Ufisadi wa Karume wazanzibari watalaumu wabara kama walivyozoea?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Kumbe na Karumeni fisadi!

Rais mstaafu wa Zanzibar, AmaniAbeid Karume

Rais mstaafu wa Zanzibar, AmaniAbeid Karume, amekumbwa na kashfa akidaiwa kutoa amri ya kukodishwa kwa majengoya Mambo Msiige bila kufuata utaratibu na sheria.

Tume iliyoundwa na Baraza laWawakilishi Zanzibar kuchunguza pamoja na mambo mengine, ukodishaji wa ardhi namajengo ya Serikali, imebaini Mambo Msiige ilikodishwa kwa miaka 99 thamani yadola za Marekani milioni 1.5 kinyume cha sheria

Kwa mujibu wa Ripoti ya Uchunguziwa kamati hiyo iliyoongozwa na Mwakilishi wa Chakechake, Omar Ali Shehe,majengo hayo yalikodishwa kwa Kampuni ya ASB Holdings Limited kupitia taratibuambazo hazikuzingatia maslahi ya Taifa.

Ripoti ya kamati hiyo inaonyeshakuwa ukodishwaji huo ulifanyika baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu)Dk Mwinyihaji Makame Mwadini, kupewa agizo na Rais Karume (mstaafu) kwamaandishi.

"Dk Mwinyihaji aliiambia kamatikuwa yeye ndiye aliyepokea agizo kwa wino mwekundu kutoka kwa Rais naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume kuwa Serikali imepatamwekezaji kampuni ya ASB Holdings Ltd, "sehemu ya ripoti hiyo ilikariri maelezoya Waziri Mwadini alipohojiwa na kamati hiyo.

Kwa mujibu ripoti hiyo, DkMwadini aliiambia kamati kuwa Rais aliagiza kampuni hiyo ikodishwe kwa mkatabawa malipo ya Dola milioni 1.5 na kulipa kiasi cha Dola 10,000 kwa mwaka.

Kwa agizo hilo, Dk Mwadinialimwandikia barua Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na uchumi Zanzibar akimwarifukupokea fedha kutoka kwa mwekezaji huyo ili aweze kujenga hoteli ya nyota tanona kwamba baada ya kupokea malipo hayo afungue akaunti maalum ya kutunza fedhahizo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ripotihiyo, Dk Mwadini alipotakiwa kutoa mbele ya kamati ushahidi wa agizo la raisalikataa na kusema kutoa dokezo la rais ambalo limeandikwa kwa wino mwekundusiyo sawa.

"Mpaka wakati huu tunawasilisharipoti hii agizo la maandishi kutoka kwa rais halikutolewa na Dk Mwadini mbeleya kamati ya uchunguzi." Kwa mujibu wa ripoti hiyo yenye kurasa 224.

Hata hivyo, ripoti hiyo imesemakwamba pamoja Kamati hiyo kumtaka Katibu wa Baraza kumwandikia Barua ya Desemba8, mwaka 2011 ya kumtaka kuwasilisha ushahidi wa agizo la Rais mstaafuameshindwa na kuendelea kutetea msimamo wake kuwa ni "Siri ya serikali."


Kamati hiyo ya uchunguzi imebainikuwa nyaraka za mpango wa ukodishwaji majengo na ufukwe wa Shangani zimepoteaWizara ya Ardhi, makazi, Maji, na nishati katika mazingira ya kutatanisha.

" Katika mafaili ya Ofisi hakunahata barua ya maombi ya ukodishwaji yaliyofanywa na mwekezaji mwenyewe, kwaufupi hata faili lenye kumbukumbu za "Lease' ya majengo ya Mambo Msiige naStarehe Club halipo." Imeeleza Ripoti hiyo.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

 
Back
Top Bottom