Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Jaribu kutumia jogoo la kisasa kwa hao kuku wa kienyeji. Kuhusu soko usiwe na shaka!
 
Mimi nafuga kuku na ninafanya crossing mwenyewe natumia majogoo ya kienyeji kwa kuku wa kisasa na sometime majogoo ya kisasa kwa kuku wa kienyeji.

Kwa ufupi ndugu yangu jogoo mmoja anatosha mitetea 7 tu na si zaidi na wala usidanganyike. Zaidi ya hapo jogoo huwa mjinga na huishiwa nguvu na kuku hudrop kutaga. nakushauri pia kama una umeme wa uhakika ununue incubator ndogo ya kutosha mayai 50 au 60 utotoe mwenyewe vifaranga kwa ni rahisi kuliko kuwekea kuku maya 10 anaangua mayai 5.
 
Mimi nafuga kuku na ninafanya crossing mwenyewe natumia majogoo ya kienyeji kwa kuku wa kisasa na sometime majogoo ya kisasa kwa kuku wa kienyeji. Kwa ufupi ndugu yangu jogoo mmoja anatosha mitetea 7 tu na si zaidi na wala usidanganyike. Zaidi ya hapo jogoo huwa mjinga na huishiwa nguvu na kuku hudrop kutaga. nakushauri pia kama una umeme wa uhakika ununue incubator ndogo ya kutosha mayai 50 au 60 utotoe mwenyewe vifaranga kwa ni rahisi kuliko kuwekea kuku maya 10 anaangua mayai 5.
Nilipata kusikia habari za incubator ndogo inayotumia mafuta ya taa,sasa sijui kama kuna mtu aliwahi kuiona Bongo au mpaka majuu,maana hiyo ingefaa sana field ambako umeme hauko.
 
[/COLOR]

Nilipata kusikia habari za incubator ndogo inayotumia mafuta ya taa,sasa sijui kama kuna mtu aliwahi kuiona Bongo au mpaka majuu,maana hiyo ingefaa sana field ambako umeme hauko.
Jaribu kutembelea SIDO huenda wanatengeneza!
 
Ivi ukiwa na incubator unaweza ukanunua mayai ya kienyeji sokoni ukayaweka umo au haitakiwi?
Na je, incubator inatumika kwa mayai yepi hasa. I mean ya kuku wa kisasa au kienyeji?
 
Nimecheka hadi basi,

Kuku wa mayai wa mabandani mara nyingi hawana jogoo. Kwa hiyo yai litakalowekwa ktk incubator ni lile ambalo jogoo na mtetea wameshirikiana kuunda yai husika.
 
Nimecheka hadi basi,

Kuku wa mayai wa mabandani mara nyingi hawana jogoo. Kwa hiyo yai litakalowekwa ktk incubator ni lile ambalo jogoo na mtetea wameshirikiana kuunda yai husika

Malila hivi hakuna kifaa cha kuweza kupima kama yai lina jogoo ili liweze kutotolewa kwa incubator?
 
Mimi nafuga kuku na ninafanya crossing mwenyewe natumia majogoo ya kienyeji kwa kuku wa kisasa na sometime majogoo ya kisasa kwa kuku wa kienyeji. Kwa ufupi ndugu yangu jogoo mmoja anatosha mitetea 7 tu na si zaidi na wala usidanganyike. Zaidi ya hapo jogoo huwa mjinga na huishiwa nguvu na kuku hudrop kutaga. nakushauri pia kama una umeme wa uhakika ununue incubator ndogo ya kutosha mayai 50 au 60 utotoe mwenyewe vifaranga kwa ni rahisi kuliko kuwekea kuku maya 10 anaangua mayai 5.

Incubator ya mayai 50 inapatikana wapi na kwa bei gani?
Je, kati ya mayai 50 yote yanaanguliwa au inaweza kuwa asilimia ngapi?
 
Malila hivi hakuna kifaa cha kuweza kupima kama yai lina jogoo ili liweze kutotolewa kwa incubator?

Hii ni sayansi iliyonipita kushoto. Ngoja tusubiri wadau waje. Kuna dogo ana incubator kapata toka America juzi, nitamdodosa. Ni vizuri kuweka mayai uliyo na uhakika kuwa ni mbegu bora bila kukisia.
 
Ivi ukiwa na incubator unaweza ukanunua mayai ya kienyeji sokoni ukayaweka umo au haitakiwi?
Na je incubator inatumika kwa mayai yepi hasa..i mean ya kuku wa kisasa au kienyeji?
Mayai ya kienyeji yanawekwa katika incubator, lakini yasizidi siku 14 toka yalipototolewa, hivyo inatakiwa uyapate kutoka katika source ya kuaminika. Muhimu ni kuwa mayai yawe yamerutubishwa na jogoo, na ndio maana mayai mengi ya kisasa hayaqualify kuwekwa kwenye incubator!!
 
Thanx Katavi. Je, una idea yoyote wapi incubator ndogo zinapatikana na kwa bei gani?
 
Nimecheka hadi basi,

Kuku wa mayai wa mabandani mara nyingi hawana jogoo. Kwa hiyo yai litakalowekwa ktk incubator ni lile ambalo jogoo na mtetea wameshirikiana kuunda yai husika !!!!!!!!.

Tehtehteh haya malila thanx kwa mchango wako
 
Habari wadau,

Naomba mnisaidie, nataka kuanza ufugaji mdogo wa kuku na nitaendelea kukua siku zinavyokwenda.
Nahitaji kuanza kufuga kuku waliochanganyika breed, wa kisasa na wa kienyeji

1. Wanaotaga wa kisasa ni vizuri kuchukua kuku wa umri gani kwa mbegu nzuri?
2. Jogoo mmoja anatosha kuku wangapi?
3. Kuna mahali wanauza vifaranga ambao tayari ni breed ya kisasa na kienyeji?
4. Soko la kuku waliochanganywa breed lipo au ni kama soko la kuku wengine?
5. Kama kuna mashamba ya mfano maeneo ya Dar au Yanayozunguka naomba mnifahamishe niweze kwenda kuona practically inavyokuwa.

Hata mimi nipo katika majaribio hayo, niliona kwa rafiki yangu yeye alichukua kuku wa nyama hawa wanaouzwa shs 3,000/- wa kisasa akaanza kuwafuga kienyeji. Kwa sasa kawa mswazi kabisa na mayai yake na vifaranga wana maumbile makubwa tofauti na wakienyeji.

Nimeanza majaribio haya na kuku wa kisasa wawili ambao nimewachanganya na wa kienyeji naona wanaanza kuzoea taratibu, wameanza hata kuokoteza wadudu
 
Wana JF

Mimi ni mfugaji; nimeanza kufuga kuku wa nyama (broiler) miezi michache iliyopita. Nimeamua kuanzisha thread hii ambayo lengo lake ni kubadilishana uzoefu katika ufugaji bora wa kuku.

Naamini hapa jamvini kutakuwa na wafugaji wenzangu pamoja na wataalamu wa mifugo; ambapo tutaweza kushirikiana na kusadiana katika kutatua changamoto mbalimbali katika sekta hii.

Ni matarajio yangu kwamba kupitia thread hii tutaweza kuwa na SHAMBA DARASA, kwani tunaweza kuleta changamoto tunazokutana nazo na kupata uzoefu wa wengine au ushauri wa kitaalamu katika kutatua tatizo.

Tarehe 27 Feb 2011 - nimeweka Kuku wa Nyama (broiler) 400 bandani. Niliweka maji yenye glucose kwa muda wa takribani masaa 4 pamoja na chakula (starter). Baada ya hayo masaa manne niliweka maji yenye dawa (Hipralona ENRO-S), kutokana na ushauri wa mtaalamu wa mifugo kwamba wakati mwingine vifaranga huanguliwa wakiwa na ugonjwa wa Salmonellosis. Ninaendelea na dawa hii mpaka leo (siku ya 3).

Kwa siku ya leo (siku ya 3), nimepoteza kifaranga kimoja na alikuwa na dalili za ugonjwa kama nilivyoonyesha katika picha hapo chini. Vifaranga wengine watano wana dalili za ugonjwa huo. Katika batch zilizopita nimekuwa nikiona vifaranga katika siku 5 za mwanzo wanakuwa na ugonjwa wenye dalili kama hizi na wakati mwingi kupoteza vifaranga vichache. Nimeamua kuleta hapa jamvini ili niweze kusaidiwa;
  • Je, huu ni ugonjwa gani?
  • Chanzo chake
  • Tiba au kinga yake
View attachment 24146View attachment 24147
Ni matumaini yangu kwamba wafugaji pamoja na wataalamu tuliopo hapa JF tutatoa ushirikiano katika kusaidiana kupunguza hasara ambazo zinaweza kuepukika kwa kupeana ujuzi na maarifa zaidi. Wakati mwingine upatikanaji wa mtaalamu wa mifugo huwa ni mgumu katika baadhi ya maeneo.

Nawakilisha
Ebenezer
 
Mimi niliingiza vifaranga wa mayai 2000, wana wiki ya tano sasa. Fasta tumia OTC plus - inatibu magonjwa mengi yanayotokana na Bacteria.

Fanya fasta utapoteza wengi.
 
Hakikisha banda ni kavu muda wote, ili bacteria wasizaliane humo ndani. Vifo chini ya 2% ni kawaida, kwa hiyo kupoteza vifaranga 14 kati ya 400 its ok.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom