Ufunguo wa seli ya Nelson Mandela katika gereza la kisiwa cha Robben warejeshwa Afrika Kusini-Waziri

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,339
Ufunguo wa seli ya gereza ya Kisiwa cha Robben alikofungwa Nelson Mandela utarudishwa Afrika Kusini badala ya kupigwa mnada nchini Marekani, waziri mmoja anasema.

Mnada huo ulikuwa ufanyike New York tarehe 28 Januari hadi Waziri wa Utamaduni wa Afrika Kusini Nathi Mthethwa alipopinga.

"Ufunguo huu ni wa watu wa Afrika Kusini," alisema.

Mandela alikaa jela miaka 27 kwa kufanya kampeni ya kukomesha utawala wa wazungu wachache.

Miaka kumi na minane kati ya hiyo ilikuwa kwenye Kisiwa cha Robben, kisiwa kilicho karibu na Cape Town.

Mnamo 1994, alikua rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini baada ya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo, na bado anabaki kuwa mwanasiasa wa kitaifa.

Bw Mthethwa alisema jumba la mnada la Guernsey lilikubali kurudisha ufunguo huo nchini Afrika Kusini na pia kusitisha uuzaji wa vitu vingine vilivyokuwa vya Mandela.

Hizi ni pamoja na mchoro asilia wa Mandela The Lighthouse, Robben Island, pamoja na baiskeli ya mazoezi aliyoruhusiwa kutumia na raketi ya tenisi gerezani

"Ufunguo unaashiria historia chungu ya Afrika Kusini huku pia ikiwakilisha ushindi wa roho ya mwanadamu dhidi ya uovu," Bw Mthethwa alisema katika taarifa.

ulikuwa umeuzwa na Christo Brand, mlinzi wa zamani wa jela ya Mandela katika jela hiyo yenye sifa mbaya. Wawili hao walikuwa marafiki wa karibu.

Mnada huo ulikuwa wa kuchangisha fedha kwa ajili ya bustani ya kumbukumbu na makumbusho karibu na eneo la maziko ya Mandela.

Mandela aliachiliwa kutoka gerezani mwaka wa 1990 wakati Afrika Kusini ilianza kuchana na ubaguzi mkali wa rangi (apartheid).

Alihudumu kwa muhula mmoja kama rais, akiondoka madarakani mnamo 1999.

Aliaga dunia mnamo 2013 akiwa na miaka 95.
 
Hao wazulu kichekesho kweli
Kichekesho chao ni kipi unaona ni sawa mali ya SA ikapigwe mnada USA watoto au vizazi vyao watakuja kujua nini huko baadae hii Nchi hata Twiga anapandishwa ndege mnaona sawa tuu siwashangai kabisa juzi kati nilikua Brantyre kuangalia bei ya petrol ipo sawa na Arusha Tanzania na wenzetu bei ni moja Nchi nzima hatafu tunawashangaa Wakhosa...
 
Hao wazulu kichekesho kweli
Kwani wazulu ndo waliosema wanataka funguo,? Na aliekwambia south Africa wanaishi wazulu peke yake mpaka uwaunganishe moja kwa moja kwenye hili nani?,,
Kwa taarifa yako hata huyo Mandela mwenyewe sio mzulu achilia mbali ramaphosa.
Wabongo wengi mnajua south Africa ni mzulu
 
South Africa Kuna makabila mengi Mandela alitokea kabila la Xhosa, Zuma ndiye Mzulu na Thabo Mbeki
 
Kwani wazulu ndo waliosema wanataka funguo,? Na aliekwambia south Africa wanaishi wazulu peke yake mpaka uwaunganishe moja kwa moja kwenye hili nani?,,
Kwa taarifa yako hata huyo Mandela mwenyewe sio mzulu achilia mbali ramaphosa.
Wabongo wengi mnajua south Africa ni mzulu
Zulu Ni kiwasilisho tu cha South Africa ndugu
 
Kichekesho chao ni kipi unaona ni sawa mali ya SA ikapigwe mnada USA watoto au vizazi vyao watakuja kujua nini huko baadae hii Nchi hata Twiga anapandishwa ndege mnaona sawa tuu siwashangai kabisa juzi kati nilikua Brantyre kuangalia bei ya petrol ipo sawa na Arusha Tanzania na wenzetu bei ni moja Nchi nzima hatafu tunawashangaa Wakhosa...
Mkuu Isanga natamanigi Sana nipate Dem wa kisauz umbo nane aliyejazia nikija huko nitawapataje? Tatizo hawapendi kuishi nje ya nchi yao hata ulaya hawataki. Nisaidie mkuu.
 
Mkuu ukija SA unaweza kumshawishi mmoja ukapanda nae Ulaya hawezi kukataa kama ukiwaambia tu twende Tanzania wanashukuru kweli ni vile hawana taarifa za Nje ila wakipata mtu wa kumueleza wanakubali tuu..Ukishuka CapeTown hapo water front wamejaa wakhosa na ni wazuri kuliko Wazulu namba nane ya ukweli sio ya kupaka rangi..
 
Ufunguo wa seli ya gereza ya Kisiwa cha Robben alikofungwa Nelson Mandela utarudishwa Afrika Kusini badala ya kupigwa mnada nchini Marekani, waziri mmoja anasema.

Mnada huo ulikuwa ufanyike New York tarehe 28 Januari hadi Waziri wa Utamaduni wa Afrika Kusini Nathi Mthethwa alipopinga.

"Ufunguo huu ni wa watu wa Afrika Kusini," alisema.

Mandela alikaa jela miaka 27 kwa kufanya kampeni ya kukomesha utawala wa wazungu wachache.

Miaka kumi na minane kati ya hiyo ilikuwa kwenye Kisiwa cha Robben, kisiwa kilicho karibu na Cape Town.

Mnamo 1994, alikua rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini baada ya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo, na bado anabaki kuwa mwanasiasa wa kitaifa.

Bw Mthethwa alisema jumba la mnada la Guernsey lilikubali kurudisha ufunguo huo nchini Afrika Kusini na pia kusitisha uuzaji wa vitu vingine vilivyokuwa vya Mandela.

Hizi ni pamoja na mchoro asilia wa Mandela The Lighthouse, Robben Island, pamoja na baiskeli ya mazoezi aliyoruhusiwa kutumia na raketi ya tenisi gerezani

"Ufunguo unaashiria historia chungu ya Afrika Kusini huku pia ikiwakilisha ushindi wa roho ya mwanadamu dhidi ya uovu," Bw Mthethwa alisema katika taarifa.

ulikuwa umeuzwa na Christo Brand, mlinzi wa zamani wa jela ya Mandela katika jela hiyo yenye sifa mbaya. Wawili hao walikuwa marafiki wa karibu.

Mnada huo ulikuwa wa kuchangisha fedha kwa ajili ya bustani ya kumbukumbu na makumbusho karibu na eneo la maziko ya Mandela.

Mandela aliachiliwa kutoka gerezani mwaka wa 1990 wakati Afrika Kusini ilianza kuchana na ubaguzi mkali wa rangi (apartheid).

Alihudumu kwa muhula mmoja kama rais, akiondoka madarakani mnamo 1999.

Aliaga dunia mnamo 2013 akiwa na miaka 95.
Africa kila kitu kinauzwa
 
Safi sana, tunamatumaini pia ipo siku funguo ya Jela alikowekwa Mbowe itatumzwa kama kumbukumbu kwa kizazi kijacho.
 
Back
Top Bottom