katika ngazi zote.

- Umakini katika utunzaji wa taarifa na kumbukumbu za Serikali

Mojawapo ya majukumu makubwa ya Makatibu Mahsusi ni uutunza wa taarifa na siri Serikali. Eneo hilimlimekuwa na changamoto kwa Makatibu Mahsusi kwakuwa wanakuwa na fursa ya kupata taarifa hizo. TAPSEA inaiomba serikali kutoa mafunzo katika utunzaji wa taarifa na kumbukumbu za Serikali.

- Maslahi duni kwa Watumishi

Miongoni mwa changamoto zinazowakabili Makatibu Mahsusi katika kutimiza majukumu yao ya kila siku ni maslahi duni kwa watumishi wa kada hii, ikiwa ni pamoja na mishahara na maslahi funi yasiyoendana na kazi.

Pamoja na maslahi duni kumekuwa na kutowathamini Makatibu Mahsusi, kwa kupewa kazi ambazo ni nje ya majukumu yao, au kutopewa kazi kwa kutoaminika.

Makatibu Mahsusi kufanya kazi zaidi ya masaa ya kazi lakini ikifika malipo wanaambiwa hawastahili kwasababu wao ni “supporting staff”, hivyo hawastahili kupewa chochote.

Vilevile kwa baadhi ya waajiri kutowashirikisha Makatibu Mahsusi katika kazi za msingi ambazo zimo ndani ya weledi wao, kufanya kazi za nje zenye maslahi.

- Upendeleo wa Mabosi

Baadhi ya viongozi kupanga kazi kwa upendeleo, hasa kwa Makatibu Mahsusi ambao umri wao umesogea, huonekana hawana mvuto kwa baadhi ya ofisi.

Makatibu Mahsusi hawa ambao wanaonekana hawana mvuto wana uwezo mkubwa wa kazi. Hali hii hupunguza morali ya kufanya kazi na kusababisha miongoni mwa watumishi wa kada ya uhazili.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Nataka niwahakikishie kuwa Serikali inatambua mchango wa chama hiki kwani Makatibu Mahsusi wana majukumu muhimu zaidi ya kupiga chapa tu.

-Kada Muhimu

Huwa najiuliza, isingekuwa kada hii mabosi tungefanya nini? Muhtasari angechukuwa nani na miadi ya wageni angeshughulikia nani? Ninyi ni watu ni watu Mahsusi hasa.

- Weledi na Uadilifu

Nitumie furasa hii kuwashukuru na kuwasihi kuwa na weledi na waadilifu. Ukikosa uadilifu unakuwa umejitoa kwenye sifa ya kuwa Mahsusi na unakuwa Mpiga Chapa tu, na unapokosa weledi ni vilevile. Mmepewa jina Mahsusi kwa kazi maalumu mnazozifanya. Kwahiyo mhakikishe mnakuwa weledi na waadilifu.

Uadilifu ni kufanya kazi yako kwa wakati. Lakini uadilifu pia ni pamoja na kuweka siri za pale mahali ulipo – kuweka siri za bosi wako na pale mazingira ya kazi ulipo.

Siyo wewe tena umemuona bosi kaingiza king’asti hapo, kwanza unakitizama kwa jicho la kushoto pembeni alafu ukitoka “Leo, mmmmm!”

Ufanisi wa wakuu wa idara, vitengo na maeneo unaanzia kwenu. Mkisema Mama anaupiga mwingi, ni masekretari wangu wanaupiga mwingi. Isingekuwa wao ungepoteza taarifa, kazi n.k

- Wapandishwe Madaraja

Waziri wa Utumishi nendeni mkaangalie kama wamepandishwa madaraja. Na hivi muundo umekwishakamilika, nawaagiza mkahakikishe wanapanda madaraja yao na kama kuna areas zinalipwa ipasavyo.

- Chuo cha Tabora Kipandishwe Hadhi
Nimesikiliza hotuba ya Mwenyekiti kuhusu kutaka kituo cha Tabora kiwe kituo maalum kwa Makatibu Mahsusi, naliunganisha na ninakubaliana nalo. Chuo kile kimefanyiwa ukarabati, naomba kiwe chuo cha kisasa na kiwe chuo ambacho kitazalisha Makatibu Mahsusi ambao watakwenda kutumika Serikalini.

Lakini pia niliunganishe na lie alilosema Mwenyekiti kwamba Mahkatibu Mahsusi watakaozalishwa pale wakae ndani ya Wizara ya Utumishi na Utaewala Bora kama “pool” ya Makatibu Mahsusi wanaojengwa kwenda kuhudumia viongozi kwenye sekta mbalimbali.

Tukifanya hivyo tutakuwa na Makatibu Mahsusi tunaowajua sisi, amabao hapa wanaonekana hawana mvuto lakini kwa kazi ndiyo wenye mvuto.

Majibu mabovu na huduma hafifu zimeanzia hapa katikati ambapo vyuo hivi vilisambaratisha na vikabeba mambo mengine. Havikuzalisha Makatibu Mahsusi kama walivyotakiwa kuzalishwa. Sasa turudi, twende tukafanye hiyo kazi.

Kuna wakati mtu ana kicheti chake lakini ana mvuto mzuri, bosi ndiyo anamuajiri; “Huyu ndiyo Katibu wangu Mahsusi, mtu akiingia akute kuna kitu hapo…”, lakini kumbe kazi na maadili hakuna.

- Utunzaji Siri za Serikali

Ndugu zangu, ninyi mmeaminiwa kwa kiasi kikubwa. Umeaminiwa kinachopita pale ni chako na bosi wako, hatakiwi kujua mtu mwingine. Umeona la kufurahisha, bana. Umeona la kusikitisha, bana.

Kuna wakati unaletewa senti kidogo unatoa kopi nyaraka za serikali unaenda kuzitumia vinginevyo. Huko kwenye mitandao wanazipata wapi kama si nyie? Ni ninyi na watunza kumbukumbu.

Watunza kumbukumbu, semeshaneni. Mnayoyafanya hayafai hata kidogo. Unakuta barua iliyosainiwa ipo mtandaoni na imesainiwa na Katibu Mkuu.
 
Back
Top Bottom