Bora Fisadi Aliyeleta Unafuu wa Maisha kwa Watu Kuliko Mwadilifu Ambaye Kila Siku Watu Wanalia Ugumu wa Maisha.

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,892
3,196
Enzi hizo zinazodaiwa za ufisadi:
-maisha yalikuwa rahisi
-hakukuwa na mfumko wa bei
-dola zilikuwepo za kutosha tena kwa bei inayojulikana
-watu wengi walijenga
-ajira zilikuwepo za kutosha
-miundombinu mingi ilijengwa zikiwemo barabara tena kwa kiwango cha lami
-shule nyingi za kata zilijengwa
-huduma za kijamii zilikuwa rahisi

Leo hii pasipokuwa na ufisadi:
-mfumko wa bei uko katika kilele!
-maisha magumu, kila siku bora jana!
-changamoto ya upatikanaji huduma
za kijamii
-benki karibia zote na sehemu za kubadilishia fedha kwa sasa hakuna dola!
n.k

Hitimisho:
Bora kuongozwa na fisadi anayejua kutafuta na kuleta unafuu wa maisha kwa walio wengi, kuliko kuongozwa na anayejiita/kuitwa muadilifu ambaye ni mzembe na asiyejua kutafuta au kulinda rasilimali za nchi na ambaye hawezi kuleta unafuu wa maisha kwa watu wake.
 
Sasa ukifika wakati wa uchaguzi na kupiga kura, usipaishe penati...
 
Huyu Mama ndio kaitoa sukari 1600 kilo hadi 4500,kaitoa petrol 1800 wakati wa Magufuli hadi 3,400 Leo hii,huyu Mama kautoa Mchele 1,200 kilo wakati wa Magufuli hadi 4,000 kilo hivi Leo,huyu Mama kayatoa maharage 1,200 kilo hadi 2,600 kilo ,huyu Mama kaitoa nyama 6,000 kilo hadi 10,000 huyu Mama kaitoa Dola 2,290 wakati wa Magufuli hadi 2,800 leo.
 
Magufuli kararibuje nchi fafanua
Nchi hii sekta binafsi ndiyo mwajiri mkuu na ndiko wananchi wanapata ustawi wa maisha.
Magufuli ndiye aliua kampuni nyingi watu wakarudi kijijini kulima kwa jembe la mkono (yaani walirudi kwenye u primitive)
Wengine waliobaki mjini wakageuka matapeli, ndio ambao kazi yao kubwa ni kutengeneza account za maudhui ya ngono na kusema wanatoa uroda au kukonekti watu kwenye magroup Ili wapate pesa.
Kwa akili za Kiafrika itachukua miaka mpaka 14 kufanya reform ya uharibifu wa Magufuli wa miaka 7.
 
-dola zilikuwepo za kutosha tena kwa bei inayojulikana

-benki karibia zote na sehemu za kubadilishia fedha kwa sasa hakuna dola!
n.k
Screenshot_20230430-113713.png
 
Nchi hii sekta binafsi ndiyo mwajiri mkuu na ndiko wananchi wanapata ustawi wa maisha.
Magufuli ndiye aliua kampuni nyingi watu wakarudi kijijini kulima kwa jembe la mkono (yaani walirudi kwenye u primitive)
Wengine waliobaki mjini wakageuka matapeli, ndio ambao kazi yao kubwa ni kutengeneza account za maudhui ya ngono na kusema wanatoa uroda au kukonekti watu kwenye magroup Ili wapate pesa.
Kwa akili za Kiafrika itachukua miaka mpaka 14 kufanya reform ya uharibifu wa Magufuli wa miaka 7.
Una hoja usikilizwe
 
Back
Top Bottom