Salathiel m.
Senior Member
- Mar 12, 2011
- 185
- 41
Daaah safi sn nami ntumie bro kwa email hii isayasalathiel@gmail.com
Naomba ushauri kuku wangu wanalalia zaidi ya watatu kweny kiota kimoja.
Haaaaa haaaaaa ka mie wana tabia hiyo hiyo ...embu nionyeshe viota vyako
chukua matofali nane za block,ziegamizie ukutani zipange chini4 na juu4,
kisha zile za juu zifunike na kipande cha ubao
utaona umepata vyiota vitatu,ndani ya hivyo viota weka mchanga kidogo na nyasi iwe mfano wa chungu,
gawa mayai yako kwa idadi sawa, mfano. kama yapo30 kila kuku atapata10, kisha tafuta kipande cha ubao kwa
ajili ya kuzuia kinakuwa kama mlango ktk kila kiota, kisha waweke kuku ktk hivyo vyumba, ukifika muda wa kula unawafungulia wanapata chakula kisha unawakamata na kuwaweka tena, fanya hivyo kwa siku saba tu, kisha kale kamlango huna tena haja ya kukaweka, kwa maana watakuwa umeshawacondition ktk viota vyao.
Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa
Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-
Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.
Habari yenu jf nimekuwa nikifuatilia tangu mwanzo na nimefurahishwa sana na kazi nzuri za Kubota na member wengine kwenye hii thread ila sasa nimeona nijitambulishe kwenu kama mtaalamu wa maswala ya mifugo hasa ufugaji wa ndege wafugwa na kuku.
lengo langu sio kukusanya mapato kwasasa ila kujaibu kuinua Tanzania yangu kwa uwezo wangu mdogo nilionao..nimeshangazwa sana na tarehe ya mwisho ya post hii ilikuwa 2013 ila natumai bado mtakuwepo.
tuendelee kuwasiliana.
mama timmy mimi si mgeni sana hapa jf.Huwa si comment chochote nachukuwa tu maujuzi.Ila nimeona nitoe mchango wangu kwa hili.Tafuta kinyesi cha ng'ombe cha tumboni (inabidi upate aliyechinjwa) jaza kinyesi kwenye mfuko wa rambo,funga mfuko vizuri,chimba shimo,fukia na uache kwa muda wa week 1 then fukua utakuta funza wakubwa sana. n.b. Nimeelekezwa sijajaribu.