Ndugu mtoa mada pongezi kwa mchanganuo mzuri wa biashara. Lakini naomba nikupe ushauri mdogo tu ya kwamba usithubutu hata siku mmoja kutoa mchango wako kwa kuanza kubeza kazi za wenzio.....kama ulivosema vitabu na dvd wanatoa story zao za utajiri.Inaonyesha hicho kitu bado unahitaji muda kukiangalia mara ya pili ukaelewa kwani mie ni mpezi wa kusoma hivyo vitabu na hizo dvd na maisha yangu kiukweli yanabadilika.Naomba nisisitize kwamba kama waandishi wengi wa vitabu vya mafanikio wanapoasisitiza IMANI ndio msingi mkuu,pigia vizuri mstari hilo neno manake ndio ukweli wa mafanikio..pia usitegemee miujiza bali jifunze imani gani na unaiapply vipi.

katika biashara yoyote changamoto zipo na unaweza kuzishinda kama sio mtu wa kukata tamaa...unachotakiwa kujua ni kwamba kwa kujua mbinu sahihi zaidi utaweza fanikiwa.Majanga(risk) zipo sana tu hazikwepeki la msingi unafanya nini kuzipunguza au unapokutana na changamoto unafanya nini? unatafuta jibu ama unaenda kupiga kelele mtaani waliniambia hivi mara vile mara sio hivyo.KILA KITU KINAWEZEKANA UAMINIPO NA KUTENDA YALE SAHIHI ILI UPATE MATOKEO MAZURI...BILA KUSAHAU BORESHA MBINU NA UELEWA WAKO KILA SIKU.
 
nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji,bado sija survey soko la kuku wa kienyeji likoje,
kama kuna mtu mwenye uzoefu na hili anishauri ,pros and cons etc.
bye the way nimeanza na Jogoo mmoja,ila natarajia kuongeza kuku within a week,
projections ni kuwa na kuku 1000,hapo ndio nianze kuuza,matarajio yangu ni kuuza via interent-hapa nalenga watu wa DAR,ambao wako bize,i can do delivery maofisini within city center,na baadae kuweka vituo vya kufanya pickup wakati watu wanarudi home jioni,e.g mwenge junction,morroco petrol station,etc,malipo via M-pesa,sms banking pia na mahoteli.
sitarajii faida ya haraka ,naomba ushauri kwa wale walifanya biashara hii,au wanajua mtu wa karibu aliyeifanya.

Newmzalendo, ka jogoo kamoja tu! ngoja nije nikachangamkie tukabanange tutajua mbele kwa mbele!! lol
 
Gazeti, kusema ukweli mradi wa kuku mzuri. ikama unataka kufuga kuku wa mayai wa kisasa inabidi uwe na mtaji wa uhakika, mimi nimeanza na 1000 (600 wana 2wiiki 12 na kuku 400 wana wiki 3 kwa sasa) laikni wananitoa jasho. kwa sasa kila wiki wanakula chakula cha 200,000/= ila wakianza kutaga si uongo. unaweza kupata angalau tray 25 kwa siku ambapo ukiuza 5500 unapata 137,500 na ukitoa matumizi unabaki na kama 70,000 kwa siku na hivyo kwa mwezi 2,100,000/= .ila kusema ukweli unahitaji sana kuwa makini na magonjwa na wizi
 
Watanzania tuliowengi tuna ideas nyingi sana za namna ya kujikwamua kiuchumi na kuishi maisha yenye neema na baraka tatizo ni kwamba kuna limitations nyingi sana zianazotuzuia kama vile

1.Ufahamu wa mambo
2.Mfumo mbaya wa sera za nchi yetu unaosababisha tatizo #3
3.Upatikanaji wa mtaji
4.Miundo mbinu mibovu yani namanisha kutoka Buguruni mpaka Tabata unatumia masaa mawili(wastage of time)
5.Ubinafsi wetu watanzania(tumeua siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo ndiyo pekee yenye manufaa kwetu)
6.Uvivu

Biashara ya kuku tena wakienyeji ni biashara nzuri inayoweza kuongeza pato binafsi na la taifa lakini ukianagalia wanaoifanya ni wachache nawanifanya bila tija ya kutosha kwasabau ya hizo limitations nilizozitaja hapo juu + uvivu

Nashauri kwa wenyefedha wekezeni kwenye biashara hii ni nzuri na mtasaidia kupunguza tatizo la njaa nchini nakuongeza thamani ya shilingi yetu dhidi ya dola ya marekani.

Hata wewe unayefikiri kuwa huna uwezo wa kufanya jambo lolote unaweza ukatafuta wenzako popote hata hapa mkaanzisha kampuni ya ufugaji kuku mkaenda mkaomba eneo popote ardhi bado nikubwa nchini sio lazima Dar tu pwani,morogoro na kwengine manaanzisha biashara hii mnaajiri watu wanfanya kazi kwajili yenu na kwajili ya wote baada ya muda lazima utoke .

Huu ni wakati wa kushikana mikono na kufanya mambo kwa pamoja (kama unaweza ku manage pake yako it is fine)tuiache serikali yetu iendelee kulipa madeni ya dowans na sisi tufanye kazi zetu wenyewe vinginevyo hali si nzuri,wakati serikali haidaiwi na rich mond hali ilikuwa mbaya sasa sijui wakati huu wa madeni.

Nafurahia JF coz nimahali tuna share ideas na kuzifanyia kazi wenzetu wa JE saccos wanakaribia kufikia tamati nzuri na ni kwa style hii hii tutakabiliana na matatizo ya uchumi chini

The discovery of agriculture was the first big step toward a civilized life.
Arthur Keith
 
Wana JF

Msaada wenu unahitajika katika hivi vitu viwili

1. Kuku wangu wa kienyeji nafugia ndani (siyo huria), wameanza kutaga ila mayai yao yanafanana sana na ya kuku wa kisasa wa mayai. Inaniletea tatizo kupata wateja wanahisi ni ya kisasa. tatizo lipo wapi?

2. Nitapata wapi mashine ndogo ya kutotolesha ya kutosha mayai kati ya 30 hadi mia?

Asanteni sana

Sijui hayo mayai yanafanana vipi, lakini mara nyingi hutofautiana kwa size na rangi, kwa maana ya kienyeji yanakuwa madogo (in average), na mchanganyiko ya brown na meupe, wakati ya kisasa yanakuwa makubwa na brown. Hata hivyo vigezo hivi sio mara zote vinaapply... Kwa kuwa wa kwako unawafungia, kuna uwezekano wakapata chakula cha kutosha na kuwa na mayai makubwa.

Kuna suala la rangi ya kiini, ambapo watu wengi wanadhani kuku wa kienyeji lazima atage yai lenye rangi ya njano, kumbe sio lazima bali inategemea kama kuku amekula majani mabichi (siku hizi kuna carotine zinauzwa madukani), yanayofanya kiini cha yai kiwe njano. Hata wa kisasa wakipewa majani au carotine kiini kinakuwa cha njano...
 
Tuko umenigusa, naomba uniambie products zenye vitamin majina yake nizitafute dukani, maana nataka kuku wangu wawe na kiini cha njano.... please please please!!
 
Nm mbona husemi kama jogoo wako anaendeleaje? Tupe updates ili tubadilishane uzoefu.

Mimi kwa sasa issue ni utitili, napambana nao vilivyo.
 
Ndugu mtoa mada pongezi kwa mchanganuo mzuri wa biashara. Lakini naomba nikupe ushauri mdogo tu ya kwamba usithubutu hata siku mmoja kutoa mchango wako kwa kuanza kubeza kazi za wenzio.....kama ulivosema vitabu na dvd wanatoa story zao za utajiri.Inaonyesha hicho kitu bado unahitaji muda kukiangalia mara ya pili ukaelewa kwani mie ni mpezi wa kusoma hivyo vitabu na hizo dvd na maisha yangu kiukweli yanabadilika.Naomba nisisitize kwamba kama waandishi wengi wa vitabu vya mafanikio wanapoasisitiza IMANI ndio msingi mkuu,pigia vizuri mstari hilo neno manake ndio ukweli wa mafanikio..pia usitegemee miujiza bali jifunze imani gani na unaiapply vipi.

katika biashara yoyote changamoto zipo na unaweza kuzishinda kama sio mtu wa kukata tamaa...unachotakiwa kujua ni kwamba kwa kujua mbinu sahihi zaidi utaweza fanikiwa.Majanga(risk) zipo sana tu hazikwepeki la msingi unafanya nini kuzipunguza au unapokutana na changamoto unafanya nini? unatafuta jibu ama unaenda kupiga kelele mtaani waliniambia hivi mara vile mara sio hivyo.KILA KITU KINAWEZEKANA UAMINIPO NA KUTENDA YALE SAHIHI ILI UPATE MATOKEO MAZURI...BILA KUSAHAU BORESHA MBINU NA UELEWA WAKO KILA SIKU.
Nimekuelewa mkuu!
 
Gazeti, kusema ukweli mradi wa kuku mzuri. ikama unataka kufuga kuku wa mayai wa kisasa inabidi uwe na mtaji wa uhakika, mimi nimeanza na 1000 (600 wana 2wiiki 12 na kuku 400 wana wiki 3 kwa sasa) laikni wananitoa jasho. kwa sasa kila wiki wanakula chakula cha 200,000/= ila wakianza kutaga si uongo. unaweza kupata angalau tray 25 kwa siku ambapo ukiuza 5500 unapata 137,500 na ukitoa matumizi unabaki na kama 70,000 kwa siku na hivyo kwa mwezi 2,100,000/= .ila kusema ukweli unahitaji sana kuwa makini na magonjwa na wizi
Niliachana kidogo na kuku nimkaingia kwenye kilimo bt nitarudi tena siku si nyingi!
 
Watanzania tuliowengi tuna ideas nyingi sana za namna ya kujikwamua kiuchumi na kuishi maisha yenye neema na baraka tatizo ni kwamba kuna limitations nyingi sana zianazotuzuia kama vile

1.Ufahamu wa mambo
2.Mfumo mbaya wa sera za nchi yetu unaosababisha tatizo #3
3.Upatikanaji wa mtaji
4.Miundo mbinu mibovu yani namanisha kutoka Buguruni mpaka Tabata unatumia masaa mawili(wastage of time)
5.Ubinafsi wetu watanzania(tumeua siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo ndiyo pekee yenye manufaa kwetu)
6.Uvivu
The discovery of agriculture was the first big step toward a civilized life.
Arthur Keith
Hapo kwenye red umenikuna mkuu, nimejaribu kilimo nikapata
mnunuzi mzuri lakini bado nimewekewa (Tumewekewa) masharti
ya wapi kwa kuuza, yaani tunachaguliwa mnunuzi huu ndo ukatili
unaonifanya nichukie kilimo.................... Eti kilimo kwanza.....mara
mtoto wa nkulima..........!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! UNAFIKI!
 
Ndugu zangu,kale kajogo,kalikuja kuwa LIJOGOO na very unfortunately kwake Familia yangu ilipiga VETO aliwe na kuwa Nyama.sometimes i feel guilty kila nikisoma hii Thread.kwani yule kuku alitakiwa kuwa Symbol ya JF.

-------
Tofauti ya kuku wa Kienyeji na wa nyama huwa tunadevelope emotional attachment na hawa kuku kwani ukipepeta nyungo tu wanakuja,na pia huwa wanajenga bonds na mtu anayewalisha.
tofauti sana na broilers wao ni mazuzu ata kuwauza na kuwala huwa unafikiria Gharama za kuwaclear fasta fasta upate pesa. ndio maana nilishawahi kusema kuku wa kienyeji ni personal consuption.though unaweza fuga kwa kuwauza
 
Je utarudia ufugaji wa kuku wa kienyeji au ndo kwishney?
 
Mkuu nimeipenda sana topic yako,imekaa vizuri ila kwa nyongeza zaidi ya jinsi ya kua tajiri,tungeanza msingi wa matayarisho kiakili,jinsi gani mabadiliko ya kimaisha yasiathiri shughuli zako,ila mi naamini utulivu wa akili ndio mwanzo wa safari ya utajiri,
 
Dah hii ndo imenileta JF maana nimeanza kuiona kwenye Blog fulani
lakini yule mtu kawa muungwana kasema wazi kuwa huku ndiko
alikoitoa. Ahsante sana mkuu mchango umeenda shule!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom