Ufisadi wa Nyumba za Serikali

FM.... Well put Sir!!! Nimekuwa nikifuatilia sana hii issue ya nyumba with interest kwa vile nami nilikuwa kati ya wale wachache ambao tungependa kudaka walau kamoja especially zile za kule Chang'ombe lakini bahati mbaya sikuwa mfanyakazi serikalini na wala sikuwa naishi katika nyumba hizo so sikuwa na langu....

Bahati mbaya ni kwamba wakati nilikuwa najipitisha pale Ujenzi kama ninaweza sikia ka"dili" hakuna aliyewahi kuiweka dhana hii as open and clear as you have in your many and other contributors (Viva JF) na sasa nimeelewa considering the fact kwamba:
"Wengi walionunua nyumba hizo ni wafanyakazi wa serikali ambao walikuwa wanaishi ndani"

Lakini pamoja na kukubali kwamba it was a well made and justifiable decission at the time (which I support fully na sasa nina Peace of mind... for NOW) still kuna mambo ambayo kwa kweli nadhani kulikuwa na utata katika zoezi hili ambapo wengi wameliweka wazi katika thread hii ukiwemo:

1. Kuna nyumba ambazo kimantiki hazikutakiwa kuuzwa kutokana na location yake - nyumba za wakuu wa vituo vya Polisi na nyingine zilizo katika maeneo nyeti

2. Uamuzi wa Serikali kuuza nyumba zile na kisha kujenga nyumba (maghorofa) maeneo ya Masaki na Victoria kwa ajili ya Mawaziri na Manaibu Waziri - hili kidogo nalilinganisha na uamuzi wa kuuza nyumba na kupanga GESTI..... Look at it katika mtizamo wa "Rehabilitate for the Ministers and D.Ministers vs Acquiring plots na kujenga nyumba mpya"

3. Kuhusu uuzwaji wa nyumba za Makatibu Wakuu.... Hili ni gumu sababu PS ni mtu ambaye ni Civil Servant na sasa kama hawa wa sasa tunawajali (wengi wao wapo kwenye their ripe years ......more than 55yrs) sasa hawa wakienda manake itabidi tena tujenge kijiji chao sijui Mbezi kama mawaziri na deputies au tutaamua kuwaacha wakae kule vikindu wanapoishi sasa!!

Wakuu, hizi ni my "Two Cents" on the matter and narudia kusema kwamba sasa nimepata kwamwanga kwenye sakata zima la hizi nyumba!!!

Naomba kuwakilisha................
 
Na juu ya hayo nadhani sasa Serikali ianze kufikiria kujenga nyumba za Makatibu Wakuu na Wakurugenzi kwenye vijiji teule kule Dodoma manake ndio tulipoambiwa (so were told and still dream) kwamba ndio yatakuwa Makao makuu ya Serikali.............

The need for further housing for Govt chaps and offices should be planned to be done with a focus on "USTAWISHAJI MAKAO MAKUU - DODOM" na ndiyo iwe chalenge ya Serikali ya Awmu ya 4 kumaliza mzozo huu na tatizo la Serikali kuu, Biashara na kila kitu kuwa Dar es Salaam.... Makao Makuu Dodoma itasaidia hata kufungua mikoa ya Mangaribi ya Tanzania kwa haraka kuliko sasa kila kitu Dar na kwingine kunabaki abunuwasi.............
 
Nia ilikuwa nzuri lakini kama wanavyosema wahenga ni safari ndefu kati ya mkono na mdomo. Makosa yalitendeka na ndiyo maana tukafika hapo tulipo. Kuna wengine walionewa, kuna wengine walipendelewa n.k. Haya yote yalitokea kwa sababu mpango mzima wa kuuza haukuandaliwa vyema na kikamilifu zaidi. Pengine yangeweza kuepukwa kama pangekuwa na uwazi zaidi. Kwa bahati mbaya hiyo sio hulka yetu.
 
Nia ilikuwa nzuri lakini kama wanavyosema wahenga ni safari ndefu kati ya mkono na mdomo. Makosa yalitendeka na ndiyo maana tukafika hapo tulipo. Kuna wengine walionewa, kuna wengine walipendelewa n.k. Haya yote yalitokea kwa sababu mpango mzima wa kuuza haukuandaliwa vyema na kikamilifu zaidi. Pengine yangeweza kuepukwa kama pangekuwa na uwazi zaidi. Kwa bahati mbaya hiyo sio hulka yetu.

FM,
Hata hiyo nia nayo inaweza onekana kwa nje tu ikiwa nzuri, lakini unapoingalia kwa ujumla, haionekani hata kidogo kama kweli hiyo nia nzuri ilikuwapo, zaidi ya matumizi mabaya ya madaraka kujinufaisha na mali ya umma. Kwa mfano mimi sijaelewa haya yafuatayo;

  1. Ni ipi ilikuwa nia ya serikali kuuza nyumba maana mpaka hivi sasa nasikia sababu mlukuki, kuanzia ya kupunguza gharama za uendeshaji mpaka wale wanaosema kuwa baadhi ya watumishi ilibidi wazawadiwe kwa vile walikuwa hawana pa kwenda?
  2. Serikali ilikuwa inategemea kufaidika vipi na huo mradi?
  3. Nani aliyeanzisha hili wazo na ni nani aliyeamua litekelezwe?
  4. Taratibu za uuzaji/ umiliki wa mali ya umma ulifuatwa? Sheria yetu inasemaje katika hili?
  5. Kama kuna makosa yaliyofanyika, kwa nini zoezi zima au sehemu ya hilo zoezi isifutwe hata kama itabidi iwe kwa kupitisha sheria mpya bungeni?
  6. Je, serikali imepoteza mapato kiasi gani au imefaidika kwa kiasi gani na hili zoezi?
Yapo maswali mengi mengine ambayo kwa kweli hayawezi kuisha kwa vile tu serikali imefunga macho.
 
1. Wote wanaotetea hizi nyumba kuuzwa kwa vigogo utaona ni watoto wa vigogo au ni vigogo wenyewe kwa hiyo wanatetea maslahi yao au wazazi wao au wamefaidika kwa huu uporaji!

2. Ni kama kule Zimbabwe % kubwa ya yale mashamba yalichukuliwa na mawaziri, makatibu wakuu..eti Mugabe aliwatetea kuwa nao waliporwa ardhi na wakoloni in 1880s! Au Kenya baada ya uhuru akina Kibaki walipora ardhi ya karibu Province na sasa ni mali ya mtu mmoja! Je huu zii wizi??

3. Haya yasipokemewa na uporaji wa mali ya umma unaachia wachukue vigogo wachache.. ndo haya sasa unaona yanayotoekea Kenya!

4. Hakuna cha sheria ya Bunge.. ni Bunge hili hili tumeona wamejipitishia sheria zinazomkamdamiza mtu wa kawaida kwa wingi wa CCM. Je mnakumbuka pia Bunge la Kenya hapa nyuma walipitisha sheria kila mbunge alipwe Shilingi 100 milioni kama ahsante kila baada ya miaka 5? Kwani sheria kupitishwa na Bunge ina ashiria nini? Wabunge wengi sii tunawaona ktk luninga wakiwa wamelala Bungeni?

Au kwa nini kule Mlimani au SUA au MU Wale Maprofesa wasiuziwe zile nyumba? Kwani wao sii watumishi wa serikali pia?

Nona Kila mtu anajali zaidi maslahi yake!

Kupiga kelele kupinga uporaji ni muhimu!!!
 
Haya na tuongee kisomi ingawa mimi huko simo. Mkuu naona unaishi Marekani. Je huko serikali inatoa huduma hii kwa wafanyakazi wake wote? Condoleeza anakaa katika nyumba ya serikali? Au uingereza? Brown kabla hajaukwaa uPM alikuwa anaishi katika nyumba ya serikali? Au Afrika kusini? Au nchi yeyote iliyoendelea? Wafanyakazi wa serkali wanapewa nyumba za kuishi bure na serikali kuu?

FM,
Nafikiri sio kila jambo linatuhitaji tujilinganishe na US, UK au nchi nyingine zilizoendelea. Mazingira ya miundo mbinu ya nchini kwetu pamoja na mishahara ya wafanyakazi wetu ni tofauti sana nchi ulizotumia kama mifano. Kwa hiyo utendaji wetu, tokea enzi za mkoloni ulikuwa tofauti hata ukilinganisha na wa wale waliokuwa wanatutawala.


Suala la kutoa huduma hii halikuwa sustainable kwa jinsi lilivyokuwa likifanyika. In the long run huduma hii inatakiwa itolewe na soko la nyumba. Mfanyakazi alipwe vizuri na sokoni pawe na nyumba za kutosha zinazokidhi mahitaji yake kwa bei atakayomudu. Kwa sasa hivi hapa kwetu hilo soko halipo. Mahitaji yamezidi mno production kiasi cha kuwafanya wenye nyumba hizo kutoza pango wanavyotaka.

Sustainability ni suala la planning iwe ni huduma au biashara. Tukiplani vizuri hakuna linaloshindikana, hasa wakati huu ambao tuna wasomi wengi na kama mambo yataendeshwa kiuwazi. Kwa mfano, kwa nini hizo nyumba za serikali zisiwe chini ya kampuni binafsi kuziendesha kibiashara kama NHC? Maana kama ulivyosema, sidhani kama huko sokoni kwenye kila mji/kituo cha kazi TZ atakachohamia mtumishi wa serikali kuna nyumba za kupanga anazoweza kutumia.

Pia unasema kuwa mfanyakazi anatakiwa alipwe vizuri ili alipe kodi at market value, Je hili limefanyika tokea zilipouzwa hizo nyumba?


Serikali kwa muda mrefu ilikuwa haitoi fungu kwa ajili ya kuzikarabati wakati pango lilikuwa pegged kwenye mshahara wa mkazi. Mshahara wa wengi waliokuwa kwenye nyumba hizo ulikuwa kati ya 100,000 na 200,000. Hawa walikuwa wanalipa asilimia 10 ya mshahara kama pango hivyo kufanya pango kwa mwezi kuwa sh 10,000 hadi 20000. Hii pango ilikuwa haitoshi hata kunua kitasa na ilikuwa chini ya pango la chumba Mwananyamala chenye umeme! Serikali kwa hiyo ilitakiwa aidha iamue kusubsidise huduma kwenye nyumba hizi ( kitu ambacho katika soko hilo la huria halikubaliwi), kuongeza mshahara wafanyakazi wake wanaoishi katika nyumba hizo ili pango liwe linaloendana na mahitaji halisi ya uendeshaji, kupangisha nyumba hizo kwa wakaaji wake kwa market rates, kuziuza n.k. Uamuzi uliochukuliwa ni huo wa kuziuza. Taratibu za uuzaji wa mali ya serikali unasema mali hiyo itauzwa kwa mnada. Hivi hizo nnyumba zingeuzwa kwa mnada wamatengo wangapi wangeona ndani? Tukumbuke hatuzungumzii za Masaki tu bali hata zile za Chang'ombe! Matokeo yangekuwa kuwa nyumba hizi zimenunuliwa na wafanyabiashara na tukiwa zaidi, wafanyabiashara ambao wengi wao wangekuwa ni wahindi, waarabu au makaburu tungesema nini?

Nafikiri hapa unajichangaya, upande mmoja unaunga mkono soko huria, upande mwingine hutaki soko huria kutumika kuuza nyumba, wapi kwa wapi....

Lakini mchanganyo wako mkubwa ni pale unaposema kuwa nyumba ziuzwe kwa vile mishahara ya wanaokaa ndani yake ni midogo kulipia kodi at market rate, sasa sijui una-solve nini hapa. Kama mishahara haiwezi ongezwa kufikia hali ya soko kwa nini basi nyumba ziuzwe? Cha kushangaza ni kuwa wanunuzi ni hao hao tunaosema kuwa hawawezi kulipa kodi? Kweli wanajua kutuchezea....


Huyo atakayeamua ku'nationalize' hizi nyumba tena itakuwa uamuzi wake na bila shaka atafanya hivyo baada ya kujiridhisha kuwa ni uamuzi utakaoangalia maslahi ya taifa letu. tulitaifisha nyumba kibao, tukaanzisha Msajili wa Nyumba, zikatushinda kuzihudumia hadi hapa tulipo ambapo tunazirudisha tena katika soko huria.

Nafikiri nyumba sio tu kuwa ziliuzwa kinyume cha sheria, bali pia zimeliingiza taifa hasara kubwa. Ushauri wangu kwa JK ni kwa serikali kuzirudisha nyumba zake mikononi mwake na kuunda kampuni ya kusimamia upangishwaji wake kwa watumishi wa uma, at a market rate subsidised by the govt.
 
Katika sera za soko huria ambzo tunazo bongo sasa hiv, serikali huwa haimiliki nyumba, ila inakusanya kodi kutoka kwenye nyumba n property, uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ulipitishwa na bunge hilo hilo kwa kushinikizwa na IMF na World Bank, under Mkapa,

Kwenye zoezi hilo, taifa letu limewanusuru viongozi wetu wasafi na waovu kuanzia kina Sozigwa mpaka kina Makani, ambao hawakuiba wakiwa madarakani, the ishu ni kuwa kuna waliouziwa ambao hawastaili, lakini sio otherwise, bila ya hili zoezi kina familia ya marehemu Mnauye, ambaye hakuiba hata senti tano ingeishi wapi?

Field Marshall,
Sina hakika na kina Nnauye, lakini Mzee Sozigwa nina hakika anakaa kwenye nyumba yake mwenyewe pale Kurasini ambayo aliijenga miaka ya 1970. Hivyo kimsingi hakuwa mmoja wa waadilifu ambao wamefaidishwa binafsi na ufisadi wa nyumba hizo za serikali.
 
Mimi nashindwa kuelewa kitu kimoja mtu kama aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM Mangu'la aliuziwa hizo nyumba kwa vigezo gani ? Mimi nadhani ingekuwa bora kama hizo wangepewa NHC ili wazirekebishe halafu wapangishwe watu wa serikali !
 
Mimi nashindwa kuelewa kitu kimoja mtu kama aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM Mangu'la aliuziwa hizo nyumba kwa vigezo gani ? Mimi nadhani ingekuwa bora kama hizo wangepewa NHC ili wazirekebishe halafu wapangishwe watu wa serikali !

Rufiji,
Mangula nyumba hakupewa yeye kwa kuwa yeye alikuwa ni mtumishi wa Chama. Nyumba aliuziwa marehemu mkewe ambaye alikuwa ni mtumishi wa serikali katika wadhifa wa ualimu wa shule ya msingi...
 
Mafuchila ,

Nashukuru sana kwa jibu lako, Kweli ukishangaa ya Musa utaona ya ....
 
Baada ya serikali kuuza nyumba kwa nini bado inawagharimia watumishi wake kuishi hotelini?

Mimi nilidhani nyumba za serikali zimeuzwa ili kila mtumishi wa serikali ajiju?
unapewa mshahara wako jua wapi utaishi, uwe waziri au katibu wa wizara ni lazima ujiju.

Huu ni wenda wazimu mkubwa kusema serikali za dunia hazihodhi nyumba wakati huohuo sisi bado tunaendelea kulipia gharama za nyumba za watumishi wa serikali?

Haya tena kuna mradi mkubwa wa nyumba zaserikali ulianzishwa mara baada ya kuuza nyumba za serikali. Sasa usemi kwamba serikali haihodhi nyumba ni wa kweli aua MH Field Marshal unatetea policy yenye kila aina ya ukinyonga?
 
FM,
Nafikiri sio kila jambo linatuhitaji tujilinganishe na US, UK au nchi nyingine zilizoendelea. Mazingira ya miundo mbinu ya nchini kwetu pamoja na mishahara ya wafanyakazi wetu ni tofauti sana nchi ulizotumia kama mifano. Kwa hiyo utendaji wetu, tokea enzi za mkoloni ulikuwa tofauti hata ukilinganisha na wa wale waliokuwa wanatutawala.


Nakubali kuwa mazingira yetu ni tofauti na hizo nchi. Lakini swali langu lilikuwa kwenye milki ya nyumba na si kuwa tuwaige. Bin maryam ameeleza vizuri zaidi yangu kwa nini mfumo wa kuwapa nyumba wafanyakazi ulikuwepo tangu wakati wa wakoloni. Cha muhimu ni kuangalia kwa nini wamejitoa kwenye kutoa huduma hii na kuona kama kuna tunachoweza kujifunza kutoka kwao.



Sustainability ni suala la planning iwe ni huduma au biashara. Tukiplani vizuri hakuna linaloshindikana, hasa wakati huu ambao tuna wasomi wengi na kama mambo yataendeshwa kiuwazi. Kwa mfano, kwa nini hizo nyumba za serikali zisiwe chini ya kampuni binafsi kuziendesha kibiashara kama NHC? Maana kama ulivyosema, sidhani kama huko sokoni kwenye kila mji/kituo cha kazi TZ atakachohamia mtumishi wa serikali kuna nyumba za kupanga anazoweza kutumia.

Pia unasema kuwa mfanyakazi anatakiwa alipwe vizuri ili alipe kodi at market value, Je hili limefanyika tokea zilipouzwa hizo nyumba?


NHC ndiyo mfano mzuri wa shirika kujiendesha kibiashara? Huko nako matatizo si yale yale? Tulibinafsisha nyumba zilizokuwa na bei zaidi ya sh laki moja miaka ya sabini, tukaanzisha chombo kinachoitwa msajili wa Majumba, zikatushinda. Leo unamuona NHC ndiyo mkombozi? Planning, Mkuu, has never been our strong point. Hatuna patience.

Nilisema moja ya njia za kuwezesha serikali kuhudumia hizo ilikuwa ni serikali iongeze mishahara hadi level ambayo mtumishi ataweza kulipa kodi iliyo katika market value. Hii haikufanyika kwa sababu serikali iliona haitaweza kubeba mzigo huo mara moja. Alternative nyingine ilikuwa ni serikali ilipie moja kwa moja huduma hizo bila kuangalia makato ya watumishi. Hii nayo ilionekana haifai maana neno subsidy limekuwa anathema kwetu.




Nafikiri hapa unajichangaya, upande mmoja unaunga mkono soko huria, upande mwingine hutaki soko huria kutumika kuuza nyumba, wapi kwa wapi....

Lakini mchanganyo wako mkubwa ni pale unaposema kuwa nyumba ziuzwe kwa vile mishahara ya wanaokaa ndani yake ni midogo kulipia kodi at market rate, sasa sijui una-solve nini hapa. Kama mishahara haiwezi ongezwa kufikia hali ya soko kwa nini basi nyumba ziuzwe? Cha kushangaza ni kuwa wanunuzi ni hao hao tunaosema kuwa hawawezi kulipa kodi? Kweli wanajua kutuchezea....


Unayejichanganya ni wewe mwenyewe Mkuu. Hakuna mahalli niliposema naunga soko huria au la. Nimejaribu kuweka pros and cons za suala lote na watu kama nyinyi ndiyo muamue kipi kingekuwa bora zaidi. Kuwauzia wafanyakazi wa serikali kwa controlled process ( bei iliyo chini ya market value, sheria za kutoziuza tena n.k.) au kuziweka kwenye soko huria ili wenye uwezo wazinunue kadri wanavyotaka. Serikali inaelekea iliona njia ya kwanza ni afueni sasa wewe ni haki yako kupinga na kusema kwamba hayo niliyoainisha si kweli. Pengine unawajua waswahili kibao wana uwezo wa kushindana katika mnada na kununua hizo nyumba! Nenda kahudhurie hiyo minada ya serikali ( wanakouza samani, magari n.k) halafu utuambie kama nako haki kweli inatendeka. Tukumbuke kuwa nyumba tunazozingumzia ni pamoja na zile za Chang'ombe.

Serikali ina limit cha kiasi ambacho kinaweza kunkata mtumishi kama pango. Haiwezi ikasema, kwa mfano, kuwa wafanyakazi wanaokaa kwenye nyumba ya serikali watakatwa asilimia 80 ya mshahara wao kama pango. Hii haiwezekani hata kama mtumishi huyo ana miradi yake na anaweza kuishi bila mshahara. Vile vile ukumbuke si watumishi wote wenye miradi yenye kuwawezesha kuishi bila kujali mshahara. Kilichoonekana ni lesser evil ni kumuizia nyumba kwa bei nafuu ambayo ataweza kulipa kwa namna anavyojua. Kwa sababu malipo haya si lazima yatoke kwenye mshahara wake kama ilivyokuwa pango la nyumba. Naamini kuwa pamoja na hii, kuna walioshindwa. Sasa wapi nimejichanganya?



Nafikiri nyumba sio tu kuwa ziliuzwa kinyume cha sheria, bali pia zimeliingiza taifa hasara kubwa. Ushauri wangu kwa JK ni kwa serikali kuzirudisha nyumba zake mikononi mwake na kuunda kampuni ya kusimamia upangishwaji wake kwa watumishi wa uma, at a market rate subsidised by the govt.

Kwa nini aunde kampuni nyingine wakati National Housing ipo? Na nani atakayetoa hiyo subsidy? Ukumbuke kuwa sio kila mfanya kazi wa serikali aliyestahili alikuwa na nyumba. Hata wakati huo, wengi tu walikuwa wakiishi mahotelini. Dawa ni badala ya kugombea hiki kidogo tulichoshindwa kukiendeleza, serikali ingefanya jitihada za kuweka mazingira ambamo watu binafsi, makampuni binafsi na vyombo vya umma vitaweza kujenga nyumba nyingi kwa ajili ya kupanga au kuuza.

Wakati umefika ambapo makazi bora iwe ni haki ya KILA mtanzania na si wafanyakazi wa serikali tu.
 
kwa hotuba ya Mkapa wakati akiwaaga? Nimeishakuambia angalia unalozungumzia. Una base yote hii kutoka[/B
]

Mkuu acha utoto, baada ya Muungwana kuchagulia kuwa mgombea, alikwenda NY kuwaaga wabongo na kushirki kwa mara ya mwisho GA, akfanya mkutano nao hotelini Hermseley, akaulizwa hii ishu na kujibu kuwa pamoja na kushauriwa na IMF, na WB, pamoja, alisema wazi tena kwa kiburi kuwa " mimi ndiye niliyeamua, mwenye tatizo anilaumu mimi..., huku akimuangalia Kikwete, akasema kuwa nasikia rais mpya ana mpango wa kuzirudisha, "..namtakia good luck...", whether unakubali au hutaki haibadili anything mkuu, hii ni fact!

Bila shaka nae uko karibu nae.

Off course mimi CCM damu nitakosaje kuwa karibu na mwenyekiti wangu, vipi huko upande wa pili mko mbali na viongozi wenu nini?

Wanasiasa wanatumia IMF na World Bank kama bogey figures pale wanapobanwa.

Mkapa alisema yeye ndiye ameamua, and I believe him, na alisema tena kwa jeuri mweye tatizo amlaumu yeye.

Kushauriwa na bunge imekuwa lini sawa na kupitishwa na bunge?

bunge lingekuwa halitaki lingesema, kama lilivyomsema na kumkimbiza Lowassa. Llilikubali ndio maana Mkapa, akaipitisha.

Nimekuuliza kuhusu hayo maghorofa ya Tabata, bei ya nyumba Obei umeshindwa kujibu. Kama haujui, nyamaza tuu, There is no shame in it.

Wewe ndio unyamaze maana unaonyesha kwa maneno yako kuwa ni huelewi kitu, nina marafiki kibao wamenunua nyumba Tabata, tena ilifikia mahali Magufuli mwenyewe ndiye aliyekuwa anaidhinisha kuuzwa, kwa mkuu tafuta facts kabla ya kurukia hapa utaaibika mkuu!
 
Wewe ndio unyamaze maana unaonyesha kwa maneno yako kuwa ni huelewi kitu, nina marafiki kibao wamenunua nyumba Tabata, tena ilifikia mahali Magufuli mwenyewe ndiye aliyekuwa anaidhinisha kuuzwa, kwa mkuu tafuta facts kabla ya kurukia hapa utaaibika mkuu!

Lord have mercy. Kwanza unasema Mkapa alilazimishwa na IMF na wengine halafu unasema alichosema ni kuwa pamoja na kushauriwa nao lakini uamuzi ulikuwa wake! Halafu unasema bunge lilipitisha halafu unasema kama walikuwa hawakubaliani kwa nini hawakupinga. Halafu unasema kuwa serikali iliuza nyumba zake kwenye maghorofa ya Tabata wakati serikali kuu haikuwahi kuwa na maghorofa ya Tabata. Unadai kuwa Maghufuli aliidhinisha nyumba baada ya marafiki zako kibao kuuziwa Tabata. Unajua kweli utaratibu uliotumika kuuza nyumba, ndugu yangu? Facts gani, ndugu yangu, wakati hata kuliko nyumba za serikali kuu haujui? Haujui hata bei za nyumba za Obei halafu unasema una facts?

Unajua, Mkuu,your ignorance shows. Unataka sana kuonekana unajua kila kitu kiasi cha kujichanganya mwenyewe. FYI you are not omniscient. Una delusions of grandeur, kuanzia uchaguzi wa jina, insistence kuwa ulikuwa baharia MSOMI mpaka your persistent name dropping. Wewe ni mtu unaependa kuzengea kwenye orbit za hao unaoona ni your betters halafu kuja hapa na ku'brag' kuhusu your closeness to them. Usichoelewa ni kuwa kwa watu makini yote haya hayakujengei kitu.Kwa vile hatukujui ( na sina haja ya kukujua) hatuna jinsi ya kuthibitisha uyasemayo. Pengine siku nyingine utakapoongea nao, waeleze kuwa kuna watu wabishi kwa hiyo siku ifuatayo waite press conference ambamo wata'refer' simu waliyopokea kutoka kwa mwanachama maarufu wa JF! Kinachopimwa ni uchangiaji wako wa hoja na jinsi unavyozitetea ndiyo kipimo halisi cha upeo wako. In my opinion, you fall alarmingly short on that score.

Sasa kwa vile naona natumia muda mwingi kupita kiasi humu ndani kulumbana na watu kama wewe, naona nipumzike kidogo na nibaki kuwa msomaji tu. Nimejiunga mwishoni mwa mwaka jana na nikiangalia idadi ya post zangu naona ninaelekea (kama sijafika) kwenye addiction.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kujaribu kuelimisha jamii kutokana na uzoefu wako. Unfortunately, I am one of those hat you have left cold and unimpressed.

I am out of here. God bless.
 
Mkuu Fundi Mchindo,

Naomba uniwie radhi mkuu kama nimekukwaza, hoja zako hapa ni muhimu sana mkuu, na ndio kwanza tulikuwa tumeanza kuchota elimu yako nzito, mkuu niko chini ya miguu yako usitumie hasira mkuu, tena, ninakuahidi mbele ya mashahidi wote hapa Jambo Forums kuwa sitarudia kukuingilia hoja zako mkuu. Usikwazike na mawazo finyu kama yangu mkuu, I know na nimekusikia mkuu nitajitahidi sana kujirekebisha mkuu, lakini please baki mkuu tusingependa Jambo Forums ife mkuu, unajua tena wewe ukitoka mkuu kwa hiyo please usikasirike mkuu, tumia busara!

Ahsante Mkuu.

Wako Mzee Wa Kumkoma Nyani: Super Emergency System, Haki ya mungu I love JF!
 
Tatizo kubwa hapa ni kuruhusiwa kwa sera ya ubinafishwaji katika Tanzania. Hili ndilo mama la matatizo ndani ya nchi yetu.

Tumekurupuka usingizini bila hata ya kupiga mswaki na kudandia sera hiyo chafu ambayo imetumiwa na watu wachache kujitajirisha na kulipotezea taifa mabilioni ya pesa.

Kwa nafasi aliyokuwa nayo Kikwete hawezi akaamka na kusema kuanzia leo nyumba zirudishwe serikalini. Inabidi taratibu na sheria zifuatwe katika hili kama vile kurekebisha hiyo sera ya ubinafishwaji. Kwani kama Raisi atakurupuka katika hili basi itabidi makampuni na mashirika mengi pia yarudishwe tokana na ukweli kwamba yaliuzwa kwa mfano huo huo wa nyumba.

Pamoja na kuwa na kumbukumbu ndogo, lakini nakumbuka moja kati ya ahadi ambazo Kikwete alizitoa pale Dodoma siku aliyokuwa akilamba dume aka kuapishwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema kwamba mikataba yote ya ubinafishwaji itapitiwa tena, na kama kuna utata basi itarekebishwa. Bila shaka alisema hivyo baada ya kusikia kelele na kero za watanzania. Lakini mpaka leo sina uhakika juhudi ya kutimiza ahadi hiyo imefikia wapi.
 
Unanifanya nijisikie sifa kuwa fundi mchundo. Couldn't have said it better!
Natumaini kwa vile msomi mwenzao umesema, watakuelewa!

Fundi Mchundo:

Sawa Fundi. Lakini unafanya kazi nzuri hapa ingawa safari yenyewe bado ni ndefu sana.

Kuna ukweli na siasa. Hapa wengi ni siasa na katika siasa unahitaji point moja iliyo vague na baadaye ku-spin. Katika ukweli inabidi uwe na facts zinazokuwa na data.

Ukweli ni kuwa model ya serikali kuwa na nyumba kwa wafanyakazi wake umepitwa na wakati.

Na tatizo la Mawaziri kuwa hotelini baada ya nyumba kuuzwa sio geni na ni kawaida kwetu kufanya vitu kinyume na utaratibu. Kuna viwanda vingi tu vilijengwa wakati nguvu za umeme hazijulikani zitapatikana wapi. Dodoma umechaguliwa mji mkuu wakati mawasiliano yenyewe yalikuwa ni treni tu.

Na wenzetu wanaofanya mambo yao vizuri wame-refine mambo yao kwa miaka mingi. Na kwa sisi wageni wa uendeshaji wa serikali za kisasa tunaweza kuiga vile vinavyowezekana katika mazingira yetu. Au kuanza upya na kutumia muda mwingi wa ku-refine makosa yetu.

Hivyo tukitaka kuongoa matatizo ya maafisa wa juu kukaa hotelini ni lazima tueleze katika taratibu zetu kuwa ni viongozi gani wa juu wanapewa nyumba. Na siku muda wao unapokwisha basi waondoke na wanaofuatia wachukue nafasi hizo. Tunaweza kuiga kwa Marekani, kwa miaka mingi idadi ya wizara zimebaki zilezile (ukiondoa mabadiliko yaliotokea baada ya september kumi na moja) na rais hana uwezo wa kuanzisha wizara mpya bila mabadiliko ya kikatiba. Hivyo ukubwa wa baraza lao ni karibu lilelile na majengo ni yaleyale. Hivyo mabadiliko ya serikali hayaongezi mahitaji ya nyumba kwa watumishi wa serikali.

Ni rahisi sana viongozi wa Tanzania kuiga jinsi kiongozi wa Marekani anavyotembelea kwenye Limo, F1 au Marine 1 kuliko kuiga mfumo wenye wizara zisizo badilika badilika.
 
Kwa nini aunde kampuni nyingine wakati National Housing ipo? Na nani atakayetoa hiyo subsidy? Ukumbuke kuwa sio kila mfanya kazi wa serikali aliyestahili alikuwa na nyumba. Hata wakati huo, wengi tu walikuwa wakiishi mahotelini. Dawa ni badala ya kugombea hiki kidogo tulichoshindwa kukiendeleza, serikali ingefanya jitihada za kuweka mazingira ambamo watu binafsi, makampuni binafsi na vyombo vya umma vitaweza kujenga nyumba nyingi kwa ajili ya kupanga au kuuza.

Wakati umefika ambapo makazi bora iwe ni haki ya KILA mtanzania na si wafanyakazi wa serikali tu.

FM:

Sasa inabidi wakupe Nobel Prize. Ukweli makazi bora ni haki ya kila mtanzania. Yule mBangladesh alipewa Nobel prize kwa kuona kuwa mikopo ni haki ya watu na alianzisha benki ya mikopo inayowasaidia watu na kubadilisha maisha yao.

Tukiashana na haya mawazo ya makazi bora ni status ya utajiri tunaweza kubadili maisha ya watanzania kuliko kutoa elimu bure.
 
Baada ya serikali kuuza nyumba kwa nini bado inawagharimia watumishi wake kuishi hotelini?

Mimi nilidhani nyumba za serikali zimeuzwa ili kila mtumishi wa serikali ajiju?
unapewa mshahara wako jua wapi utaishi, uwe waziri au katibu wa wizara ni lazima ujiju.

Huu ni wenda wazimu mkubwa kusema serikali za dunia hazihodhi nyumba wakati huohuo sisi bado tunaendelea kulipia gharama za nyumba za watumishi wa serikali?

Haya tena kuna mradi mkubwa wa nyumba zaserikali ulianzishwa mara baada ya kuuza nyumba za serikali. Sasa usemi kwamba serikali haihodhi nyumba ni wa kweli aua MH Field Marshal unatetea policy yenye kila aina ya ukinyonga?

Madilu:

Mbona umeacha kutumia neno lako takatifu SISIEMU.
 
Back
Top Bottom