Ni kweli mkuu, na mwaka mmoja baada ya kifo chake, ziliibuka taarifa kuwa Nyimpine ameonekana nchini Ureno na taarifa hizo ziliambatana na ukweli kwamba hata mama yake alikuwa na safari za mara kwa mara za kwenda nchini humo kiasi kwamba watu wakaziamini taarifa hizo, kwamba huenda zilikuwa na lengo la kumtembelea mwanaye huyo. lakini hata hivyo ilikuja kuonekana ni uvumi tu na mtoa taarifa hakupata kufahamika.Hii stori nilipata kuhadithiwa na Rafiki yangu Raia wa Msumbiji, inasemekana hata kifo cha Nyampine kina mkono wa Babake na Vigogo wengine ambao walifahamu fika kuwa Nyampine hakuwa na namna ya kukwepa hukumu na hivyo kuwepo uwezekano mkubwa wa dili zao nyingine kuibuliwa kwenye kesi zilizokuwa zinamkabili Nyampine. Hivyo njia rahisi ilikuwa ni Mtuhumiwa kufa ili kesi dhidi yake zifutwe.