Ufisadi tena: EWURA walipandisha bei ya mafuta kufidia chaguzi za CCM!

Uwe na uhakika na taarifa unazotoa! Unasema wiki mbili zilizopita ndio bei ya mafuta ilipanda..una uhakika na taarifa yako? Bei zinabadilika kila mwanzo wa mwezi ndio Ewura wanatangaza bei elekezi..sasa unapotengeneza hoja kuwa bei ilipanda kwajili ya chaguzi za ccm wiki mbili zilizopita ni uzushi ambao huwezi hata kuutetea! Huna hoja tafuta hoja nyingine!

hata kama zimepanda jana ukweli utabaki kwamba zimepanda kufadhiri uchaguzi wa CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Kwenye utaalaam acheni politics weka hizo data zako hapa nasi tukwambia ukweli

Mafuta yalipanda ili kufidia loss walizopata makapuni ya mafuta miezi miwili mitatu iliyopita baada ya mafuta kuja kwa wingi.

Take my word, mafuta yatendelea kushuka bei kwa sababu hizi

Kuanzia mwezi huu/ujao wameongeza/wataongeza uwezo wa upakuwaji wa mafuta bandarini ambayo itapunguza sana demorage cost

Hiyo ni sababu moja tu, lete data zako niendele kukujibu!!!

Makampuni ya mafuta yamewekewa 'kinga' ya kupata hasara ??
 
ukweli utabaki kuwa ukweli!

ni wazi kuwa kada wa ccm haruna masebu, ambaye ni mkurugenzi wa ewura yuko kazini kisawa sawa, masebu ambaye akiwa mkufunzi wa chuo cha ardhi wakati ule, alikuwa pia ndiye katibu wa ccm tawi la chuo cha ardhi na swahiba mkuu wa lowasa. lowasa alivyochaguliwa mara ya kwanza kuwa waziri wa ardhi, jambo la kwanza lilikuwa ni kumteua masebu kuwa mkurugenzi mkuu wa national housing, baadaye PSRC na sasa EWURA.

wiki mbili zilizopita ewura ilitangaza ongezeko la bei ya mafuta kwa kiasi kikubwa, ongezeko hilo lilikuwa ni makubaliano kati ya mtu huyu na makampuni makubwa ya kifisadi ya mafuta na mkumbuke kuwa chaguzi za ccm nazo zilianza wiki mbili zilizopita. makampuni hayo yalikuwa yanatoa kama shs 100/- kwa kila lita ya mafuta hayo kufidia au kugharamia chaguzi za ccm

chaguzi za ccm zinakaribia kumalizika, na kwa kuwa ewura wanaogopa kuumbuka, leo wametangaza kushusha bei za mafuta karibia na ile bei iliyokuwepo kabla ya kupandisha kupata fedha za kufidia chaguzi za ccm.

ewura waje hapa wakane taarifa hii, nitawapa data toka yanakoagizwa mafuta , na hali ya mafuta nchi jirani za soko la pamoja la afrika mashariki.

ni vema pia kwa hujuma hii mkajua masebu ni ani katika nchi hii, ambapo uraia wake ukweli ni toka nchi ya rwanda

solurce" wazalendo ndani ya ewura

validity 90%
 
Dah hiki chama chetu cha kijani kitatufukisha tukiwa tumechoka huko tunakotaka kwenda kama hali ndio hii,maana haiwezekani matumizi ya chama yatokane na jasho la wananchi kila kukicha mara utasikia bei elekezi kumbe zinaenda kusaidia uendeshaji wa chama inasikitisha kwa kweli.Mbona chama kiko na vitega uchumi lukuki wanashindwa kuwa wabunifu kujiongezea vipato kutoka kwenye hivyo vitega uchumi vyao ndio maana kuna kauli za baadhi ya viongozi kama kuwa chama kitatawala milele kumbe ni kutokana na mambo kama haya inasikitisha kwakweli.
 
Kwa utaratibu huu, na kwa gharama yoyote, mafisadi watahakikisha CCM haiondoki madarakani.
 
Kumbe bado chama kinashika hatamu!
Ninachojiuliza ni kwamba hizi Regulatory bodies zinadhibitiwa na nani?
hizo zinazibitiwa na mafisadi wachache kupitia viongozi wa magamba kwa mkono wa serikali ya magamba
 
Mtandao huu umekuwa wa kipumbavu kama unaruhusu watu wanaofikiria kutumia masaburi waweke Uzi wa kutukana watu wanaosaidia nchi. Hizi bei hutolewa kila Jumatano ya kwanza ya mwezi. Mtu HUMU hata hajui anadai inatolewa kila wiki mbili. Mbili mchango ya CCM kama inatolewa kama Alivyodai wasingewashitaki ewura kama ulisoma magazeti

Generally wanaochangia mtandao huu kwa sasa ni watu wasiotumia ajili
 
Nakupongeza kaka kwa taarifa hiyo but ulifanya kosa kukaa kimya mpaka dakika za mwisho tena wanapoanza kushusha bei ndo unakuja na issue hiyo,huoni kama tayari tumeshaibiwa??????????????
WatanzaniatTutaibiwa sana tusipoangalia. Na kwa kweli LOWASSA AKIWA RAISI NDO TUTAIBIWA MPAKA KIBOGA TUSIPOANGALIA.
 
Tujadili hoja kwa uelewa kama mtandao huu ulivyokuwa unsheshimika huko nyuma. Hivi inaingia akilini watu hao hao waishitaki ewura kwa kupunguza bei ( soma magazeti ya jumatatu ) halafu wakae meza moja kuisaidia CCM? Tusitumie masaburi kufikiri kama aliyeketa Uzi huu. Bei ewura inatangaza kila Jumatano ya kwanza ya mwezi na si kila wiki mbili kama alivyodai mchangiaji mmoja ambaye naye nadhani anatumia masaburi kufikiri. Hebu tufikiri ni bidhaa
 
Tujadili hoja kwa uelewa kama mtandao huu ulivyokuwa unsheshimika huko nyuma. Hivi inaingia akilini watu hao hao waishitaki ewura kwa kupunguza bei ( soma magazeti ya jumatatu ) halafu wakae meza moja kuisaidia CCM? Tusitumie masaburi kufikiri kama aliyeketa Uzi huu. Bei ewura inatangaza kila Jumatano ya kwanza ya mwezi na si kila wiki mbili kama alivyodai mchangiaji mmoja ambaye naye nadhani anatumia masaburi kufikiri. Hebu tufikiri ni bidhaa ipi iliyowahi kutangazwa kupunguzwa bei Kama si mafuta? Angalia sukari instill wa hapa
 
Ndachuwa, makampuni makubwa ya mafuta yanamilikiwa na nyie wenyewe magamba Dalbit, Lake Oil nk.) mtashindwa kuhamisha mipesa yenu kutoka mfuko wa suruali kwenda mfuko wa koti?
Ndyali mimi hata kiwanja kimoja kilichopimwa sina kwa nini kuniweka kwenye kundi la mafisadi?
 
Last edited by a moderator:
Kuna hesabu zake zinapigwa kitaalam, na pakuifidia loss panaonekana ....
hapo kwenye red ndio upuuzi unaotumika kuwaibia wananchi mitaani na sio humu jf,..tuambie hiyo aina ya utaalam na sio blahblah
 
Whatever the veracity, validity or source of this news, I still would buy something from it.

Ufisadi kupitia taasisi za serikali kwa manufaa ya CCM ni mkubwa na wa muda mrefu. BOT, TRA, TPA, NSSF, PPF, TCRA na Wizara ya Madini kwa mifano michache tu vimewahi/vimekuwa vikitumika kwa manufaa ya CCM kuliko hata Taifa na wananchi kwa ujumla.

Mimi nawaambia ndugu zangu; siku CCM inaondoka madarakani haya tunayoyaona na kuyasikia leo tutayaona ni cha mtoto....tone tu. Ziko scandal na scums za tsunami proportion ktk mfumo wa uendeshaji wa hii nchi we basi tu. Sometimes the lesser you know the better!

Tuendelee kutega masikio na kufungua macho yetu tu
 
jamani wananchi tutaendelea kulalamika mpaka lini? Hivi kwa wasomi tuliopo sasa hapa tz hatutoshi kuchukua hatua tukawawakilisha wale wasiojua nchi inavyofisidiwa kila siku! So sad!
 
Mwikimbi, kama uko ndani ya ewura lete data na proof ya unayoandika. Kama sivyo, unatumia mtandao wa JF vibaya kwa kuzusha uongo. Unaharibu sifa ya JF kuwa ya Great Thinkers. Unatufanya woote tunaosoma na kukusapoti kuwa wapumbavu tusioshughulisba bongo zetu. Masebu angepa ndisha bei kiholela bila kuzingatia ile formula ungeshindwa kujua? Si ile formula iko mtandaoni kila mtu anaweza kujua bei halisi ni ipi?
 
Back
Top Bottom