ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,650
Kama ulidhani ufisadi umekwisha ktk sekta ya maliasili na utalii, fikiria upya. Haijulikani hili lilipangwa bila kujua au la, lakini ukiliangalia kwa jicho la tatu utagundua kuwa 'dili' za ufisadi bado zinaendelea kuchezwa tena kwa ustadi mkubwa.
Kwa kuzitumia benki za EXIM na CRDB wizi mkubwa umeendelea kufanywa kupitia sekta ya utalii. Hebu tujiulize inaingiaje akilini kwa nchi masikini kama TZ kuendelea kuzikarimu benki tajwa hapo juu kuchukua dola 5 kwa kila dola 30 zinazolipwa na watalii wanaotembelea mbuga zetu za Taifa? Hili limefanyika kwa maslahi ya watanzania au ndo mtindo ule ule wa 10% tulouzoea? Haiingii akili kwani kwa style hii ni wazi benki husika zinavuna kiasi kikubwa cha hela bila kuzifanyia kazi.
Habari za awali zinaonyesha kuwa huu ni mkakati maalumu uliopangwa na 'wakuu' ili kufanikisha wizi wa rasilimali za nchi kutoka maliasili zetu kwani ilionekana ni ngumu sana kufanya ufisadi kupitia uwindaji au usafirishaji wa wanyama hai kwa kuwa huko wananchi walizinduka zamani. Inaelezwa kwamba kati ya hizo dola 5 kwa kila kichwa kinachoingia mbugani, ni kiasi kidogo sana kinachoingia kama mapato ya benki kwa kuingia kwao mkataba na serikali. Sehemu kubwa ya hizo dola 5 (kati ya dola 3.5 na 4), zinaingia mifukoni mwa wakubwa 'mafisadi' wanaoendelea kuitafuna nchi hii na mfumo mzima wanaoutumia.
Ama kweli 'haka kanchi katamu kama ukikapatia', mweeeeh!