Ufisadi wa CCM na Kujitanua kwa Clouds FM!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Nilikuwa na washikaji wakati tunajadili issue za pilitik, ikaja suala la miropoko inayotolewa na Mtangazaji mmoja wa clouds fm ambaye wengi tunamjua. Wakati mjadala unaendelea jamaa mmoja akatueleza kwamba kwa kuwa hii redio imekuwa mstari wa mbele kupitia huyo mtangazaji kuipandisha chati ccm, eti ccm imeamua kuifadhili ili iweze kujitanua sawasawa ikiwezekana mikoa yote.

Lengo la ccm kutoa huo ufadhili kwa hii redio ni kuhakikisha kwamba ikifika 2015 iweze kutumika katika kampeni zake. Hii imetokana na redio husika kusikilizwa na watu wengi tofauti na redio uhuru ambayo imekosa umaarufu na wasikilizaji wa maana. Hii inatokana na ukweli kwamba redio hii imekuwa mstari wa mbele kukisemea ccm, ingawa redio yenyewe sio ya chama.

Wajemeni ni ngumu sana kwa haka kanchi kupata maendeleo maana ingawa tuko ktk mwaka wa pili tangu uchaguzi mkuu, watu wameshaanza kuandaa mashambulizi, ili hali watz bado tupo katika lindi la umasikini.
 
Sidhani kama hii Redio ina maslahi ya Kudumu na CCM. Watu wengi walianza kuihusisha na chama hicho hasa baada ya mtangazaji wake kuwa mbunge wa Viti Maalum (Marehemu Amina-RIP). Ninachokijua ni kuwa hawa jamaa, hasa familia ya mmiliki wake (Joseph Kusaga) wana maslahi ya kudumu na J.K. Haya wanayoyafanya sasa nikuwahadaa wananchi ili waipende Serikali ya J.K kwani chuki zidi ya serikali yake inazidi kukuwa kila kukicha kutokana na matendo yake. Ila hakuna lisilowezekana mbele ya pesa

Halafu mkuu hii habari haina hadhi ya News Alert, labda ungeiita Tetesi
 
Watanzania si mabwege siku hizi! Watafulia hao

Wanajidanganya wenyewe. Kusikilizwa sana siyo kukubaliwa kwa kila wasemalo. Hata gazeti la Rai lilisomwa sana lakini maggamba walipolichukua unaona mwenyewe wasomaji nao wamehama. So maggamba ni kama mfa maji, siku zao zinahesabika.
 
Mkuu ndyoko ni kweli hii radio siku hizi ndio imekuwa mtetezi wa serikali JK na chama chake sasa hivi inaanza kupoteza umaarufu wake. Labda nikutoe wasiwasi hata waitumie vipi hawatafanikiwa hata kidogo CCM imechokwa
 
Sidhani kama hii Redio ina maslahi ya Kudumu na CCM. Watu wengi walianza kuihusisha na chama hicho hasa baada ya mtangazaji wake kuwa mbunge wa Viti Maalum (Marehemu Amina-RIP). Ninachokijua ni kuwa hawa jamaa, hasa familia ya mmiliki wake (Joseph Kusaga) wana maslahi ya kudumu na J.K. Haya wanayoyafanya sasa nikuwahadaa wananchi ili waipende Serikali ya J.K kwani chuki zidi ya serikali yake inazidi kukuwa kila kukicha kutokana na matendo yake. Ila hakuna lisilowezekana mbele ya pesa Halafu mkuu hii habari haina hadhi ya News Alert, labda ungeiita Tetesi
Kuna uwezekana mimi au wewe mmoja wetu akili yake haiko sawa juu ya ufahamu wa neno 'news alert'. Ngoja niwasiliane na bakita pengine walinipotosha!
 
Mkuu ndyoko ni kweli hii radio siku hizi ndio imekuwa mtetezi wa serikali JK na chama chake sasa hivi inaanza kupoteza umaarufu wake. Labda nikutoe wasiwasi hata waitumie vipi hawatafanikiwa hata kidogo CCM imechokwa

noted with lots of thanx!
 
Kuna uwezekana mimi au wewe mmoja wetu akili yake haiko sawa juu ya ufahamu wa neno 'news alert'. Ngoja niwasiliane na bakwata pengine walinipotosha!

Penye nyekundu inahusiana vipi na Lugha?
 
Nilisha achaga kuisikiliza hii radio toka 2009,ila kama mikakati yao ndio hiyo ndio wanajichimbia kaburi na kujizika rasmi kwenye medani ya vyombo vya habari
 
Hizo zilikuwa ni porojo zenu kijiweni ili kusukuma weekend. Kwani Radio Clouds si ya mtu binafsi na huyu mtu si hazuiliwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa anachokitaka? sasa hapa cha ajabu ni kipi? Acheni hizo bana.
 
Nilisha achaga kuisikiliza hii radio toka 2009,ila kama mikakati yao ndio hiyo ndio wanajichimbia kaburi na kujizika rasmi kwenye medani ya vyombo vya habari

Kupanga ni kuchagua na wewe si mtu pekee utakaye leta ustawi wa Clouds Radio.
 
Ni kweli clouds sasa hizo ndo biashara zake lkn usihofu mkuu watu wa maana mijini na vjjni wataishit tu hiyo.hakuna aliyegemea radio uhuru itakuwa hivi ilivo leo!
 
Sidhani kama hii Redio ina maslahi ya Kudumu na CCM. Watu wengi walianza kuihusisha na chama hicho hasa baada ya mtangazaji wake kuwa mbunge wa Viti Maalum (Marehemu Amina-RIP). Ninachokijua ni kuwa hawa jamaa, hasa familia ya mmiliki wake (Joseph Kusaga) wana maslahi ya kudumu na J.K. Haya wanayoyafanya sasa nikuwahadaa wananchi ili waipende Serikali ya J.K kwani chuki zidi ya serikali yake inazidi kukuwa kila kukicha kutokana na matendo yake. Ila hakuna lisilowezekana mbele ya pesa

Halafu mkuu hii habari haina hadhi ya News Alert, labda ungeiita Tetesi
Binafsi najua akina Kusaga walipotoka mpaka kufikia hata hao CCM kuona umuhimu wao.wamepigana sana toka zama zile kule mwenge! Walipendwa kama watu wa burudani na ukitaka burudani lazima utafute walipo hawa! Pengine Kusaga hajui au anapotoshwa hali halisi mtaani.Sura ya Clouds machoni mwa watu si ile tena! Vijana wanaanza kuwachukia dhahiri kabisa kwa kujihusisha na siasa za ccm! Wanafaidi nafasi wanazopata now lakini mwisho wake si mzuri hasa unapo deal na wanasiasa! Wajiangalie upya na kutengeneza policy zitazowaongoza waachane na siasa! Wengine tunaona nchi inapoelekea wakae mbali upepo usije kuwabeba na wao! Kusaga umerusha sana mateke usikubali watu wakutumie kwa faida ya muda mfupi!
 
Clouds FM mbona aina matatizo yaani kuhubiri amani ndiyo tatizo au mnataka ifanye kazi kama zile radio za Rwanda au Kenya.
 
Clouds FM mbona aina matatizo yaani kuhubiri amani ndiyo tatizo au mnataka ifanye kazi kama zile radio za Rwanda au Kenya.

Clouds kama radio hawana tatizo, tatizo ni hao watangazaji wao wasiokuwa na shule ukimwondoa milad ayo labda kidogo na regina mwalekwa wengine wote ni hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom